Huwezi elewa. Ya Mungu nayafata lkn ya binadamu hapana aisee. Kumbuka Matayo ni binadamu
Yote yalioandikwa kwenye biblia yameandikwa na binadamu!
Kimsingi binadamu walikua wanaongozwa na MUNGU waandike maandiko unayoyaona kwenye biblia uijuayo.
Hawakuandika hivi hivi from nowhere kwa mfano tukiangalia agano la kale tunaona watu walaindika matukio kulingana na mambo yaliyotokea wakati huo pia wapo ambao waliongea na MUNGU kwa namna yao.
Ukija hapa kwenye agano jipya unaona wale mitume waliandika matendo aliyotenda Yesu na habai nyingine waliongozwa na Roho Mtakatifu kuziandika.
Kwa hiyo ndugu yangu basically sio kazi ya wanadamu bali ni kazi ya MUNGU.
Ingelikua wamejiandikia wao kwa namna walivyojisikia wao basi wangeliweka hilo wazi kama Mtume Paulo alivyofanya.
Soma 1 Wakorintho 7:6 "Ninayowaambieni sasa ni mawaidha si amri.........."
Pia anakazi kabisa 1 Wakorintho 7:12 "Kwa wale wengine (Mimi binafsi si Bwana) Nasema hivi...."
Unaona sasa kwa hiyo mistari miwili uonaona kabisa ni meneno ya Mtume Paulo na wala sio Bwana au MUNGU so ukielewa hii hakuna kitakachokkusumbua.
Ukitoa mambo machache ambayo wahusika wamespecify kama Mtume Paulo hapo yote yametoka kwa Mungu na Yesu sio binadamu kama unavydai wewe.
Kwa kifupi binadamu kazi yake ni kufikisha ujumbe wa kile anachoambiwa na MUNGU! Tumeyaona haya kwa manabii kaba Eliya, Elisha, Musa, Daniel n.k
Sidhani kama utapata shida tena hapo.