Ni nani alimtesa vile Rose Mhando?

Ni watu waliokuwa wanasimamia kazi zake, ashawahi kuwataja zamani...

Lakini ukiacha hilo, yeye mwenyewe ni chanzo cha kufika hapo alipofika...

Alifanya muziki wa injili kuwa biashara kama muziki wa kina Chamelion, Mr Nice n.k maana ndio alikuwa anashindana nao umaarufu wakati huo...

Mungu akafanya yake (ukisoma sentensi hii usitumie akili ya kuvuka barabara kuielewa)
 
niliskiza interview yake na SALAMA hakika amepita pagumu ila Mungu huyu atamsimamia tena
 
Shida ni Rose mwenyewe,
Alifanya biashara ya dini badala ya kueneza injili.
Kama ngono ilikuwa ni sehemu ya propeller yake, malipo halisi badala ya malipo wezeshi basi alikuwa mfanyabiashara wa dini
Amepata anachistahili,
Ni mfano kwa wengine usimletee MUNGU dhihaka
 
Inaonekana kuna nguvu ya ziada ya mvuto alikua akupata kutoka kwa huyo meneja wake. Sasa hivi haipo ndio mana unaona hawiki tena kama awali
 
Hapa nakubaliana na wew. Kuna kipindi ilifika yaani karibia Kila Jumapil ana show mbil au tatu kwa siku na n makanisa na mikutano tofaut. Kiasi alishindwa kwenda mpaka kuitwa tapel
 
Yeye alikua vizuri ila msimaiz wa kaz zake alikua tapel
 
Mimi nashindwa kuelewa, kwani wakati wanaandikiana mikataba ya kazi, Upande Rose Muhando yeye alikuwa na wakili wake? Kama hakuwa naye kwanini alikubali kuwana chini ya Msama production Wakati hakutimiza masharti ya mikataba ya kazi kama hizo? Anavuna alichopanda?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…