n-propanol
JF-Expert Member
- Apr 7, 2019
- 5,349
- 7,000
Nathan Wami Mwaluganje, huyu ndio alikuwa manager wa Rose mhando. Katikati ya safari huko wakawa mpaka wapenzi na booking zote pamoja na pesa za shows za ndani hata nje ya nchi huyo mzee alikuwa anazi handle yeye.Katika interview yake pale Clouds ameeleza situations mbalimbali alizopitia katika maisha za mateso na kuumizwa hata kupelekea kubaki na makovu ya mwili na rohoni.
Ni nani huyo mtu tishio kwa kiwango hicho? mpaka anaogopa kabisa kumtaja na anaishia kusema nimesamehe!
Japo tumjue tu, hata kwa picha pia wala si kwa ubaya maana amesamehewa na mhusika.
Dada alikuwa mraibu kabisa, ili aweze kuimba na kucheza kama chizi na akikataa hizo mishe alikuwa anakula kipigo heavy.