Ningependa nichangie kwenye hilo kama ifuatavyo:-
Matumizi ya kompyuta/au kifaa chochote chenye access na internet ni muhimu sana katika maisha yetu ya sasa ukizingatia umuhimu wa taarifa zilizopo kwenye mtandao.
Kwa upande wa chuo kikuu; uwa kuna kazi mbalimbali ambazo ili zifanyike uhitaji uwepo wa kompyuta. Kazi zenyewe ni kama ufanyaji wa assigments, utafutaji wa materials mbalimbali na mara nyingine Lecturers utoa notes katika mfumo wa "soft copies" so its essential uwe na laptop ili ikuwezeshe kuifadhi notes hizo kwani itakupunguzia gharama za kwenda ku-print ili ziwe hard copy.
Kwa upande mwingine, kuna baadhi ya taaluma ambazo zinalazimu mwanachuo kuwa na kompyuta, mfano taaluma kama Computer engineering, Computer Science, Telecommunication, Information technology, Information system management n.k, hizi taaluma zinamlazimu msomi wake awe na laptop kwa kuwa kompyuta uwa ni sehemu ya taaluma hizo kwa kiwango kikubwa.
Mbali na umuhimu wa matumizi ya kompyuta pia ningependa kutoa tahadhari kwa watakao miliki kompyuta wawapo chuoni, kwa lengo jema tu. Kama tujuavyo, jambo lolote lina faida na hasara yake, hivyo hivyo kwenye kompyuta. Kipindi nilipokuwa chuo, kuna watu wakapata boom na kununua laptop haraka, jambo lililo wakuta ni kupoteza muda wao mwingi kutazama movies na mara nyingine ikapelekea mpaka kupotezea vipindi darasani. Hili lizuie kwa namna yoyote ile, lina madhara.
Yangu ni hayo.