Mkandara,
Logic yako ina mawaa yafuatayo.
Dr. Slaa alikuwa mgombea katika uchaguzi, alikuwa mmoja wa wagombea wengi. Kwa hiyo iliwezekana kabisa kwa watu ambao hawamtambui Dr. Slaa kama rais leo, hawakumtambua huko nyuma pia na wala hawakumuona kama ana uwezo wa kuwa rais, wakampigia Lipumba. Kwa hiyo mfano wako, kwa sababu unahusisha uchaguzi ambao unachagua rais kutoka wawakilishi wa vyama mbalimbali, kwa kupitia watu mbalimbali, hauwezi kufanana na uhakiki wa bunge ambao umeletwa bungeni na mtu mmoja, rais Kikwete.
Narudia
Pendekezo la Pinda lililetwa na mtu mmoja, Kikwete. Alilileta kwa kutumia kofia yake ya urais, kama ilivyosemwa katibani. Kitendo cha wabunge wa CHADEMA kushiriki kupiga kura katika uhakiki huu kilikuwa tayari ni kumtambua Kikwete kama rais.
CHADEMA wangeletewa jina limependekezwa na Matonya, wakaambiwa Matonya hajachaguliwa kuwa rais, lakini kampendekeza Chonya wa Chilonwa kuwa Waziri Mkuu, wangeshiriki kupiga kura kuhakiki pendekezo hili ?
Kama wangeshiriki ni kwa sababu gani ? Kama wasingeshiriki ni kwa sababu gani?