Elections 2010 Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Status
Not open for further replies.
- Hapana katiba haiwezi kubadilishwa kienyeji namna hii, yaani wananchi 46 tu wawe na nguvu ya kutubadilishia katiba wananchi 45 Millioni kwa sababu eti wanatoka Rais akihutubia, sasa hili litakua taifa gani mkuu?

William.

Ndugu hao watu 46 wanawakilisha mamilioni ya watanzania..,wanawakilisha mikoa yote chadema walipopewa kura,wanawakilisha kura zoote alizopewa dr.slaa,wanawakilisha wale wote walioichoka katiba mbovu.
 
Itakuwa jambo la msingi na la maana kama Chadema hawatarudi tena Bungeni hapo Januari mwakani....

Ninaamini kama kikwete atakuwa anahudhuria bungeni,basi jamaa wataendelea kumkacha..,wabunge wa chadema hawana tatizo na wabunge wenzao,ndio maana wali-sign form za kukubali kushindwa majimboni.kwa waliokataa kesi ziko mahakamani.msichoelewa ni kipi?
 
Walishiriki kwa kukataa pendekezo hilo(ungeuliza sababu labda ungeambiwa kuwa mojawapo ni kutomtambua aliyeleta pendekezo etc)..,binafsi naona walichokifanya kwa kulikataa pendekezo alilolileta Rais batili ni sahihi,kwani wameprotest pia.
Kwa matiki yako utawataka wabunge wachadema wasingetoka bungeni kwani kwa kufanya vile wangekuwa wanamaanisha wanatambua kuwa wanayempisha ni Rais,ndio maana hawamtambui.

Hujui kwamba walikataa pendekezo, kura zilikuwa za siri na kura za hapana hazija tally na namba za wabunge wa CHADEMA.

Ukishiriki tu uchaguzi unaotakiwa kupendekezwa na rais, maana yake unamtambua mpendekezaji kama rais.
 
sasa wewe unataka kuleta ubishi wakitoto,kwahiyo zile kura ni za cuf au CCM?

kama unalo jibu kichwani kwako then hamna atakayekujibu...,
 
Swali moja sijapewa jibu bado,

Wabunge wa CHADEMA walivyoshiriki kupiga kura katika kulihakiki pendekezo la Kikwete kwa kiti cha Waziri Mkuu, walikuwa wanalipigia kura pendekezo la nani?
Kwa ufupi walikuwa hawajui wanafanya nini! Aidha kwa kuwa kauli za kususa zinatokakwa Slaa pekee, nae alichelewa kuwaambia wabunge wake nini maana ya kutomtambua rais. Kwa namna moja ama nyingine wameenda mkenge kwa hilo.

Kwa kuwa sasa wameshatoka huko bungeni ni vema wasirudi tena hadi pale madai yao yatakaposikilizwa, na iwapo watarudi ina maana wanamtambua rais.
 
Huku ni kupoteza muda na ni protest isiyo na kichwa wala miguu in the long run. Kama mna mkataa Raisi mjue huo ndio mwanzao tu, kwa kuwa raisi ndie anaechagua baraza la mawaziri na hiyo ndio executive branch of the government. Na wao ndio huleta agenda za mikakati ya serikali Bungeni kujadiliwa kwa maana hiyo mna ikataa serikali nzima ijayo.

Hivyo kutotupotozea muda watanzania bora mseme mapema kuwa amuafiki uchaguzi wote urudiwe. Cut the joke, angaikeni na katiba na si hivi vitu vilivyokuwa short sighted. By the way kama mkiafiki kukataa uchaguzi ni bora huko bungeni msirudi muende mahakamani sasa kwa mwenendo mtakuja zua balaa tu.
 
sasa wewe unataka kuleta ubishi wakitoto,kwahiyo zile kura ni za cuf au CCM?

kama unalo jibu kichwani kwako then hamna atakayekujibu...,

Kura zilikuwa za siri, hatujui kura zilikuwa za nani.

Kushiriki kupiga kura tu kulikuwa ni kitendo cha kumtambua Kikwete kama rais, si kwa maneno, kwa vitendo. Kama walitaka kutomtambua wangesusia kupiga kura.
 
Huku ni kupoteza muda na ni protest isiyo na kichwa wala miguu in the long run. Kama mna mkataa Raisi mjue huo ndio mwanzao tu, kwa kuwa raisi ndie anaechagua baraza la mawaziri na hiyo ndio executive branch of the government. Na wao ndio huleta agenda za mikakati ya serikali Bungeni kujadiliwa kwa maana hiyo mna ikataa serikali nzima ijayo.

Hivyo kutotupotozea muda watanzania bora mseme mapema kuwa amuafiki uchaguzi wote urudiwe. Cut the joke, angaikeni na katiba na si hivi vitu vilivyokuwa short sighted. By the way kama mkiafiki kukataa uchaguzi ni bora huko bungeni msirudi muende mahakamani sasa kwa mwenendo mtakuja zua balaa tu.

Mi nasubiri kuona kama watashiriki katika miswada itakayowasilishwa na mawaziri wa rais huyu wasiyemtambua au la ?
 
Ndugu hao watu 46 wanawakilisha mamilioni ya watanzania..,wanawakilisha mikoa yote chadema walipopewa kura,wanawakilisha kura zoote alizopewa dr.slaa,wanawakilisha wale wote walioichoka katiba mbovu.

- Matokeo yanaonyesha ni wananchi Millioni 2.2 tu waliompigia Dr.Slaa, Tanzania tuna wananchi 45 Millioni kwa kutumia njia hii mkuu kuna tatizo sana kutuelimisha kuhusu kesi ya Chadema kwa sababu hawatuwakilishi wananchi wote wa Tanzania, na hatuwezi kuweka historia ya kubadilisha katiba kwa kutumia wabunge 46 tu,

- kwamba wabunge 46 tu wanaweza kubadilisha katiba ya jamhuri ya wananchi Millioni 45, unajua mkuu hii ishu kwa mazungumzo ya mtaani it makes a lot of sense mpaka ukiileta kwenye books ndio inapwaya sana!

William.
 
- Hapana katiba haiwezi kubadilishwa kienyeji namna hii, yaani wananchi 46 tu wawe na nguvu ya kutubadilishia katiba wananchi 45 Millioni kwa sababu eti wanatoka Rais akihutubia, sasa hili litakua taifa gani mkuu?

- Hili ni la ridhaa ya wananchi wangewapa wabunge majority bungeni kweli, lakini wabunge 46 tu, hapana, NEC ina matatizo sawa, serikali iyasikilize na kuyatafutia ufumbuzi on its time lakini in the meantime wawache wabunge wa Chadema waendelee kugomea, maana hapa ndio tutajua ukweli ulipo, kama CCM na Rais hawahusiki na kinacholiliwa haina sababu yoyote ya kuhangaika, unless wamehusika kweli ndio tutaona wakihangiak kuwabembeleza!

William.

This is briliant Bill,
Nimetafakari nikakumbuka kuwa uchaguzi ulipoisha tu, wabunge wote walienda Dodoma kwa ajili ya kuapishwa na shughuli nyigine za Bunge. Hivyo basi ni wazi kabisa kuwa maamuzi wanayoyafanya huko Dodoma ni yao binafsi na wala si ya wananchi, kwa sababu bado hata hawajapata muda wa kuwashukuru wananchi kwa kuwapigia kura, let alone kuwauliza msimamo wao juu ya urais.
Hii imedhihirisha kuwa wabunge hawa wanakitumika chama chao na si wananchi wao. Hii ni moja ya mfano wa chama kwanza!
 
Mi nasubiri kuona kama watashiriki katika miswada itakayowasilishwa na mawaziri wa rais huyu wasiyemtambua au la ?
sidhani kama ni kitu walicho kifikiria vizuri chote na itakuwa pointless kwenda bungeni kabisa kwa sababu the executive branch of the gov, ni uteule wa raisi. Sasa whats the point of all this wakati raisi mwenyewe hawamtambui si waseme tu hawato itambua serikali nzima.

Ps mi simo tena humu.
 
Kwa ufupi walikuwa hawajui wanafanya nini! Aidha kwa kuwa kauli za kususa zinatokakwa Slaa pekee, nae alichelewa kuwaambia wabunge wake nini maana ya kutomtambua rais. Kwa namna moja ama nyingine wameenda mkenge kwa hilo.

Kwa kuwa sasa wameshatoka huko bungeni ni vema wasirudi tena hadi pale madai yao yatakaposikilizwa, na iwapo watarudi ina maana wanamtambua rais.

Bunge lenyewe sehemu yake moja nzima ni rais, kwa hiyo kukubali kiapo cha bunge maana yake ni kumtambua rais.

Mtu kama una fikra za ku assume unaweza kufikiri hili la kutomtambua rais ni la Slaa tu, wabunge walikuwa poa. Na Slaa ana usongo binafsi na sasa hivi ana wa bulldoze wabunge kwa sababu yeye ni kiongozi wa juu wa chama tu aliyejitwalia umaarufu.
 
kwani wale ambao hawaamini Mungu huwa wanatumia maneno gani kuelezea
kutoamini kwao? naamini hata wao husema "hawaamini Mungu" lakini kwa kusema hivyo
haibadilishi msimamo wao/imani yao na sijapata sikia muumini akisema "mbona mnatumia
jina la Mungu wakati hamuamini" la hasha.

sasa kwanini inawapashida kusikia chadema wakisema hawamtambui raisi? kwani mlitaka
waseme hawamtambui nani? kikwete? au mlitaka waseme sentensi nzima kila mara yaani
"chadema haimtambui kikwete kama raisi wa jamhuri ya tanzania" ? hata hivyo hata wakisema
hivyo haimaanishi kikwete sio raisi kwani bado kwa hali ilivyosasa kikwete ni raisi bali ni raisi asiyetambuliwa
na chadema na watanzania wengine ambao hawajapendezwa na mchakato mzima uliompa kikwete huo
uraisi na wameamua kutomtambua. sasa hata hilo watu mnaliona gumu kulikubali kwamba japokuwa kikwete
ni raisi kuna chama kimejitokeza na kutamka hadharani bila kujiumauma kwamba hawamtambui.

waacheni chadema wadai haki yao wanayoamini wameporwa. kama kutomtambua kikwete ni njia
mojawapo ya kudai haki yao waendelee tu. kutumia kwao maneno kama hawamtambui raisi haina maana
wanamtambua raisi labda kwa wale wenye mazoea ya kuchakachua.

duh, bongo!
 
- Matokeo yanaonyesha ni wananchi Millioni 2.2 tu waliompigia Dr.Slaa, Tanzania tuna wananchi 45 Millioni kwa kutumia njia hii mkuu kuna tatizo sana kutuelimisha kuhusu kesi ya Chadema kwa sababu hawatuwakilishi wananchi wote wa Tanzania, na hatuwezi kuweka historia ya kubadilisha katiba kwa kutumia wabunge 46 tu,

- kwamba wabunge 46 tu wanaweza kubadilisha katiba ya jamhuri ya wananchi Millioni 45, unajua mkuu hii ishu kwa mazungumzo ya mtaani it makes a lot of sense mpaka ukiileta kwenye books ndio inapwaya sana!

William.

Kwa hesabu hizi basi hata Kikwete si Raisi wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania, ikiwa Kikwete amepata kura mil. 5 hawakilishi maoni ya hao watanzania mil. 46 unawaongelea, katiba yetu ilitungwa na wakoloni ilifanyiwa mabadiliko baada ya uhuru na marekebisho mengine wakati tunaingia kwenye mfumo wa vyama vyingi, marekebisho tunayataka si Chadema tu wenye kilio hicho bali ni watanzania wenye kutaka mfumo wenye demokrasia ya kweli ambao utalenga kwenye kuleta usawa ndani ya jamii yetu, sitegemei viongozi wa juu wa CCM wao na familia zao kufurahia marekebisho ya katiba hiyo ni sawa na kuuondoa tonge mdomoni, katiba si msahafu wala biblia serikali inaogopa kitu gani kuita kura ya maoni? Wanajua nini yatakuwa matokeo yake ndio maana hawataki kusikia kilio cha marekebisho ya katiba.
 
kwani wale ambao hawaamini Mungu huwa wanatumia maneno gani kuelezea
kutoamini kwao? naamini hata wao husema "hawaamini Mungu" lakini kwa kusema hivyo
haibadilishi msimamo wao/imani yao na sijapata sikia muumini akisema "mbona mnatumia
jina la Mungu wakati hamuamini" la hasha.

sasa kwanini inawapashida kusikia chadema wakisema hawamtambui raisi? kwani mlitaka
waseme hawamtambui nani? kikwete? au mlitaka waseme sentensi nzima kila mara yaani
"chadema haimtambui kikwete kama raisi wa jamhuri ya tanzania" ? hata hivyo hata wakisema
hivyo haimaanishi kikwete sio raisi kwani bado kwa hali ilivyosasa kikwete ni raisi bali ni raisi asiyetambuliwa
na chadema na watanzania wengine ambao hawajapendezwa na mchakato mzima uliompa kikwete huo
uraisi na wameamua kutomtambua. sasa hata hilo watu mnaliona gumu kulikubali kwamba japokuwa kikwete
ni raisi kuna chama kimejitokeza na kutamka hadharani bila kujiumauma kwamba hawamtambui.

waacheni chadema wadai haki yao wanayoamini wameporwa. kama kutomtambua kikwete ni njia
mojawapo ya kudai haki yao waendelee tu. kutumia kwao maneno kama hawamtambui raisi haina maana
wanamtambua raisi labda kwa wale wenye mazoea ya kuchakachua.

duh, bongo!

Tuache maneno, tuangalie vitendo.

Walipopiga kura kumhakiki Pinda walikuwa wanapigia kura pendekezo la nani ?
 
Katika mambo ambayo JK ameyaongea kwa msisitizo na sauti ya kimadaraka ktk hotuba yake ya ufunguzi wa Bunge, ni suala la UDINI, kuwa udini unaanza kujitokeza. Naomba mnijuze wapambanuaji, ni nini kimetokea mpaka JK alikemee kwa sauti kubwa kiasi hicho suala la UDINI? Je ni kwasababu matokeo ya uchaguzi hayakufika 80% kama walivyotarajia? au kuna sehemu wakati wa kampeni na hata uchaguzi huu, kulitokea UDINI? Nionavyo mimi, tamko lake hilo, laweza kuleta mka'nganyiko kwa wananchi. Natoa hoja.

Rais sema!!!!!!!

Hapa ni lazima uwe mkali na paondoke na mtu.
 
Kwa hesabu hizi basi hata Kikwete si Raisi wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania, ikiwa Kikwete amepata kura mil. 5 hawakilishi maoni ya hao watanzania mil. 46 unawaongelea, katiba yetu ilitungwa na wakoloni ilifanyiwa mabadiliko baada ya uhuru na marekebisho mengine wakati tunaingia kwenye mfumo wa vyama vyingi, marekebisho tunayataka si Chadema tu wenye kilio hicho bali ni watanzania wenye kutaka mfumo wenye demokrasia ya kweli ambao utalenga kwenye kuleta usawa ndani ya jamii yetu, sitegemei viongozi wa juu wa CCM wao na familia zao kufurahia marekebisho ya katiba hiyo ni sawa na kuuondoa tonge mdomoni, katiba si msahafu wala biblia serikali inaogopa kitu gani kuita kura ya maoni? Wanajua nini yatakuwa matokeo yake ndio maana hawataki kusikia kilio cha marekebisho ya katiba.

- Katiba inakubali kwamba wananchi Millioni 5, wanaweza kuwakilisha maoni ya wananchi Millioni 45 isipokuwa katiba haisemi kwamba wabunge 46 wanaweza kubadilisha katiba, isipokuwa wabunge 2/3 ya bunge zima, again ninasema hivi Chadema na wabunge 46 hawana mandate ya wananchi wote sisi Millioni 45.

- Nilijua kuwa baada ya kuzidiwa kwenye serious debate, utarudi kwenye familia, and then itakua elimu na baadaye umaarufu, unasema serikali iite kura za maoni kwa sababu ya wabunge 46 kugomea hotuba ya rais? Na hizo kura vipi hazitaibiwa? Kama nilivyosema haya mambo yana make a lot of sense kule mtaani, isipokuwa hapa uwanja wa werevu!

William.
 
Haya JK na Philosophy ya Uongozi. Sasa Kikwete Anaelekeza Kila Jambo Kwenye Udini. Uchaguzi Ulishindwa na Wananchi Hawakutaki na Hii Political Strategy ya Kutafuta Support Kwa Waislamu Itakuback Fire Like Missile. Kikwete na CCM Kweli Wamepitwa na Wakati Wanaona Kuzungumzia Dini Katika Siasa Ni Njia ya Kujenga Tanzania. Uchaguzi Umeonyesha Wananchi Wengi Hawakutaki na Sio Wakristo Peke Yao. Anza Mbele JK..........
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom