Ni mwana Simba SC mwenye roho mbaya na ya kichawi ndiyo hatolifurahia 'Classic Goal' la Stephane Aziz Ki

Ni mwana Simba SC mwenye roho mbaya na ya kichawi ndiyo hatolifurahia 'Classic Goal' la Stephane Aziz Ki

Hivi Simba waliweka hata ukuta pale au walimuachia Ki ajimwambafai tu? Hii game tulikuwa tunafunga mahesabu kipindi cha kwanza.
Nilipokuwa natizama huu Mpira Jana kuna Mtu nilikaa nae Jirani na kila mara nilikuwa nikimwambia kuwa Wachezaji wa Simba SC waepuke mno kucheza Faulo karibu na eneo la 18 yetu kwani wana Mpigaji mzuri Stephane Aziz K.

Unaweza usiniamini ila Mwenyezi Mungu Shabidi jana ilipotokea tu ile Faulo na kuona Mpigaji alikuwa ni Aziz K nilimwambia Jamaa ( Jirani ) kuwa Simba SC tunafungwa na Aziz K na kweli akatufunga na Jirani ( Jamaa ) Kunishangaa mno.

GENTAMYCINE nilianza Kumuogopa Stephane Aziz K baada ya Kumuona akiwa katika Klabu aliyotoka na Kugundua ni mzuri ( Mwamba ) mno wa kupiga Mipira ya Faulo na huwa ni Nadra sana Kukukosa hasa maeneo kama yale na ule Mguu wake wa Dhahabu ( Mashoto )

Ni Goli superb hata kama limeniuma.
 
kwa hiyo azizi ki kuifunga simba leo ndio kawa bora. Tuambie kaonekana wapi zaidi ya lile goli. Mbona hakuwavusha yanga kwenda group stage. Kama unae chama ki wanini. acha kwenda na matukio kama upepo
Huna Akili na Heshimu maoni yangu hapa Jamiiforums sawa? GENTAMYCINE siyo tu ni Shabiki wa Simba SC ila pia ni Mwanamichezo hivyo hata kama nikiona upande wa Yanga SC kuna Jambo Jema au Mchezaji mzuri sitoacha Kupongeza na Kumpongeza sawa?

Una Roho Mbaya, Mswahili na Mshamba.
 
Kama mwana Simba SC ni Goli ambalo limeniuma kwani amesawazisha ila Kiuanamichezo na hasa nikiwa kama Mdau wa Soka GENTAMYCINE nisiwe Mnafiki na naomba niseme tu kuwa ni Goli zuri hakuna mfano kwani alijiseti vyema kabisa na Kunipigia 'Muwa' wa maana ulioenda kule kule anakotagia Mayai Ndege.

Sijui Simba SC yangu (hasa Mwekezaji Mo Dewji) alishindwa nini na wapi kumpata huyu Kiungo Mshambuliaji Raia kutoka nchini Burkina Faso Stephane Aziz K kwani kwa Kipaji chake na Uwezo wake angetua Simba SC na kukutana na Mafundi tupu akina Chama, Phiri na Okra nina uhakika hivi sasa tungekuwa tunasema mengine.

Hongereni Yanga SC kwa kuwa nae.
Heshima yako bro, hapo ndipo huwa nakubali kwenye ukweli unakuwa mkweli lile gori ni superb asee
 
kwa hiyo azizi ki kuifunga simba leo ndio kawa bora. Tuambie kaonekana wapi zaidi ya lile goli. Mbona hakuwavusha yanga kwenda group stage. Kama unae chama ki wanini. acha kwenda na matukio kama upepo
Kuivusha team kwenda group stage ni Jambo jingine na ubora wa mchezaji ni Jambo jingine.. mfano Salah ni bonge la player lakn ameahindwa kuivisha Egypt kwenda World cup, huu ni mfano mmoja wapo
 
Heshima yako bro, hapo ndipo huwa nakubali kwenye ukweli unakuwa mkweli lile gori ni superb asee
Asante Mkuu ila nachukiwa na wana Simba SC wengi Wapumbavu ( Mapopoma ) na Washamba ( Mambwiga ) ambao wao wanadhani Uanamichezo ni kuwa mwana Simba SC na Kuiichukia Yanga SC hata kama kuna mazuri au Mchezaji wao kafanya Jambo jema.
 
Kama mwana Simba SC ni goli ambalo limeniuma kwani amesawazisha ila kiuanamichezo na hasa nikiwa kama mdau wa soka GENTAMYCINE, nisiwe mnafiki na naomba niseme tu kuwa ni goli zuri hakuna mfano. Kwani alijiseti vyema kabisa na kunipigia 'muwa' wa maana ulioenda kule kule anakotagia mayai ndege.

Sijui Simba SC yangu (hasa Mwekezaji Mo Dewji) alishindwa nini na wapi kumpata huyu kiungo mshambuliaji raia kutoka nchini Burkina Faso Stephane Aziz K? Kwani kwa kipaji chake na uwezo wake angetua Simba SC na kukutana na mafundi tupu akina Chama, Phiri na Okra, nina uhakika hivi sasa tungekuwa tunasema mengine.

Hongereni Yanga SC kwa kuwa naye.
Sasa🦁wenzio wanasema refa aliwapa yanga foul iliyowapa goli,wakiambiwa wanazidiwa uwezo wanabisha😂
 
Goli zuri sana ila ukiondoa goli alikua kapotea uwanjani. Okrah had a good game ila ubinafsi umefanya aonekane wa kawaida tu mwehu yule.


Ule Mgoli wa Aziz Ki ni mwana ukome
Tofauti na assist Chama ulimuona wapi? Phiri nae ulimuona wapi?
 
Angalia rekodi ya derby 8 za karibuni zaidi😂.pia ndoto ya ubingwa wa ligi tunachukua miaka7 mfululizo🚶
Tunaongelea mechi iliyotoka kuchezwa, mlizidi nini? Kama ni historia mlishawahi kubamizwa 5G na misimu ya karibuni 4G. Timu ya maana haiwezi kujivunia ubingwa wa aina hii ya ligi huku kimataifa ukivurunda. Yaani hamna tofauti na klabu bingwa ya ligi ya nchini Shelisheli.
 
Back
Top Bottom