Ubungoubungo
JF-Expert Member
- Jul 28, 2008
- 2,502
- 741
Kama CCM itashindwa kuona na kusikia ukweli huu ya kuwa main actors na successors wao hawataweza shindana na wale waliopo CHADEMA basi watakuwa wanamacho lakini hawaoni na masikio lakini yasiyosikia. Ukiangalia hata tafsiri ya results za uchaguzi inaonyesha kuwa behind CHADEMA kuna nguvu ya waelewa (Literate) ambao kutokana na history ya Siasa za zamani wameshindwa kujionyesha waziwazi so they play indirectly. Na in the front line CHADEMA ina vijana wasomi wenye confidance yakutosha na wenye uwezo wakujenga hoja ambayo itawafanya CCM wajikute mara zote wana resort kwenye kutumia stick measures (Kwasababu ya kuwa proveked) ambayo itasababisha public i sympathize na CHADEMA. Mwisho wa siku CCM itaji identify kama chama chenye kulazimisha mambo na hivyo kukosa public support ya kutosha hivyo kuwa weakened kiasi ambacho....well niishie hapo. Mwenye macho na atazame na mwenye sikio asikie....This is 2010. CCM angalien succession plan yenu!
Mimi binafsi nampongeza Mh. Jakaya Mrisho Kikwete kwa hatua yake ya kukemea udini maana kweli upo.
Kama mnabisha angalieni: Kuna vyama vingine vimejaa watu wa dini moja tu na nafasi za juu zote zimeshikwa na watu wa dini hiyo hiyo tu!
Hata wakiambiwa wateue watu kwenye nafasi fulani basi watateua watu wa dini hiyo tu! Hata kama nafasi ni tatu, wote watakuwa ni wa dini hiyo tu! Kwa hili Watanzania wenzangu udini upo ila mimi ningekuwa na uwezo wa kumwuliza ningetaka kujua mtu hasa anayeendekeza huo udini ili nimjue. Ningemwomba rais wetu ambaye si mdini hata aniambie huo udini anao usema ni nani hasa ameupanda na kuupalilia!!
Kikwete na kikundi chake ndani ya CCM wameamua kutumia udini kama tatizo ili kufunika mambo muhimu yenye utata katika nchi kwa sasa. Nchi ina matatizo ya kifisadi, utendaji mbovu wa serikali, maisha magumu kwa wananchi na mengine muhumu. Udini sio tatizo Tanzania, unatumika kugeuza upepo.
Mimi ninacho kiona nikwamba watu wengi wanajua nini nisiasa nakila aliye na nafasi yakuongea kwenye jamii akiongelea siasa wakati yupo kanisani ccm wanasema niudini!mfano ni askofu kakobe aliongea kanisani na akatoa mistari inayoelekeza watu wakamchague kiongozi lakini ccm waliibebea bango!!wakasahau misikitini nini kilichokuwa kikisemwa kila siku kwenye miadhara hadi kwenye sala za ijumaa!!
Wanausalama wanapokaa kimya hata km Mkuu anapoteleza, au nao wamegawanyika?
Abraham Lincolin The father of Democracy alipata misukosuko ya hapa na pale ili kupata Democracy ya kweli, sio kazi rahisi kupata uhuru wa kweli, siku moja utafahamu ni nini kinaongelewa hapa, ni mapambano kuelekea Democracy ya kweli sio chenga chenga tunazoziona sasahivi,
nafikiri tunapaswa kuishi karne ya 21 na siyo kurudi nyuma tena. i thought you'll be the one to support! mapambazuko ndiyo hayo, endelea kufuatilia yanayotokea.
Kwa nini huyu asibanwe aeleze huo udini ukoje? Tumemchoka na 'rhetorics' zake kuhusu udini. Kwa mtazamo wangu yeye ndiye anayeamsha hisia za udini. Tanzania yetu haina ujinga wa udini kwa sababu utakuta watu wa familia moja wengine wakristo na wengine waislamu na hakuna tatizo maisha yanaenda. Huyu anawaaga ndugu zake kuwa anaenda msikitini, na mwingine anaaga anakwenda kanisani na hakuna tatizo lolote. Huu udini anaousema Kikwete u wapi? Anaudhi sana.