Ni nani mwenye jukumu la kupendezesha kijijini kwenu?

Ni nani mwenye jukumu la kupendezesha kijijini kwenu?

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
41,558
Reaction score
64,966
Wengi hatuendi vijijini tulipo toka kutokana na labda mazingira sio rafiki.

Inawezekana labda, bado kuna nyumba za nyasi, udongo, choo kisichokuwa na ushirikiano, hakuna umeme, au mazingira ni machafu.

Ingawa huku mjini tunajimwambafai kuwa tuko vizuri, kwa kuendekeza starehe, kujifanya wasomi, tuna mijengo mizuri n.k

Lakini kijijini tunakotoka tuna miezi, miaka hatujawahi au hatutaki kwenda kutokana na sababu tulizonazo.

Sasa, wewe unategemea ni nani mwenye jukumu la kupendezesha kijijini kwenu?​
 
Kutokana na nilipo umeandika mada muhimu sana, maana niliyoyaona yanasikitisha mjini watu wazito lakini twende kijijini kwao wanapoishi wazazi wao ni aibu, miaka hii choo hakina ushirikiano watu tunajisaidia kwa kuchimba kishimo
 
Hii changamoto nimekutana nayo karibia vijiji vingi sana
 
Watu wengi waliofanikiwa mjini wamebadilisha pia kijijini
Kama kuna mtu anatamba mjini na anapakimbia kwao huyo ameshika hela za kula tu au pesa za haraka ambazo huwa zinapita
We wachunguze tu, wanaweza kwenda kijijini mara moja kwa mwaka au hakuna kabisa
 
Wengi hatuendi vijijini tulipo toka kutokana na labda mazingira sio rafiki.

Inawezekana labda, bado kuna nyumba za nyasi, udongo, choo kisichokuwa na ushirikiano, hakuna umeme, au mazingira ni machafu.

Ingawa huku mjini tunajimwambafai kuwa tuko vizuri, kwa kuendekeza starehe, kujifanya wasomi, tuna mijengo mizuri n.k

Lakini kijijini tunakotoka tuna miezi, miaka hatujawahi au hatutaki kwenda kutokana na sababu tulizonazo.

Sasa, wewe unategemea ni nani mwenye jukumu la kupendezesha kijijini kwenu?​
Hayo yote tunapendelea wafanye Lissu na Heche.Mola akubariki sana.
 
Hiyo labda vijiji vya huko kwingine lakini kwetu Kaskazini kijijini kwetu chaka huko kuna mijengo kibao, ukiingia mwanzo utakutana na miti lakini ukizidi kuingia ndani huko ndo utachanganyikiwa zaidi nyumba za maana na zinatisha, ubaya ni kwamba hazina watu wengi wanaokaa maana familia nzima utakuta Kila mmoja Yuko mjini wengine abroad huko....
 
Ukitaka uone vituko, fanya kazi ya kuhesabu watu yaan sensor afu ufanye kijijini, wooi! Ni shida bin taabu tupu. Usione mjini mtu kapendeza kila sector kwao kijijini acha tu.
Kuna cku tumeenda mkoa flani ukiambia hapa ni kwa akina flani huamini kabsaa. Mimi ushauri wangu kama unajiweza mjini wezesha na kijijini kwenu hata kwa kujenga nyumba ndogo tu na choo ndo ukae kwa amani mjini muache kusingizia wachawi
 
Back
Top Bottom