Ni mwana Simba SC mwenye roho mbaya na ya kichawi ndiyo hatolifurahia 'Classic Goal' la Stephane Aziz Ki

Ni mwana Simba SC mwenye roho mbaya na ya kichawi ndiyo hatolifurahia 'Classic Goal' la Stephane Aziz Ki

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Kama mwana Simba SC ni goli ambalo limeniuma kwani amesawazisha ila kiuanamichezo na hasa nikiwa kama mdau wa soka GENTAMYCINE, nisiwe mnafiki na naomba niseme tu kuwa ni goli zuri hakuna mfano. Kwani alijiseti vyema kabisa na kunipigia 'muwa' wa maana ulioenda kule kule anakotagia mayai ndege.

Sijui Simba SC yangu (hasa Mwekezaji Mo Dewji) alishindwa nini na wapi kumpata huyu kiungo mshambuliaji raia kutoka nchini Burkina Faso Stephane Aziz K? Kwani kwa kipaji chake na uwezo wake angetua Simba SC na kukutana na mafundi tupu akina Chama, Phiri na Okra, nina uhakika hivi sasa tungekuwa tunasema mengine.

Hongereni Yanga SC kwa kuwa naye.
 
Kuna mtu kidogo afie uwanjani dadadeki
FB_IMG_1666563464649.jpg
 
Ninacho sisitiza ni Kamati ya saa sabininambili ichukue hatua za kinidhamu dhidi ya Chama Kwa kitendo chake Cha kumkanyaga Aucho Kwa maksudi akiwa Hana mpira na refarii hakuweza kumchukulia hatua yoyote ya kinidhamu.
Matumaini Bodi ya Ligi hawata liacha Ili lipite.
 
Goli zuri sana ila ukiondoa goli alikua kapotea uwanjani. Okrah had a good game ila ubinafsi umefanya aonekane wa kawaida tu mwehu yule.

Ule Mgoli wa Aziz Ki ni mwana ukome
 
kwa hiyo azizi ki kuifunga simba leo ndio kawa bora. tuambie kaonekana wapi zaidi ya lile goli. mbona hakuwavusha yanga kwenda group stage. kama unae chama ki wanini. acha kwenda na matukio kama upepo
Kwani asist kwenye ngao ya jamii nani alitoa kamq sio aziz ki, mchezaji muhimu uamua mechi muhimu inapotokea ajafanya ivyo inakuwa ni bahati mbaya na ndo mpira sio kila mara utaamka vizuri
 
Ninacho sisitiza ni Kamati ya saa sabininambili ichukue hatua za kinidhamu dhidi ya Chama Kwa kitendo chake Cha kumkanyaga Aucho Kwa maksudi akiwa Hana mpira na refarii hakuweza kumchukulia hatua yoyote ya kinidhamu.
Matumaini Bodi ya Ligi hawata liacha Ili lipite.
Mkuu kama unafatilia mpira ile haikuwa makusudi ndio maana refa aliiona lakini hakutoa kadi, nakuhakikishia chama hatopata adhabu yoyote
 
Back
Top Bottom