Elections 2010 Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Elections 2010 Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Status
Not open for further replies.
- Wakuu kuuliza si ujinga ninauliza hivi: Chadema wana tatizo na NEC kwa sababu kikatiba ndio wenye mamlaka ya kuamua nani awe Rais kutokana na kura za wananchi walizonazo mikononi,

- Au wana tatizo na Rais kwa sababu amewaibia kura ambazo zinaonyesha kwamba Dr. Slaa ndiye aliyeshinda U-Rais?

William.
 
Kiongozi William,

Swali lako jibu lake liko kwenye tamko la Dr. Slaa. Wao wanatatizo na kuwepo kwa Kikwete kama Rais, na hajataja NEC hata kidogo. Hivyo wanataka katiba mpya, kwa shinikizo la kisiasa.
Hata hivyo mimi si msemaji wa Chadema, I stand to be corrected.
 
Halafu tuelezane, hao wasiomtambua Rais Kikwete je Rais wao ni nani?
Hili swali nauliza maana naona hii kauli ya Dr. Slaa imeanza kwa wimbo wa taifa!

Sasa nchi hii bora tupigane tu manake watu wamerukiwa na damu za kifasadi wanaleta comments za ajabu. Naona hii forum sasa imevamiwa na watu elimu za Memkwa, kwani alichongea Slaa hakieleweki nini?. Hivi hujawahi sikia watu hawamtambui rais?. au ndio mara ya kwanza kusikia?. Urais is just a symbol (Office). kwani wewe unaemtambua unatofauti gani na asiye mtambua, au ukimtambua unalala nae nyumbani. Slaa kasema hivi hatambui mfumo uliompeleka madarakani rais, kwamba mfumo si halali na wanashinikiza ubadilishwe .Rudia kusikiza hotuba
 
- Wakuu kuuliza si ujinga ninauliza hivi: Chadema wana tatizo na NEC kwa sababu kikatiba ndio wenye mamlaka ya kuamua nani awe Rais kutokana na kura za wananchi walizonazo mikononi,

- Au wana tatizo na Rais kwa sababu amewaibia kura ambazo zinaonyesha kwamba Dr. Slaa ndiye aliyeshinda U-Rais?

William.

CHadema wana Tatizo na wote..,kwa sababu kwa mfumo BUTU wa Tanzania mabosi wa NEC ni RAISI-KIKWETE..,so kama wana tatizo na NEC -basi wana tatizo na aliyewaweka pale.
naamini ukienda hotelini ukaletewa chakula chenye nzi/mende utakuwa na tatizo na muhudumu,asipokusikiliza utamfuata mpishi,asipokuelewa utamuomba meneja wa mgahawa etc..,

hicho ndicho walichokifanya CHADEMA,walianza na NEC..,hawakuwasikiliza..,si VIBAYA wakimzonga bosi wao/aliyewaajiri/RAIS/KIKWETE
 
Mwanzoni anasema CHADEMA wametoka wakati Mh. Rais wa Jamuhuri Ya Muungano akiingia. Hii tayari ni kutambua kuwa kuna Rais. Pia anasema wanapeleka maelezo yao serikalini, inamaana wanaimani na serikali. Je, serikali inaongozwa na nani? Sio kwamba haya maelezo yanapelekwa kwa serikali ya Kikwete? Halafu, tatizo ni madai ya utekelezaji wa madai mbalimbali au tatizo ni uchaguzi? Mbona kama wanalalamikia sheria na madai yasiyo na uhusiano na uchaguzi? Pia anahitaji utekelezaji wa hayo katika uchaguzi wa 2015, inamaana uchaguzi huu amekubali kimsingi kwamba CHADEMA wameyakubali matokeo? Kwahiyo tatizo lipo katika maeneo hayo tu aliyotaja na si Urais? Maana hajazungumzia kabisa uwezekano wa yeye kunyang'anywa Urais.

nice one buddy... very articulate folk, clap clap!!
 
Katika mambo ambayo JK ameyaongea kwa msisitizo na sauti ya kimadaraka ktk hotuba yake ya ufunguzi wa Bunge, ni suala la UDINI, kuwa udini unaanza kujitokeza. Naomba mnijuze wapambanuaji, ni nini kimetokea mpaka JK alikemee kwa sauti kubwa kiasi hicho suala la UDINI? Je ni kwasababu matokeo ya uchaguzi hayakufika 80% kama walivyotarajia? au kuna sehemu wakati wa kampeni na hata uchaguzi huu, kulitokea UDINI? Nionavyo mimi, tamko lake hilo, laweza kuleta mka'nganyiko kwa wananchi. Natoa hoja.
Mimi nadhani hilo swali inabadi tumuulize yeye mwenyewe ndie anajua zaidi. Nadhani kama ni udini tumefikia hatua hiyo kwa sababu ya kuwa na raisi dhaifu. Mbona hayo mambo hayakufikia hatua anazosema miaka iliyopita?
Labda udini wenyewe kama unavyosema ni kupungua kwa kura za CCM na kunyang'anywa majimbo muhimu.
Pia bila kusahau inabidi atuonyeshe na vielelezo sio kuzungumza tuu bila ushahidi.
 
Mkandara,

Logic yako ina mawaa yafuatayo.

Dr. Slaa alikuwa mgombea katika uchaguzi, alikuwa mmoja wa wagombea wengi. Kwa hiyo iliwezekana kabisa kwa watu ambao hawamtambui Dr. Slaa kama rais leo, hawakumtambua huko nyuma pia na wala hawakumuona kama ana uwezo wa kuwa rais, wakampigia Lipumba. Kwa hiyo mfano wako, kwa sababu unahusisha uchaguzi ambao unachagua rais kutoka wawakilishi wa vyama mbalimbali, kwa kupitia watu mbalimbali, hauwezi kufanana na uhakiki wa bunge ambao umeletwa bungeni na mtu mmoja, rais Kikwete.

Narudia
Pendekezo la Pinda lililetwa na mtu mmoja, Kikwete. Alilileta kwa kutumia kofia yake ya urais, kama ilivyosemwa katibani. Kitendo cha wabunge wa CHADEMA kushiriki kupiga kura katika uhakiki huu kilikuwa tayari ni kumtambua Kikwete kama rais.

CHADEMA wangeletewa jina limependekezwa na Matonya, wakaambiwa Matonya hajachaguliwa kuwa rais, lakini kampendekeza Chonya wa Chilonwa kuwa Waziri Mkuu, wangeshiriki kupiga kura kuhakiki pendekezo hili ?

Kama wangeshiriki ni kwa sababu gani ? Kama wasingeshiriki ni kwa sababu gani?

kuchamba kwingi kutoka na mavi mengi

kupiga kura ya kukataa na kutokupiga wewe unaona kutokupiga ndio kutomtambua rais...... ,,,,,,,,,,,,,kiranga bana
 
- Wakuu kuuliza si ujinga ninauliza hivi: Chadema wana tatizo na NEC kwa sababu kikatiba ndio wenye mamlaka ya kuamua nani awe Rais kutokana na kura za wananchi walizonazo mikononi,

- Au wana tatizo na Rais kwa sababu amewaibia kura ambazo zinaonyesha kwamba Dr. Slaa ndiye aliyeshinda U-Rais?

William.

Tuambie wewe unawasomaje ,?
 
kuchamba kwingi kutoka na mavi mengi

kupiga kura ya kukataa na kutokupiga wewe unaona kutokupiga ndio kutomtambua rais...... ,,,,,,,,,,,,,kiranga bana

Kura ilikuwa ya siri na ukiondoa wabunge wenyewe, hakuna mwingine anayejua kama walipiga YES or NO,

Mi sijasema chochote kuhusu kutomtambua rais, nauliza tu.

Wabunge wa CHADEMA waliposhiriki kulihakiki pendekezo la Kikwete kwa kiti cha Waziri Mkuu, walishiriki kuhakiki pendekezo la nani?

Unaweza kulijibu hilo swali? Kama huwezi unaweza kusema huwezi tu.
 
Next time mwambieni Slaa asome a prepared statement, hapo juu kajiadhiri tu, hata Kiswahili hajui.

Kama kitu kingeandikwa na kupata proofreaders watu wangeweza kuona makosa hayo.

Anazidi kuonyesha watu tu kwamba CHADEMA is not ready for prime time.

As much as I don't like CCM, napata tabu kuona mtu asiye makini kama Slaa kuwa rais. Kama mambo yake ndiyo shoddy hivi?

Unaacha wabunge wapigie kura pendekezo la Kikwete kama rais, halafu unataka kuprotest kwenye tafrija, unafikiri tunawezaje kumchukulia seriously hata kama tunataka CCM ifundishwe adabu ?

unajua tofauti ya mambo na vijimambo???
 
Urais is just a symbol (Office). kwani wewe unaemtambua unatofauti gani na asiye mtambua, au ukimtambua unalala nae nyumbani. Slaa kasema hivi hatambui mfumo uliompeleka madarakani rais, kwamba mfumo si halali na wanashinikiza ubadilishwe .Rudia kusikiza hotuba

Tofauti kati ya mimi na asiyemtambua Rais ni kwamba mimi ninaweza kusema I am proud to be a Tanzanian, my president is Jakaya Kikwete, my national flag has four colours; blue,yellow,black and green and my natinal anthem is ...
Wale wasiomtambua, hapo kwenye kipengele cha president wanaweka nini?
 
Kama hujaelewa speech ya Slaa rudia kuisikiza vizuri maana ni kawaida binadamu wanatofautiana kuelewa vitu kwa haraka.

Ikishindikana zaidi kajiandikishe MEMKWA ili upige msasa ubongo wako. Kutomtambua rais hakujaanzania Tanzania, ni jambo la kawaida, and it was convinience platform for Chadema today, na ujumbe umefika,

Wewe unayesema mbona walishiriki kura wakati wa kumpitisha Prime Minister, soma data vizuri, Pinda hakupata kura zote za ndio, zilikuwepo za hapana na zilizoharibika.

Mwanakijiji Hongera sana hao watu wanatishia uhai wako tunawafamu, na wao pia wajue kwa sasa siku zao zinahesabika, maana wametangaza vita, statement ile siyo ya kuipuzia hata kidogo, ni nzito na wajue inafanyiwa kazi.
 
CHadema wana Tatizo na wote..,kwa sababu kwa mfumo BUTU wa Tanzania mabosi wa NEC ni RAISI-KIKWETE..,so kama wana tatizo na NEC -basi wana tatizo na aliyewaweka pale.
naamini ukienda hotelini ukaletewa chakula chenye nzi/mende utakuwa na tatizo na muhudumu,asipokusikiliza utamfuata mpishi,asipokuelewa utamuomba meneja wa mgahawa etc..,

hicho ndicho walichokifanya CHADEMA,walianza na NEC..,hawakuwasikiliza..,si VIBAYA wakimzonga bosi wao/aliyewaajiri/RAIS/KIKWETE

- Sawa sawa mkuu katika mazingara ya katiba tuliyonayo na namba za wabunge tulionao, hili litarekebishwa vipi bila katiba kubadilishwa kwa sababu kiongozi fair wa NEC atatoka wapi na atachaguliwa na nani kwa muono wako?

William.
 
Kama hujaelewa speech ya Slaa rudia kuisikiza vizuri maana ni kawaida binadamu wanatofautiana kuelewa vitu kwa haraka.

Ikishindikana zaidi kajiandikishe MEMKWA ili upige msasa ubongo wako. Kutomtambua rais hakujaanzania Tanzania, ni jambo la kawaida, and it was convinience platform for Chadema today, na ujumbe umefika,

Wewe unayesema mbona walishiriki kura wakati wa kumpitisha Prime Minister, soma data vizuri, Pinda hakupata kura zote za ndio, zilikuwepo za hapana na zilizoharibika.

Mwanakijiji Hongera sana hao watu wanatishia uhai wako tunawafamu, na wao pia wajue kwa sasa siku zao zinahesabika, maana wametangaza vita, statement ile siyo ya kuipuzia hata kidogo, ni nzito na wajue inafanyiwa kazi.

Swali moja sijapewa jibu bado,

Wabunge wa CHADEMA walivyoshiriki kupiga kura katika kulihakiki pendekezo la Kikwete kwa kiti cha Waziri Mkuu, walikuwa wanalipigia kura pendekezo la nani?
 
unajua tofauti ya mambo na vijimambo???

Mambo ni pale unaposema humtambui rais halafu hushiriki lolote la huyu mtu anayedaiwa kuwa rais, kama kupigia kura mapendekezo yake.

Vijimambo ni ku half step kama wanavyofanya CHADEMA sasa hivi, mara hawamtambui, mara wanamuita rais wa jamhuri ya muungano, mara wanashiriki kupigia kura mapendekezo yake kama rais, mara hawamtambui yeye kama rais.

Hiyo ndiyo tofauti ya mambo na vijimambo.
 
Kiongozi Kiranga,
hili la u-nusunusu wa utekelezaji wa kutokumtambua Rais lisikupe shida kwa sasa. Wengi watashuhudia pale utakapofika wakati wa kumuuliza mwaswali waziri mkuu na mawaziri wengine. Hapo watakiri kuwa utekelezaji wa azimio hili wameukosea, na waliukosea toka mwanzo.
 
Kiongozi William,

Swali lako jibu lake liko kwenye tamko la Dr. Slaa. Wao wanatatizo na kuwepo kwa Kikwete kama Rais, na hajataja NEC hata kidogo. Hivyo wanataka katiba mpya, kwa shinikizo la kisiasa.
Hata hivyo mimi si msemaji wa Chadema, I stand to be corrected.

- Hapana katiba haiwezi kubadilishwa kienyeji namna hii, yaani wananchi 46 tu wawe na nguvu ya kutubadilishia katiba wananchi 45 Millioni kwa sababu eti wanatoka Rais akihutubia, sasa hili litakua taifa gani mkuu?

- Hili ni la ridhaa ya wananchi wangewapa wabunge majority bungeni kweli, lakini wabunge 46 tu, hapana, NEC ina matatizo sawa, serikali iyasikilize na kuyatafutia ufumbuzi on its time lakini in the meantime wawache wabunge wa Chadema waendelee kugomea, maana hapa ndio tutajua ukweli ulipo, kama CCM na Rais hawahusiki na kinacholiliwa haina sababu yoyote ya kuhangaika, unless wamehusika kweli ndio tutaona wakihangiak kuwabembeleza!

William.
 
Itakuwa jambo la msingi na la maana kama Chadema hawatarudi tena Bungeni hapo Januari mwakani....
 
Swali moja sijapewa jibu bado,

Wabunge wa CHADEMA walivyoshiriki kupiga kura katika kulihakiki pendekezo la Kikwete kwa kiti cha Waziri Mkuu, walikuwa wanalipigia kura pendekezo la nani?
Walishiriki kwa kukataa pendekezo hilo(ungeuliza sababu labda ungeambiwa kuwa mojawapo ni kutomtambua aliyeleta pendekezo etc)..,binafsi naona walichokifanya kwa kulikataa pendekezo alilolileta Rais batili ni sahihi,kwani wameprotest pia.
Kwa matiki yako utawataka wabunge wachadema wasingetoka bungeni kwani kwa kufanya vile wangekuwa wanamaanisha wanatambua kuwa wanayempisha ni Rais,ndio maana hawamtambui.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom