Infantry Soldier
JF-Expert Member
- Feb 18, 2012
- 15,892
- 16,476
Habari za wakati huu waungwana wa jamiiforums.
Ni nani alikuwa nyuma ya kuvunjika kwa taifa la Sudan? Je, ilikuwa ni vita ya mabeberu dhidi ya uchumi (mafuta) wa Omar al-Bashir?
Ni kweli kwamba wazungu walijua kiburi cha Al Bashir kilitokana na hazina kubwa ya mafuta hivyo wakaamua kuchochea kujitenga kwa Sudan Kusini?
==========
==========
Nchi ya Sudan Kusini ilipata uhuru wake kutoka kwa Sudan ya Kaskazini (binafsi ninapendaga kuiita Sudan ya Waarabu) mnamo mwezi Julai 9, mwaka 2011 kama matokeo ya makubaliano ya mwaka 2005 ambayo yalimaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa muda mrefu sana barani Afrika. Sudan Kusini ni moja wapo ya nchi kubwa zaidi barani Afrika kwa kuwa inaundwa na majimbo 10 makubwa nchini humo.
HUKO BUNGENI MAREKANI MWAKA 1997
==========
Mnamo siku ya Alhamis tarehe 15 mwezi May mwaka 1997 katika bunge la Senate la Marekani, kulifanyika kikao cha kamati ya bunge ya masuala ya uhusiano wa kimataifa (Committee on Foreign Relations) ambapo kamati ndogo ya masuala ya Afrika (Subcommittee on African Affairs) ilikutana.
Bwana JOHN ASHCROFT aliyekuwa Seneta kutoka jimbo la MISSOURI alipewa fursa ya kuwasilisha report yake ndefu sana kuhusiana na tuhuma za taifa la Sudan Kufadhili makundi ya magaidi yanayojiita ni ya kiislam. Haya ndio baadhi ya maneno ya seneta Ashcroft katika report yake ile ndefu sana ya masaa 3 kuhusiana na taifa la Sudan;
"Osama bin Laden anahamasisha jihad dhidi ya Marekani, na haswa dhidi ya wanajeshi wa Marekani huko Saudi Arabia. Bin Laden alikuwa amehifadhiwa na Sudan kwa karibu miaka 5, na alikuwa akihusika katika mashambulizi kwa wanajeshi wa Marekani huko Somalia, Saudi Arabia, hususan maeneo ya Riyadh na Dhahran.
Moja wapo ya hatari kubwa zaidi ya vitisho hivi vipya vya usalama wa taifa letu ni kuongezeka kwa ugaidi wa kimataifa. Tunafanya kikao hiki leo katika Kamati Ndogo ya Masuala ya Afrika kushughulikia hatari ya ugaidi inayofadhiliwa na Serikali ya Sudan.
Tangia mara ya kwanza ilipotambuliwa kama taifa la ufadhili wa shughuli za ugaidi mnamo mwaka 1993, Sudan imekua na kupanuka haraka katika shughuli za udhalimu na kufanana na Iran kama wafadhili wabaya zaidi wa ugaidi wa kimataifa.
==========
==========
Sudan inahifadhi na kuficha makundi mengi ya kigaidi yenye vurugu zaidi ulimwenguni. Makundi kama yale ya Jihad, kikundi cha wanaojiita Waislam chenye silaha kali, Hamas, Abu Nidal, makundi ya Jihad ya Palestina, Hizbollah, na vikundi vingine vinavyojiita vya kiislamu vyote viko katika kambi za mafunzo ya kigaidi nchini Sudan.
Vikundi hivi vya kigaidi vinahusika na mamia ya mashambulio ya kigaidi ulimwenguni kote ambayo yamegharimu maisha ya maelfu ya raia wasio na hatia. Sudan sio tu mahali pa kwenda likizo kwa magaidi bali pia ni kiwanda cha kutotolea magaidi (Incubator for terrorist).
Serikali ya Sudan ndio msaidizi mkuu anayehusika na shughuli hizi za kigaidi. Kuna taarifa kuwa Sudan ilitoa silaha na nyaraka za kusafiri kwa wauaji waliomshambulia Rais Mubarak lakini hawakumuua.
==========
==========
Wanadiplomasia wawili wa Sudan katika Umoja wa Mataifa huko New York walikula njama za kuwasaidia magaidi wanaojiita wa kiislam kuingia ndani ya eneo la Umoja wa Mataifa (UN) na kulipua jengo hilo"
SWALI: Ni nani alikuwa nyuma ya kuvunjika kwa taifa la Sudan?
Note: Ninajua humu JF kuna wataalam sana wa siasa za Afrika na dunia na watatusaidia sana katika kutupa taarifa zaidi. Karibuni sana wakuu.
USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Maoni ya wadau;

==========John Garang alitaka Sudan iwe moja,wadinka,Nuer,Warabu,Wanubi waishi na kufanya kazi pamoja.Priority ya CIA was to divide and rule ambayo wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa, baada ya Sudan kusini kuwa huru kichobaki ni kuwapiganisha Wadinka na Nuer huku asilimia 90 ya pato la mafuta linatumika kununulia vifaa vya kivita.RIP John Garang.
==========Nakubaliana na wengine hapo juu. Tulishuhudia mauonevu mengi ya kaskazini dhidi ya kusini. Nadhani sababu itakuwa yaleyale mnayosema - kwamba wa kaskazin - machotara wa kiarabu? Kujiona superior zaidi ya wenzao wa kusini - weusi tiii.
Hivyo pamoja na mambo mengine kusini kuwa na maendeleo kidogo kulinganisha na kaskazini na manyanyaso mengine dhidi ya watu wa kusini. Sishangai sana kwa nchi kuwa na mambo kama hayo. Tumeona kubaguana kati ya wahutu na watutsi. Kenya wakikuyu au wajaluo etc. kujiona kustahili kuliko makabila mengine. Msumbiji kusini kuonekana labda kustahili zaidi ya kaskazini. Afrika ya kati waislam na wakristo na nk.
Jamii/ dini/ kanda/ kabila kujiona juu ya wengine katika nchi yapo sana na naona ufumbuzi wa hii changamoto ni ngumu kupatikana.
Utamwambia nini yule aliyefundishwa tangia utoto kwamba yeye mwenye rangi inayofanana na mwarabu ni bora kuliko mweusi tiii? Etc. Ni ngumu sana hii
Kwahyo nnavyoona wasudan kaskazin ni watu wenye mtizamo fulani wa kibaguzi. Hii itakuwa kuanzia mtaani mpaka kwenye nafasi za juu serikalini na nafasi za umma. Sina uhakika na hili lakini napata picha hali kuwa hivyo.
Ikishakuwa hivyo inakuwa kazi rahisi kwa wachonganishi (CIA, etc.) kutumia mwanya huu kufanya wanachotaka. The higher the stake the more the effort. Kama kusini wasingekuwa na natural resources zozote wangeachwa hivyo hivyo wapambane na hali yao.
Lakin kwa kuwa wana mali ni jambo la maana kuwasaidia. Faida zipo nyingi. Kama mnavyosema mwenye fedha kidogo hana uwezo mkubwa wa kufadhili magaidi. Kusini ya wakristo ni rahisi kuelewa somo la wazungu tofauti na Kaskazini ya waislamu damu.
Huenda Kusini walitamani sana kuishi kwa amani na wenzao wa kaskazini lakin kaskazini naona hawakuweza kufanya lolote la maana kutaka amani ya kweli na wenzao wa kusini.
Ubaguzi ni kitu kibaya sana. Kwamba binadamu mwenzio hastahili cha maana sababu ya dini yake au rangi yake au kabila lake etc. Ubaguzi naona ndo mzizi wa kutengana kwao.
Akina CIA naona wametia timu kuja kumalizia mechi waliyoianza wenyewe. Ila nafikiri CIA wasingetaka kutengana kwa north na south wasingetengana
To cut a long story short, Nubian Christian iliendelea ku-survive hadi na wenyewe walipoangukia mikononi mwa Ottoman Empire, na kutokea hapo Uislamu ukaanza kuenea Sudan!
Hata hivyo, kule kusini wengi walikuwa hawajapokea imani za wageni!
Ukaingia Utawala wa Waingereza!!
Utawala wa Kiingereza waliikuta Sudan Kaskazini ikiwa ya Waislamu, na kule kusini dini ilikuwa haijatawala sana, na hivyo kumfanya Mwingereza apeleke Ukristo kusini.
Lakini wakati Uingereza inaingiza Ukristo Southern Sudan, kule Kaskazini walikuwa wameshapiga hatua kimaendeleao kulinganisha na kusini!
Mwingereza nae, ni kama akafuata mfumo ule ule... wakati anawapa Bible Kusini, shughuli nyingi zikawa zinafanyika kaskazini to the point, by 1902 Kaskazini wakawa na chuo chao cha kwanza na hivyo kuwawezesha kujenga Tabaka la Watawala huku kusini wakibaki na bible yao!!
Sasa lilipoanza vuguvugu la kudai uhuru barani Afrika bila shaka unaweza kupata picha ni nani alianzisha harakati na hatimae kuhodhi madaraka... ni Sudan Kaskazini!
Ibrahim Abboud alipoingia madarakani, mambo ndo yakaanza kuwaka moto rasmi, na kosa kubwa ambalo alifanya ni kuiingiza Sudan Kusini kwenye utamaduni Kiislamu na Kiarabu ambao ulikuwa umeshamiri Kaskazini iliyokuwa imehodhi madaraka!!
Hata Mitaala ya Kiingereza iliyokuwa inatumika kusini, ikabadilishwa na kuingizwa ya Kiarabu na Kiislamu!!
Watu wa Kusini hawakuwa tayari kwa hilo, na mtifuano wa wazi kati ya kusini na kaskazini ukaanzia hapo. Hyo hiyo ilikuwa mwanzoni mwa miaka ya 1960's kabla hayo mafuta hayajagunduliwa!!!
Na tangu mgogoro huo wa mwanzo kabisa kuanza, Sudan mbili hizi hazikutulia tena hadi walipokuja kugawana nyama mbichi! Kwahiyo naweza kusema with confidence, popote ambapo haki haitekelezwi ipasavyo, hapahitaji kuwa na mafuta kutokea kilichotokea Sudan Kusini!
Mbaya zaidi, Sudan Kaskazin wanaojiona ni Waarabu, ni Wabaguzi wa kutisha kuliko hata hao Waarabu wenyewe wa Middle East!!
Sasa unapokosa kutoa haki, hapo hapo ukiwabua wananchi wa taifa lako, matokeo yake ndo hayo ya kuwepo kilichopo hivi sasa!!
Hata hivyo, wakati mafuta sio chanzo cha Sudan mbili hizi kugawana nyama mbichi, sina shaka ni hayo mafuta ndiyo inaifanya Sudan Kusini isiwe imetulia hadi sasa licha kuwa wameshaachiwa nchi yao!! Sasa badala ya kupambana na mbaya wao, wamejikuta wakichapana wenyewe kwa wenyewe!!