Unajua watu wanaangalia tatizo la Sudan Kusini na Sudan kwa ujumla kuanzia utawala wa Omar Bashir lakini root ya matatizo ya mataifa haya ni mbali sana!!!Hakuna cha kuona mbali bora walivyogawana mbao ,yeye angekuwa mnufaika wa utawala hivyo hakujali wengine
Sudan Kusini ilisimama itakuwa na nguvu Sana kiuchumi hapa EAC
Na hata madai yako kwamba Garang aliona angekuwa ni mnufaika ni madai yanayoweza kuwa ya kweli kwa sababu, serikali ya mwanzo kabisa, miaka michache tu baada ya kupata uhuru, serikali ya Sudan ilikuwa na wajumbe wawili kutoka kusini, na mmoja wa hao wajumbe alikuwa ni John Garang!!
Binafsi, naweza kumlaumu sana Mwingereza na ile staili yake ya divide and rule! Sudan ya Kaskazini ilikuwa na mambo mengi mno ya kuifanya pande hiyo kuwa superior over south! Yaani ukoloni tayari ulishaiandaa Sudan Kaskazini kuwa ruling class!!
Sasa ukichanganya tabia yao ya ubaguzi ambayo ipo hadi kesho, ikawa ni chumvi kwenye kidonda kibichi!!