Ni muda wa serikali kukaribisha wawekezaji kwenye barabara zetu

Ni muda wa serikali kukaribisha wawekezaji kwenye barabara zetu

Lunovar

Member
Joined
Mar 26, 2022
Posts
11
Reaction score
31
Kiukweli mi naona kwenye swala la maendeleo ya barabara katika nchi hii serikali imeshindwa kabisa. Barabara nyingi nchini na muhimu kwa ustawi wa uchumi wa nchi ni mbovu kupita maelezo na cha ajabu unakuta ndio barabara ambazo hata viongozi hutumia kwenda kwenye shughuli zao.

Nitolee mfano wa barabara kuu(highway) inayotokea mwanza mpaka Lamadi, Lamadi mpaka Bariadi. Hii barabara inahatarisha usalama wa mtu na mali yake, kuna pia barabara ya Singida, n.k. Na kinachoshangaza ni kuwa TANROAD hashitakiwi kwa ubovu wa barabara ila wewe unashtakiwa kwa ubovu wa gari uliosababishwa kwa ubovu wa barabara.

Kwa mtazamo wangu naona ni bora wakakubali wawekezaji kama ilivyofanya kwenye mwendokasi.

Mwanajamii unamaoni gani kuhusu hili?
 
Wakikaribisha wawekezaji watoe na matozo yao ya kujenga barabara kuanzia bandarini hadi kwenye mafuta
 
Then wakiingia wawekezaji mjiandae na toll/peages/tozo..Jana tulikuwa na mjadala humu kwenye thead moja hivi watu wanalalamikia Bridge Toll ya buku jero pale Kigamboni,nikawaambia heri Toll ya hapo ni buku jero Congo DRC umbali wa km 500 tu unakutana na Toll gates zaidi ya saba na zote ni kuanzia dola 50$ nyingine mpk 300$..Hiyo yote ni kwasababu wawekezaji wamejenga madaraja na barabara hivyo wanakusanya chao..
 
Ni utaratibu mzuri tu utengenezwe maana lengo kuu ni ustawi wa mwananchi na uchumi wa nchi sio kwa kukomoa mwananchi kwa manufaa ya mtu binafsi

Back
Top Bottom