Ni ngumu sana kufanya biashara ya Familia kwa wakristo, biashara za Familia tuwaachie waislam?

Ni ngumu sana kufanya biashara ya Familia kwa wakristo, biashara za Familia tuwaachie waislam?

Wakristo hata biblia ipo kwa kiswahili tamaduni hadi uvaaji ni wa kiswahili ila nyie ni too much kujiona kama wasaudi punguzeni
Tamaduni zipi? uvaaji upi ndio ni utamaduni wa Kiswahili?

Unataka wanawake wavae vimini na kuacha maziwa nusu nje? umewahi kuona picha za Mother Teresa anavyovaa?
Unawaona masister huko Kanisani wanavyo vaa?
 
Tatizo la waislam wengi weusi wanajichukuliaga waarabu kama ndugu zao yaani wakiona maisha ya waarabu ndio wanajiona kama ndio wao kumbe waarabu wana falsafa tofauti kabisa na ndio maana hawataki kabisa kuowana na watu weusi
Wajinga tu.
 
Mweusi ni mweusi tu hana mawazo mapana ya biashara
 
Biashara huwa zinarithishwa kwa watoto hasa wa kiume wanaoendeleza kizazi lakini kwa wakristo hali ni tofauti, Baba akifa nusu ya mali zinaenda kwa mke ambae anaweza akawa hajui chochote kuhusu biashara, hapo ataona heri auze biashara ili apate pesa za kuendeleza huko kwao na akatoe sadaka kwa Mwamposa, biashara inakufa kifo cha mende.

Tukija kwa waislam mke anapewa Asilimia 10 tu ya mali, mali kwa Asilimia kubwa zinabaki kwa watoto wa kiume wanaoendeleza kizazi, mabinti wanaenda Kuendelea vizazi vya wengine hupewa nusu ya mali wanazopata watoto wa kiume. Hivyo watoto wa kiume kupewa kipaumbele kurithisi sehemu kubwa kuna uwezekano wa kuendeleza biashara.

Hata wazungu ukiangalia wamefanikiwa zaidi lakini biashara za Familia zimekuwa ni tatizo kwasababu mifumo ya kifamilia inawakandamiza sana kina baba, mama akifungua mdomo kidogo tu anapewa nusu ya mali zote na watoto, ndio maana unakuta wakifariki biashara zao zinamilikiwa na watu wengine, hata urithi wao wakifa wanaona heri wagawe kwa mashirika ya misaada. Tajiri kama. Bill gates hatawaachia chochote watoto wake, mke wake alishamuacha akapunwa matrilioni ya mgao wa mali.
wewe na akili yako kwan we hujui walaka wa urithi??
Kuna ndoa inalazimisha umuachie mkeo mali? au ni sheria ua nchi ya mirathi?

mtoa maada jielimishe elimu na uelewa wako mfinyu sana hukupaswa hata kuanzisha uzi ulibiid uwe msikilizaji au ungeuliza swali ueleweshwe kuliko kuandika usichokijua
 
Sio waarabu tu, uislam ni mfumo wa maisha, Kuna Familia za kiislam nazijua watoto wa kiume ndio wanaoendeleza biashara za baba zao kama real estate, mashamba, logistics, n.k. Watoto wa kiume wanaoendeleza kizazi ndio wasimamizi wakuu.

Kwa wakristo ni ngumu hii, mke anapewa nusu ya mali zote anaweza kuziuza zote ajenge kwao, watoto wa kike wanaoendeleza vizazi vya watu wa nje nao wanapewa mali Sawa na watoto wa kiume,
Oya hii nadhani ni report ya familia yenu au mtu wa karibu eeh?

Ninavyojua mimi katika ukristo hakuna formula rasmi ya hayo mambo na kama ipo watu hawafanyii kazi kivile.

Wengi wanarudi katika maelekezo ya marehemu, sheia ya nchi au mila/tamaduni.

Halafu turudi kwa sisi watu weusi wa kitanzania, suala la biashara ya familia naweza kusema ni asilimia 10 tu bila kujali kabila ndio wameweza kuendeleza na kufanikiwa.

Wengi wanagangia njaa tu kwa kukosa mishe nyingine.
Mtoa mada akomae aanzishe yeye na aweke misingi hiyo, mambo ya kurithi ni ya wachache, hela zianzie kwa babu huko, baba ashike kijiti vizuri, kisha ampe mtoto baada ya kumuandaa
 
Back
Top Bottom