Elections 2010 Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Elections 2010 Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Status
Not open for further replies.
Waungwana!!
Jambo hili tukianza kulipa nafasi binafsi juu ya viongozi wetu kuwa na udini...ni kwamba TUTAANGAMIA. Hatujawahi katika historia ya Tanganyika na hata baadae tazania kuwa na viongozi wakuu wa nchi kutokuwa na dini wanazoziamini kwa mujibu wa imani zao. Kwa mfano:-
Tumekuwa na Nyerere,
Tumekuwa na Mwinyi ambaye aliwakutanisha viongozi wakuu wa madhehebu ya dini hapa nchini huku DR. Slaa akiwa ni katibu mkuu wa muungano wao kiimani na hata baadhi ya vikao hivyo alikuwa aki-chair,
Tumekuwa na Mkapa,
Na sasa tunae Kikwete...tumpe nafasi juu ya mpasuko wa udini ulioanza kusheheni hapa nchini, ila kumekuwa na hali mbaya kabisa ikizungumzwa juu ya udini.

ANGALIZO:
Sisi wanajamii (JF) tusiwe na hali ya mambo kama UDINI, itatugharimu saana. Hebu tutazame Palestine, Iraq, Nigeria, Pakistan etc...narudia hii itatugharimu waungwana naomba tulione kwa visionery hasaaa. Tukiliruhusu na kweli likapenya na kushika HATAMU ya udini nchini...tutateketea kama kumbikumbi na Tanganyika yetu maana Zanzibar inajulikana kuwa ni nchi ya kiislamu na hakuna anaebisha kwa hilo...TUJILINDE.
 
Nilisema na narudia kusema kuwa Mdini ni yeye mwenyewe na asijaribu kumtafuta mchawi mahali pengine popote. Alichokifanya katika hotuba yake ya uzinduzi ni pre-emptive strike ili kuwanyamazisha wale wote watakaothubutu kupinga mipango yake ya kichinichini ya kidini. Hii yote ni psychological preparation kuwaandaa watanzania kuikubali OIC na Mahakama ya Kadhi. Anachokifanya katika hotuba yake ni ku-create hali ya woga kwa watanzania ili watu waogope kupinga mipango ya kidini anayoitekeleza kichinichini. Hii yote ni muendlezo wa udini alionao na anaotaka kuuendeleza.

Just wait and See, Time will Tell.
 
kusema kweli, mdini ni kikwete mwenyewe...kwanini anaruhusu mambo hayo ya udini kuingia nchini, na kama kuna watu amewaona wana udini, kwanini asiwafesi moja kwa moja na kuwatangaza kwa kosa walilofanya,...kwasababu naongea hivyo kutokana na kwamba kauli hiyo yeye anawalenga wakristo, wakati wakristo nao wanaona yeye ni mdini kwa kuto kuwakemea mashehe wanaohubiri chuki huko msikitini na kwenye radio kheri na magazeti ya kiislam,, amenyamaza kimyaaa, toka lini kwenye magazeti ya kikristo au radio zetu tukahubiri udini?akawaseme waislam wenzie huko, sasa yeye anaamini kuwa wakristo ndio wadini...ajabu kweli.
 
Gazeti la Mwananchi la leo linatupasha habari ya kuwa kinyume na wanasiasa wachovu ndani ya CCM ambao wamekuwa wakitumia msamiati wa udini ili kuzuia raia kukemea maovu kwenye jamii, Mheshimiwa Kardinali Pengo ametoa tamko kuwa kukemea uovu siyo udini...

Hii tafsiri imekuja wakati muafaka kwani kwenye chaguzi hii iliyokwisha baadhi ya makada wa CCM wenye kukabiliwa na tuhuma nzito za ufisadi wamekuwa wakitumia kauli mbiu ya udini ili kuzima mijadala nyeti ya kitaifa dhidi ya matendo yao na hivyo kudhoofisha uwajibikaji serikalini...
 
Lakini wajibu wake kukemea maovu. Na hasa kama angetambua kuwa 80% ya transactions za kifisadi zinafanywa na sisi wakristo.
 
Hongera mh Pengo. lkn mbona huwa mankemea pale rais anapokuwa muislam tu. na huwa kimya mkiona rais ni mkiritso. zinduka

Wewe Malaria sugu si uende Afghanistan au Iraq ukawasaidie wenzako kujilipua kuliko kuendelea kupost pumba ndani ya JF? Ula ujihadhari usijekushikwa na wamarekani, watakunyonga kama uncle wako Saddam Hussein
 
Nafikiri Pengo alikuwa akimjibu Kikwete. Kikwete kaanzisha udini na hataki wengine wazungumzie ila yeye tu.
 
JK anadhani na anaamini kuwa kura za WAKRISTO zilipungua kwake. Huo ndio aliouita UDINI! Anasahau kuwa watu walimtarajia kuibadili hali ya NCHI yetu hasa kwa masuala ya rushwa na ufisadi. Hakufanya hivo. Badala yake akaanza vibaya kwa kumteua Lowassa kuwa WM wake.
 
Mi nadhani JK mwislam alitakiwa amudabishe Edward Lowassa mkristo kisha amschape Basil Mramba mkristo baada ya hapo amfuate mwislam mwenzake Rostam kisha kwa Chenge Mkristo, amtafute Mkapa mkristo amuulize nini issue ya kiwira bila jibu zuri mahakamani mtu kama Daniel Yona na Mgonga badaye Meghji, huku akituondolea takataka kama Makongoro Mahanga, Steve Wasira wakristo kwenye hii serikali lakini naona JK muoga na mdini anakimbilia kusema taifa lipo kwenyeTATIZO la udini. nilidhani alitakiwa kusema taifa limeingia kwenye tatizo kubwa la ufisadi lakini matokeo yake anawachekea na kuwaombea kura ili wale wote pamoja. Makamba = MS
 
Asante Chiefm Tz
Mbona hajamkemea Padri Slaa kwa wizi wa mke wa mtu? au huo si uovu! Kama anaiba mtu mwenzie angekwenda ikulu si hazina angeikausha? Bwana pengo wizi wa mke wa mtu pia ni ufisadi mbaya ukemee tukusikie
 
Hongera mh Pengo. lkn mbona huwa mankemea pale rais anapokuwa muislam tu. na huwa kimya mkiona rais ni mkiritso. zinduka

sijakuelewa mwanangu unachotaka ni nini kwa nini dini usiiweke pembeni umeing'ang'ania kama ndio ufumbuzi wa matatizo tanguliza uzalendo kwa nchi yako kwanza dini ifuate kama vile MWENYEZI Alivyo umba kwanza dunia baadaye kaweka utaratibu wa kuishi humo ambayo ni dini nenda hija pitiliza kukaa hata siku moja utafukuzwa na kuambiwa uislamu kafanyie kwenu hapa kwetu JITAMBUE MWANANGU...
 
Asante Chiefm Tz
Mbona hajamkemea Padri Slaa kwa wizi wa mke wa mtu? au huo si uovu! Kama anaiba mtu mwenzie angekwenda ikulu si hazina angeikausha? Bwana pengo wizi wa mke wa mtu pia ni ufisadi mbaya ukemee tukusikie

Huyo mchumba wa Slaa ni mtu mzima kwa hiyo alikuwa na uwezo wa kukubali au kukataa kuanzisha urafiki na Slaa, yeye aliamua kuwa rafiki. Kwa upande mwingine, mafisadi wanabaka mali ya watanzania kupitia kutotii viapo vyao vya kazi na ahadi watailinda katiba ya jamhuri. Zaidi ya hapo wanapora mali asili na fedha za nchi kupitia nafasi na nyadhifa zao. Kalamazoo, angalia hizo tofauti ubainishe kuwa kuanzisha urafiki na mke wa mtu ni tofauti kabisa na ufisadi utokanao na kudharau kiapo cha kazi na kuiba mali ya umma, na mara kwa mara kwa gharama ya kudidimiza huduma zitolewazo. Athari za ufisadi utaziona kwa watoto kurundikana darasani, wamekaa chini hjawana waalimu, wagonjwa kulazwa wawili hata watatu kitanda kimoja bila kujali aina ya magonjwa, barabara kutokamilika, mrahaba wa wachimba dhahabu wa asilimia tatu wakati Botswana hapo jirani ni asilimia 45. Ufisadi ni tatizo la kiuchumi lakini la kupoka mke wa mtu ni la kisosholojia!!
 
Hiyo midini yenu mngekuwa mnaifuata walau kwa asilimia 20, we wouldn't need to have this conversation.

BTW, viongozi wa dini nao ni sehemu ya tabaka tawala hivyo wote ni walewale tuu..same shyt different toilets.
 
Hongera mh Pengo. lkn mbona huwa mankemea pale rais anapokuwa muislam tu. na huwa kimya mkiona rais ni mkiritso. zinduka

WEWE SASA HADI UNAKERA....YAANI KILA KITU UNA-REFLECT KWENYE DINI....NO.

Aaaaaah...Mimi ni Muislam swafi lakini ndugu yangu umezidi...unataka akina Rev Masanilo na Quinine waje waanza kutukashfu ndio starehe yako? au wewe ni KAFFRRI Hivyo unapenda sana kuona watu wakitoa comment za kuudhal
 
kalamazoo wewe unaturudisha nyuma saaaaaaaaaaaaaaaaaaaaana nina mashaka na unavyofikiri -ufisadi lazima upigwe vita na kila mtu lakini viongozi wa dini kama viongozi wanakemea maovu. Na uovu hauchagua umefanywa na nani kwa sababu , mramba, yona, na wengine wengi wanaolindwa na ccm ni mafisadi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom