ni muhimu kuwa na laptop kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza?

donMramba

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2013
Posts
250
Reaction score
42
wakuu nisaidieni kwenye hili jambo,ni lazima niwe na pc nitakapoanza masomo chuoni?
 
Mambo dear. Leo utakuja tena pande hizi...mmekumiss mwaya!..laptop ya nn na wewe jaman.....kusoma bongooo...ntumie vocha basi simu yangu haina crdt
 
Ningependa nichangie kwenye hilo kama ifuatavyo:-

Matumizi ya kompyuta/au kifaa chochote chenye access na internet ni muhimu sana katika maisha yetu ya sasa ukizingatia umuhimu wa taarifa zilizopo kwenye mtandao.

Kwa upande wa chuo kikuu; uwa kuna kazi mbalimbali ambazo ili zifanyike uhitaji uwepo wa kompyuta. Kazi zenyewe ni kama ufanyaji wa assigments, utafutaji wa materials mbalimbali na mara nyingine Lecturers utoa notes katika mfumo wa "soft copies" so its essential uwe na laptop ili ikuwezeshe kuifadhi notes hizo kwani itakupunguzia gharama za kwenda ku-print ili ziwe hard copy.

Kwa upande mwingine, kuna baadhi ya taaluma ambazo zinalazimu mwanachuo kuwa na kompyuta, mfano taaluma kama Computer engineering, Computer Science, Telecommunication, Information technology, Information system management n.k, hizi taaluma zinamlazimu msomi wake awe na laptop kwa kuwa kompyuta uwa ni sehemu ya taaluma hizo kwa kiwango kikubwa.

Mbali na umuhimu wa matumizi ya kompyuta pia ningependa kutoa tahadhari kwa watakao miliki kompyuta wawapo chuoni, kwa lengo jema tu. Kama tujuavyo, jambo lolote lina faida na hasara yake, hivyo hivyo kwenye kompyuta. Kipindi nilipokuwa chuo, kuna watu wakapata boom na kununua laptop haraka, jambo lililo wakuta ni kupoteza muda wao mwingi kutazama movies na mara nyingine ikapelekea mpaka kupotezea vipindi darasani. Hili lizuie kwa namna yoyote ile, lina madhara.

Yangu ni hayo.
 
hahahahahahahaha weeeeh vocha me mama yako,
 
wakuu nisaidieni kwenye hili jambo,ni lazima niwe na pc nitakapoanza masomo chuoni?

Muhimu kama unasoma kozi hizi hapa 1.engineering 2.law 3.medicine 4.architecture 5.accounting&finance,, zaidi ya hapo nunua labda ya kulogin facebook
 
N muhmu hasa kwa kuangalia yale mambo ya wakubwa,hasa kama cku hio hauna pindi au pepa ikikukamata
 
Ningependa nichangie kwenye hilo kama ifuatavyo:-

Matumizi ya kompyuta/au kifaa chochote chenye access na internet ni muhimu sana katika maisha yetu ya sasa ukizingatia umuhimu wa taarifa zilizopo kwenye mtandao.

Kwa upande wa chuo kikuu; uwa kuna kazi mbalimbali ambazo ili zifanyike uhitaji uwepo wa kompyuta. Kazi zenyewe ni kama ufanyaji wa assigments, utafutaji wa materials mbalimbali na mara nyingine Lecturers utoa notes katika mfumo wa "soft copies" so its essential uwe na laptop ili ikuwezeshe kuifadhi notes hizo kwani itakupunguzia gharama za kwenda ku-print ili ziwe hard copy.

Kwa upande mwingine, kuna baadhi ya taaluma ambazo zinalazimu mwanachuo kuwa na kompyuta, mfano taaluma kama Computer engineering, Computer Science, Telecommunication, Information technology, Information system management n.k, hizi taaluma zinamlazimu msomi wake awe na laptop kwa kuwa kompyuta uwa ni sehemu ya taaluma hizo kwa kiwango kikubwa.

Mbali na umuhimu wa matumizi ya kompyuta pia ningependa kutoa tahadhari kwa watakao miliki kompyuta wawapo chuoni, kwa lengo jema tu. Kama tujuavyo, jambo lolote lina faida na hasara yake, hivyo hivyo kwenye kompyuta. Kipindi nilipokuwa chuo, kuna watu wakapata boom na kununua laptop haraka, jambo lililo wakuta ni kupoteza muda wao mwingi kutazama movies na mara nyingine ikapelekea mpaka kupotezea vipindi darasani. Hili lizuie kwa namna yoyote ile, lina madhara.

Yangu ni hayo.

mkuu umesomeka sana na asante sana kwa ushauri wako mzuri naamini utakuwa umenisaidia mimi na wengine wengi humu ndani asante sana
 
Muhimu kama unasoma kozi hizi hapa 1.engineering 2.law 3.medicine 4.architecture 5.accounting&finance,, zaidi ya hapo nunua labda ya kulogin facebook

me naenda kusoma accounting na sina uwezo wa kuwa na laptop kwa sasa nategemea boom,je itasababisha kufanya vibaya kwny masomo?
 
Katika ulimwengu huu ni jambo la lazima kuwa na laptop, kozi yoyote ile utakayosoma ni lazima kuwa na komputer, materialS na tutorialS nyingi zipo kwenye net, ni matumaini yangu kuwa huitaji kuuliza mtu, afadhali usiwe na nguo nzuri, lakini vifaa vyako kwa ajili shule viwe vimetimia. NUNUA LAPTOP YAKO HARAKA!!, usipoteze muda. LAPTOP NI LAZIMA!!!!!
 
tatizo uchumi unabanaaaaaaaaaaaaa
 
hapana co muhimu kuwa na laptop lakini desktop ni muhimu sana usiache.
 
Back
Top Bottom