Dah Mimi sio mwanasiasa, ila jambo lililotokea Leo limeniuma sana, nimewaza leo yanatokea kwa wenzagu kesho yanaweza kutokea kwa Familia yangu au watoto wangu, Mwisho nitaishi kwa visasi na chuki..
Naona hii sio siri tena, walioko madarakani hawataki kuachia kwa namna yoyote ile, tumekubali kuishi kwenye mfumo wa wanasiasa kuishi maisha ya kitajiri, huku maskini akizidi kukandamizwa.
Mbaya zaidi maskini wenye uniform, wanawapiga maskini wenzao ili matajiri waishi vizuri, je tumechagua huu mfumo wa kuishi?
Nimeona taarifa Moja, mtu mmoja ameuliwa na police, huku naibu katibu mkuu amani, akijeruhiwa saana,..
Hivi Hawa police wanadhani chadema wanafanya yoote kwa faida ya nani?
Hawaoni jinsi wanasiasa na mawaziri wakijitajirisha huku wao wakiwa na maisha ya chini ya hovyo? Na mwisho wa mwezi akipokea laki mbili baada ya mkopo?
Hapana aisee hii sio sawa,..bahati mbaya nchi nyingi za kiafrica ndiyo maisha viongozi waliochagua kuishi...