Ni nani hasa huitumia ndege ya Rais wetu 5H- ONE Gulfstream G550 maana inaonekana ikizurula tu mikoani na kupaki Zanzibar?

Hii ndege ya rais iliyonunuliwa kwa bei ya $40,000,000 kwa nini haikutumika kumpeleka rais Belgium/France na nchi nyingine za magharibi na badala yake inazurura tu mikoani pasipo kuwa na ratiba maalamu.

Sisi walipa kodi tuna haki ya kujua ndege iliyonunuliwa kwa hela zetu kwa nini inazurura kila mahali wakati rais anapanda Air Tanzania au Emirates.

Na kama kuna mtu fulani anaitumia basi tupaswe kumjua, maana isije kuwa inatumika kufanyia biashara za magendo, ama kutumiwa na baadhi ya watu kufanya starehe/ufuska au ndio imekwisha kabidhiwa ramsi kwa Raisi wa Zanzibar kama ndege yake binafsi maana haiwezekani ukiangalia kwenye Flight past history unapata taarifa za ndege hiyo kuzurula sana Kilimanjaro na mikoa mingine ila inarudi kulala zanzibar

Mwenye ufahamu tunaomba atujuze, Nawasilisha.

Hapa chini ni tracking past flight history ya ndege ya Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

View attachment 2128144

kipi hapo kinaonesha kua hiyo ni ndege ya rais iliofanya safari hizo?
 
Asante sana kiongozi kwa kutrack ujambazi unaendelea kwa kutumia ndege ya rais, hizo sehemu zina madini ghafi kwahiyo hilo dege linatumika kuyavusha bila kibali na bila bughudha na kuyapeleka Zanzibar, watanzania tuamke kutoka usingizi wa pono.
hebu niambie ndugu, hapo ni kipi kilichokufanya ufahamu kua hiyo iliofanya safar hizo ni ndege ya rais
 
kipi hapo kinaonesha kua hiyo ni ndege ya rais iliofanya safari hizo?
Unaifahamu hii ndege

72704B24-4FDF-4670-A1D2-BC9E6418AE19.jpeg
 
hapo lazima tufuatilie kwann,inaonekana kulala zbar Mara kwa Mara!!? Halafu root zenyewe niza maeneo potential kwa madini,ndovu n.k. final destination ya hii ndege kulala ni eidha dar au Dodoma ,maana ndiko ikulu ziliko. huko zbar vipi tena!!??

tunashindiliwa vitu vizito vichwani watz.
Mama yenu hana ajualo!,

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
 
Tarehe 12 saa 09:38am ilikuwa Klm/jro na saa 09:59am ikawa Zanzibar, je dakika 20 ndege yaweza kufika Zanzibar?
Nijuavyo kutoka Jro to Znz kwa airbus au dreamliner ni dkk 50 to 55 na pangaboi hadi dkk 60, je hizi taarifa zina ukweli?
Nadhani unapata mkanganyo ila neno last seen lina maana zaidi
 
Hii ndege ya rais iliyonunuliwa kwa bei ya $40,000,000 kwa nini haikutumika kumpeleka rais Belgium/France na nchi nyingine za magharibi na badala yake inazurura tu mikoani pasipo kuwa na ratiba maalamu.

Sisi walipa kodi tuna haki ya kujua ndege iliyonunuliwa kwa hela zetu kwa nini inazurura kila mahali wakati rais anapanda Air Tanzania au Emirates.

Na kama kuna mtu fulani anaitumia basi tupaswe kumjua, maana isije kuwa inatumika kufanyia biashara za magendo, ama kutumiwa na baadhi ya watu kufanya starehe/ufuska au ndio imekwisha kabidhiwa ramsi kwa Raisi wa Zanzibar kama ndege yake binafsi maana haiwezekani ukiangalia kwenye Flight past history unapata taarifa za ndege hiyo kuzurula sana Kilimanjaro na mikoa mingine ila inarudi kulala zanzibar

Mwenye ufahamu tunaomba atujuze, Nawasilisha.

Hapa chini ni tracking past flight history ya ndege ya Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

View attachment 2128144
Umempata wapi signals
 
Parachuti la injini moja ni kama lile alilotumia dada yake Lisu (kutoka ubelgiji) kuizunguka dunia na kutokea tena Belgium 2021. Alichelewa zaidi urusi na Japan baada ya China mawasiliano kukwama
 
Hii ndege ya rais iliyonunuliwa kwa bei ya $40,000,000 kwa nini haikutumika kumpeleka rais Belgium/France na nchi nyingine za magharibi na badala yake inazurura tu mikoani pasipo kuwa na ratiba maalamu.

Sisi walipa kodi tuna haki ya kujua ndege iliyonunuliwa kwa hela zetu kwa nini inazurura kila mahali wakati rais anapanda Air Tanzania au Emirates.

Na kama kuna mtu fulani anaitumia basi tupaswe kumjua, maana isije kuwa inatumika kufanyia biashara za magendo, ama kutumiwa na baadhi ya watu kufanya starehe/ufuska au ndio imekwisha kabidhiwa ramsi kwa Raisi wa Zanzibar kama ndege yake binafsi maana haiwezekani ukiangalia kwenye Flight past history unapata taarifa za ndege hiyo kuzurula sana Kilimanjaro na mikoa mingine ila inarudi kulala zanzibar

Mwenye ufahamu tunaomba atujuze, Nawasilisha.

Hapa chini ni tracking past flight history ya ndege ya Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

View attachment 2128144
Tunakushukuru mno. Lazima kuna Jambo limefichika huko. Na mleta mada ninaomba damu ya Yesu ikulinde na familia yako. I smell a rotten fish. Hiyo mikoa ni potential Sana. Usiniulize.
 
Back
Top Bottom