PreGE2025 Ni ngumu sana Sugu, Wenje, Mbowe kubakia CHADEMA hii yenye msimamo mkali ya Lissu na Heche

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Mungu ataamua huu ugomvi soon, ni suala la muda tu.
 
Msimamo mkali uko wapi wakati chama kwa ujumla wake waliamua no reform no election? Kwa nini sasa ionekane ni msimamo wa lisu na wenzake.Matamshi ya mtu hayawezi kuwa msimamo mkali sana sana kujilinda dhidi ya uonezi wanaoupata;kwani wewe hufahamu chama kinavyoandamwa? Unategemea waongee lugha gani kama sio ya kujilinda?
 
Uko sahihi, nimeandika kwa tumekwisha!Labda saratog ya USA iambae Indian ocean! hivi hivi hatoki....kumnyonga hapana, watamshikilia mpaka may be end of uchaguzi
Ataachiwa tu. Hana impact yeyote zaidi ya kujaza watu kwenye mikutano yake. Hasa kwa vile chama chake hakitaingia kwenye uchaguzi.

Amandla...
 
Sijaelewa maana yako ni nini hasa na mada hii, hasa ulivyo malizia na huo mstari wa mwisho.

Inaelekea utakuwa ni sehemu ya kujipa matumaini kwamba CHADEMA watadhibitiwa kwa nguvu ya dola, na ikisha kuwa hivyo, CCM itaendelea kwa raha zake yenyewe.
Unacho sahau ni kwamba si CHADEMA pekee ndio wanaodai mabadiliko. CHADEMA ni sehemu tu ya waTanzania wengi wanaoona mambo hayaendi ipasavyo. CHADEMA kama chama, na viongozi wao wanaunganisha tu juhudi za waTanzania kukataa uovu huu unaoendeshwa nchini mwetu sasa, kwa kutumia jina la chama kitukufu cha CCM.
Elewa pia kwamba, hata huko huko ndani ya CCM kume3anza kuwa na maswali mengi ya kujiuliza chama chao kinakoelekea.
Chama kimetekwa na GENGE la waovu, chini ya Samia Hassan Suluhu; GENGE hilo sasa linatumia jina la chama kama ngao tu huku likifanya uovu kwa waTanzania.
Kwa hiyo, hata hao viongozi walioko huko ndani ya CCM, ambao kwa muda mrefu wamekaa kimya wakiona chama chao kikipotea njia, na hawakusema chochote kwa kulinda maslahi yao, nao sasa wataanza kuhoji mwelekeo wa chama chao. Hatimae na wao itawabidi waachane na maslahi binafsi, waangalie maslahi ya taifa lao.

Kwa hiyo, hayo matumaini mnayojipa kwa kutegemea uliyoandika katika huo mstari wa mwisho, utakuja kuwa ni jinamizi kwenu nyote mnaoyategemea hayo yatokee na kuwaacha nyinyi mkiendelea kulihujumu taifa hili.

Be Warned!
 
Mbowe Sugu na Wenje ni watu wanaoiangalia siasa kama Bidhaa in capitalist lenses tofauti na Lissu aliyejikita kwenye Justice only.
 
Mtu yeyote mwenye akili timamu hawezi kuongozwa na Braza K Mapovu anatekeleza maslahi ya vibaraka wa nje.
 
Mbowe haondoki Chadema. Akiondoka CDM itayumba sana na yeye anakipenda sana. Ndio maana watu kama Mnyika na Boni Yai wanatumia nguvu sana kuaminisha umma kuwa Mbowe hahusiki na G-55.

Amandla...
 
Ataachiwa tu. Hana impact yeyote zaidi ya kujaza watu kwenye mikutano yake. Hasa kwa vile chama chake hakitaingia kwenye uchaguzi.

Amandla...
OOoooh!

Wewe na huyo mkuu 'Retired', hadi mmejishusha hadi kwenye ngazi hii? Kwa sababu zipi hasa, watu wenu kuondolewa kwenye uongozi?
Hawa watu wenu kuwa kwenye uongozi ni muhimu zaidi ya kupigania maslahi ya nchi hii, kweli?

Mnakosea sana, kama mnadhani mapambano haya ni ya Tundu Lissu, Heche na wengine waliochukuwa uongozi wa chama.
Haya ni mapambano ya waTanzania dhidi ya GENGE linalokishikilia chama Cha Mapinduzi sasa hivi chini ya Samia Suluhu Hassan.

Ningewaelewa vizuri, kama na nyinyi mngeunga juhudi hizi za waTanzania.
 
Hao wamejazana sana huko ndani ya CCM; ndiyo maana imetufikisha hapa.
Kuna haja gani ya kuhangaika huko nyikani wakati CCM tayari ipo kukupa shibe yako unayoitafuta!
 
Kwa hiyo wote tusiowaunga mkono sio watanzania?

Amandla...
 
Hao wamejazana sana huko ndani ya CCM; ndiyo maana imetufikisha hapa.
Kuna haja gani ya kuhangaika huko nyikani wakati CCM tayari ipo kukupa shibe yako unayoitafuta!
Hapo kwenye shibe siungani na wewe mkuu. Issue hapa si kula na kushiba, ni hii cake tuliyoikuta kuila kwa pamoja. Haiwezi kugawiwa sawa ila basi iliwe kistaarabu kila aliyezaliwa TZ afaidike nayo. Cake inafujwa sana mkuu. Japo binafsi nilishatoa kabisa akilini kuwa eti kuna mwanasiasa anapambana kwa ajili yangu ili mm niishi vizuri, ila bado ninaamini kuwa wanahitajika watu wa aina ya upinzani kuchagua siasa kuwa maisha yao kuwashtua watawala wanajisahau sana
 
Vipi kuhusu waliokuwa wakizikubali sera za hayati Magufuli? Wanaokubali sera za huyu wa sasa!?
 
Mbowe Sugu na Wenje ni watu wanaoiangalia siasa kama Bidhaa in capitalist lenses tofauti na Lissu aliyejikita kwenye Justice only.
Na ndivyo ilivyo siasa ya kileo. Lisu bado yuko kwenye siasa za akina Patrice Lumumba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…