Ni nani waliongeza cha juu kwenye manunuzi ya ndege ya mizigo?

Ni nani waliongeza cha juu kwenye manunuzi ya ndege ya mizigo?

Kwenye bili ya dola 37 elfu ikaongezwa cha juu dola 49 elfu [emoji23] halafu watu kama hawa uwaambie kuhusu katiba mpya watakuelewa kweli
Mshana naungana na wewe watu walioko madarakani ndo wanaoiba hela na rasilimali za umma,alafu wanatumia hela hiyo hiyo kukwamisha baadhi ya Mambo yasiende mfano kukwamisha kuwepo kwa katiba mpya itakayo kuwa na meno ya kutoa adhabu kali kwao.
Pili Mama alijitenga sana na kundi alilolikuta kwenye uongozi kawatoa wote,karudisha kundi la wale wapigaji na watu wenye dharau kwa taifa,tusishangae hizo pesa pia zikakaja kumwondoa yeye kwenye Nafasi ya uenyekiti na uraisi.
 
Shirika la ndege la Tz alijawahi kuleta faida yoyote na hasara ya ma billion hiyo pesa ingewekezwa kwa kupeleka maji vijijini huenda maisha ya mtazania wa kawaida yange badilika.
Serikali haiwezi kufanya biashara. Period.
 
Wanafahamu mama anaweka safi yake mpya,Toka ameingia urais hivyo watu wanapita parefu maana wanakula muda wowote wanatolewa
 
Mkuu kujuana ni kwingi sana kwahiyo sioni mtu yoyote wakuwajibishwa kwa hili. Kwa ike kauli alozungumza inanipa uhakika zaidi ya 90% hamna hatua stahiki zitachukuliwa.

Manunuzi ya kiserikali hasa ya nje ya nchi yana chain ya watu weng sana. Sasa wote mpaka sasa ingetajiwa wapigwe ban alafu hatua nyingine zifuatwe
 
Adi siku itokee watanzania wote tuhame kwa muda wa mwaka 1 alafu waje mabeberu hapa for just a year,tukija kurudishwa nchini kwetu tutapoteana mana hutajua buza wapi,bunju wapi,masaki wapi yani maji safi kila sehemu,hospitali hujui ipi private ipi public zote nzuri,shule sasa yani kuanzia social services mpaka infrastructure zitabadilika na hapo ndo watanzania tutaanza sasa kuishi mana sa hivi tunasogeza siku tu!
Kama hili haliwezekani basi tusubiri tu raha za mbinguni mana hapa TZ haiwezekani tena mana zipo kwa wachache!
 
Makosa ya Boeing asibebeshwe mteja, tena mteja anayenunua ndege moja.

 
Tatizo mama analalamika sana. Hii nchi bwana, wananchi wanalalamika, viongozi wenye dhamana nao wanalalamika!! Sasa ni kulaumiana tu na mambo hayaendi.
Viongozi kuendelea kulalamika ni ishara tosha kuwa nafasi walizo nazo hawastahili.
 
Baada ya ulafi wa mali za umma kuanikwa na CAG, hakika rais wetu Samia anatakiwa asaidiwe pakubwa na kwa haraka, ikiwemo kumwombea Mungu ampe ujasiri, akili na hekima itokayo juu.

Kakwama kabisa na kuishia tu kulalamika na kutukana: "...stupid..., ...pumbavu..."!

Nani ataogopa kuendelea kuiba na kula fedha za umma kwa kulalamikiwa na kutukanwa tu bila kuchukuliwa hatua kali za kinidhamu na kisheria?!

Credit: Gwappo Mwakatobe
Mama rasmi ameonyesha hana uwezo wa kupambana na wapigaji..
Watampekenyua mpaka kilemba this time.
 
Back
Top Bottom