Ni nani waliongeza cha juu kwenye manunuzi ya ndege ya mizigo?

Ni nani waliongeza cha juu kwenye manunuzi ya ndege ya mizigo?

Hawezi, mkono wa mstaafu uko hapo.

Narudia tena, hawezi.

Hakuna wa kufukuzwa hata mmoja.

Mama kama angekuwa na uwezo huo hakupaswa kutoka na kutuambia. Tulitakiwa tuone watu ni fired bila sisi kujua kinachoendelea. Ndo uongozi.

Mama aliona Magu hana huruma. Akasahau kuwa hii nchi ina wajanja fulani wanaendesha nchi kama choo binafsi.

Atamkumbuka Magu, na nchi ishamshinda. Watu wanapekenyua hadi kilemba chake.
Hivi ile trillion 1.5 iliyomfukuzisha kazi Assad iliishia wapi?

CAG alipotaka kuhoji gharama za manunuzi ya ndege (ambazo hazikuidhinishwa na bunge na Wala haikutangazwa zabuni kama Sheria ya manunuzi ya umma inavyotaka) akaambiwa aende ikulu yaani aachane na hiyo issue hukuona hilo? Bunge liliidhinisha ujenzi wa Chato International Airport? Kandarasi ya ujenzi ilitangazwa Ili makampuni ya ujenzi yashindanishwe? Kadhalika Burigi national park n.k n.k? CCM haikuwahi kuwa na msafi acha kujidanganya
 
Sema mama analalamika sana na hakuna watu wakumsaidia, huwezi ukasikia kuna chombo chochote cha serikali hasa polisi au takukuru kuwa wanafanyiakazi report ya jana.Hii nchi hatutafika kamwe..yaani kuanzia JUU mpaka CHINI wote wanalalamika
Si mliambiwa bunge lenu ni dhaifu mkaishia kum harass CAG Prof Assad na kumfurusha ofsini kibabe
 
Tanzania tatizo siyo viongozi,tatizo ni sisi wananchi tumelala sana katika maswala mazima ya kuhoji ,wanatuchezea sana hawa jamaa,magufuli alikuwa hapendwi na viongozi wenzake kwa kuwa aliwabana,EE MUNGU NAPIGA GOTI TULETEEE MAGUFULI MWINGINE,PAMOJA NA MAPUNGUFU YAKE AMBAYO NDO YALIKUWA YANAKAMILISHA UBINAADAMU WAKE,LAKINI YULE MTU ALIKUWA ANAJUA, tanzania rais akiwa mpole sana wanamuonea sana hawa watu wa serikalini ,na hela wanazoiba ni za wananchi so mean hawana upendo na sisi,,asante sana rais samia kwa kutamka haya hadharani, natamani ningekuwa na elimu ya kutosha then niwe sehemu fulani,hakika mngenyooka,mi sijali kuuliwa kwani hakuna atakayebaki hapa,na yoote haya ni matakataka ya dunia
Unamzungumzia yule mpigaji wa trillion 1.5 au
 
Hasara za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kwa miaka 9 (2014-2022)

2014/2015 - Tsh. Bilioni 94.3
2015/2016 - Tsh. Bilioni 109.2
2016/2017 - Tsh. Bilioni 113.8
2017/2018 - Tsh. Bilioni 26.6
2018/2019 - Tsh. Bilioni 48
2019/2020 - Tsh. Bilioni 60.24
2020/2021 - Tsh. Bilioni 36.2
2021/2022 - Tsh. Bilioni 35.2

Ripoti za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), zimeendelea kuonesha Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) limeendelea kupata hasara tangu Serikali ilipoamua kulifufua kwa kununua ndege mpya 12.

ATCL imekodishwa Ndege 11 zilizonunuliwa kwa Tsh. Tril 1.47 zinazotoa huduma ya Usafiri sehemu mbalimbali ndani na nje ya Nchi, baadhi yake zimepata hitilafu za kiufundi na 1 inashikiliwa Nchini Uholanzi.
Hapa katikati si tuliambiwa ATCL imepata faida wakatoa na gawio[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Tukiwaambia hii nchi inataka mkono wa chuma kuiendesha mnaanza kulalama, mkono wa huruma na kubembelezana kwa walafi wa mali za umma kwa namna hii then tunasema "Mungu anawaona"?

Watu tunakatwa kodi kubwa, maisha yanazidi kuwa magumu lakini kuna walafi wachache wanaangaliwa tu eti tunataka "utawala wa sheria", mijitu mijizi na milafi unacheka na kuibembeleza kweli in the expense of millions of Tanzanians who toil blood to make ends meet?

Haya, tusubiri wao ndio wajiuzulu, inakasirisha sana aisee. From 37b to 88b, that's not even 100%, huu ufisadi unahitaji mtu brave sana kupambana nao.
Sio mtu tunahitaji mifumo narudia tunahitaji mifumo thabiti
 
Mipuuzi itaanza kusema aliyeweka cha juu ni JPM inadhani na sisi ni ndondocha kama myenyewe
Hahahah hamtaki JPM aguswe kabisa, hivi Prof Assad alipohoji gharama za manunuzi ya ndege na upotevu wa trillion 1.5 akaliwa kichwa ilikuwa ni utawala wa nani vile
 
Hahahah hamtaki JPM aguswe kabisa, hivi Prof Assad alipohoji gharama za manunuzi ya ndege na upotevu wa trillion 1.5 akaliwa kichwa ilikuwa ni utawala wa nani vile
Tatizo hamkumjua JPM au kwa kutojua au kwa makusudi. Nitaanzisha sredi kuhusu ukweli wake
 
Haya mambo kipindi cha numa yalikuwa yanafichuliwa na vyama vya upinzani lakini saiv imekuwa tofauti...R.I.P upinzani
Na ndio maana inasemwa,asiyeutaka upinzani huyo ni mwizi bobezi anayetaka madudu yake yasiwekwe hadharani.
 
Tatizo hamkumjua JPM au kwa kutojua au kwa makusudi. Nitaanzisha sredi kuhusu ukweli wake
Tatizo mahaba yanakupofusha, angalia ripoti ya CAG Toka 2014 ATCL inapata hasara ya mabilioni ya pesa ila hapo katikati tuliambiwa ATCL imepata faida wakatoa na gawio? Halafu Kwa Nini ripoti ikionyesha ubadhilifu wa kuanzia 2016-2020 mnachukia na kusema sio kweli ila ukionyeshwa wa sasa mnafurahi sana
 
Back
Top Bottom