Ni nani anastahili kuwa MwanaJamiiForums bora wa mwaka?

Ni nani anastahili kuwa MwanaJamiiForums bora wa mwaka?

Nani Mwana JamiiForums bora wa mwaka kati ya hawa?

  • The Boss

  • Faiza Foxy

  • Mzee Mwanakijiji

  • BAK

  • Pasco

  • Heaven Sent

  • Victorie

  • Technically

  • Mshana Jr

  • Lizaboni


Results are only viewable after voting.
Kiaina hii ni kama list ya mleta mada, labda kuifanya ya wote watu wangetoa maoni yao, majina yakachambuliwa kutokea humo...

Labda msaada wetu ni kumtafutia bora kati ya hao anaowafikiria.
 
Habari zenu wakubwa,

Matumaini yetu ni kuwa nyote ni wazima wa afya na mnaendelea vema na shughuli zenu ili kuepuka kusoma namba.

Malengo ya uzi huu ni kuweka utaratibu wa kuweza kupata mwanaJF bora wa mwaka hasa jukwaa la siasa, mambo ya kimataifa na mengineyo.

Mambo yafuatayo ndiyo vigezo vitakavyotumika kumpata;

1. Mwenye hoja na uchambuzi mzuri wa masuala yanayohusu taifa letu kwa ujumla
2. Anayechambua mambo ya kisiasa kwa wigo sawa bila kuegemea au kupendelea upande wowote ule, kaka ni CHADEMA au CCM au CUF yuko tiyari kukosoa kwa hoja haijarishi ni chama chake
3. Mwenye nidhamu juu ya majibu anayowapa wengine na mwenye kujibu bila kubagua au kukejeli wengine na kuwadharau au kuwatamkia matusi(makosa yanayopelekea ban)
4. Mwenye michango mingi ya kuelimisha jamii,
5. Asiye mdini au mkabila wala asiyechanbua kwa kupendelea kabila/dini yake na kukashfu za wengie,
6. Mwenye kuheshimu wengine na mamlaka ya nchi haijarishi kamchagua kiongozi aliyeko madarakan au lah.

Orodha yangu ni kama ifuatavyo, ninyi ndio mtapiga kura kwenye poll na kupata mshindi;

1. The Boss
2. Faiza foxy
3. Mzee mwanakijiji
4. BAK
5. Lizaboni
6. Pasco
7. Heaven sent
8. Victorie
9. Technically
10. Mshana jr

Haimaanishi ambao hawajawekwa hawakuchangia hapana wamechangia sana ila kwa mwaka huu hawakufika viwango vya hawa hapa.

PIGA KURA YAKO.
Mleta Uzi umesema asiyeegemea chama fulani halafu kwa maajabu mtu kama Lizaboni na FaizaFoxy wamo kwa orodha yako
 
Tutazuia vipi wimbi la ukeketaji, wakati ngariba ni Diwani wa kata mwenye kijiji......Mr jf upooo
 
He hee mwamba ngozi huvutia kwake... Hivyo kura yangu ni kwangu[emoji12]

Hapajaharibika kitu maana kwako ni kwangu😛.

Wanakuita Muree, kwangu we ni wa kipekee
Ndo maana yeye na yule, hawaeshi upekepeke
Kila siku kwakwaru, kelele zilezile
Hawamtishi hata kenge, mwenye makazi kwenye pagale
Seuze hili jembe, la Ikungu sabo igembe

Nimemaliza na mic naidondosha.
 
Toa hao akina faiza,lizabon na pasco..ulitakiwa kuweka watu Neutral kama akina Mshanajr
 
Hao waliowekwa kwa vigezo gani? maana hata kwenye list ya like hawana za kutosha zaidi ya kupost upupu tu
 
Mleta uzi haujatenda haki kwa wanajamiiforums kwa ujumla wapo member waliotoa mchango wao wa hali na mali kwa maslahi ya taifa ila hawapo in the list. Kifupi naomba kuwatambua wafuatao:

CHIEF MKWAWA kwa watuamiaji wa jukwaa la Teknolojia watakubaliana nami kuwa huyu ni mtu wa kipekee na mwenye moyo wa kusaidia wengine. Naomba mchango wake utambuliwe kama mtoa ushauri wa masuala ya kiteknolojia bora zaidi jukwaani.

Amesaidia wengi katika kufanya maamuzi sahihi juu ya simu zinazofaa na utambuzi wa simu halisi na kuwakinga members na utapeli. Pia mkuu huyu hujibu maswali yote kwenye uzi na PM. Kwangu mimi anastahili tuzo ya MwanaJF analiyeitumikia Jamii.

Pili naomba utambuliwe mchango wa joka kuu, nguruvi3, Rutashubanyuma Mkandara ,barafu, The bold na BAK kama members bora wanaotekeleza dhana ya great thinking kwa vitendo. Mfuatiliaji wa mijadala iliyoshiba na yenye hoja atakubaliana nami kuwa hawa jamaa hujadili facts backed by data na huweka hoja zilizoshiba Mezani zikiambatana na uchambuzi mujarabu. Hawa wanastahili tuzo ya Great Thinkers of the Year.

Tatu wapo wanaowakilisha jamiiforums kweye anga la kimataifa wakitanguliza maslahi ya taifa mbele. Hawa ni wazalendo wa kweli na hututetea bila kuchoka na kuteteleka, hawa ni wanajeshi wetu katika at ardhi ya ugenini wakipigana vita dhidi ya propaganda chafu na kutangaza mazuri ya taifa letu kwenye majukwaa ya ughaibuni. Kwangu mimi JF Foreign Dignitary Award of the Year goes to Geza Ulole.

Kundi la mwisho ni kundi la maripota bora wa mwaka. Watu hawa wametuhakikisha kauli ya be the first to know kama ilivyoada yetu. Tuzo hii pia naomba iende kwa live coverage reporter wa mwaka. Am honoured to nominate Mwanahabari Huru kama best reporter of the Year na mwanaJF Francis12 kwenye category ya live coverage reporter of the Year.

Wa mwisho kabisa ni mwanaJF aliyeimpact maisha ya wanaJF na Watanzania kuondokana na umasikini na kuingia kwenye ujasiriamali. Yupo mwanaJF ambaye alitumia platform hii kuhubiri ujasiriamali na kufundisha ujasiriamali kwa vitendo. Mjasiriamali huyu leo hii ameunganisha mamia ya WanaJF na jamaa zao kufungua makampuni na kuwekeza kwenye kilimo, ufugaji na mazao ya misitu. I am humbled to represent JF Entrepreneur of the Year Mr. Malila


Ombi langu kwa uongozi wa JF kama mna funds ningependelea muwaaward members hawa kwa mchango wao uliotukuka.
 
Back
Top Bottom