Ndugu
Lwiva naomba niwe na mtazamo tofauti kidogo hapa kwenye hili la kuilaumu JF (kwa maana ya wamiliki na wafanyakazi)
Mimi binafsi naona wanapambana sana na kwakweli wanajitahidi mno kuuwezesha huu mtandao kubaki hai hata wa leo
Kuna changamoto kubwa sana zisizosemwa popote wala kuwekwa hadharani wanazopitia kutokana tu na maudhui ya wanachama wake kwakuwa wao ndio wa kwanza kuulizwa
Sisi tunatumia utambulisho bandia hapa upenuni lakini uhalisia wetu wetu wote wanao wao na ndio walinzi wetu wanaotulinda.. Kuna nyakati walikuwa tayari kuumizwa na kuteswa lli tu kutulinda sisi wanachama wake
Hiki kitu kinaitwa SERIKALI kioneni hivihivi, tutanietanie tu hapa lakini kuna mipaka yake.. Serikali ina mikono mirefu sana na nguvu nyingi sana
Kuna baadhi ya maudhui yanaondolewa kwa faida yetu wenyewe, afya ya forum na ulinzi wa wamiliki na wafanyakazi wake.. Mimi na wewe inaweza kuchukua muda kufikiwa na ile mikono mirefu lakini sio wao wamiliki na wafanyakazi.. Wao kudakwa ni dakika tuu
Inawezekana kweli kuna mahali kuna mapungufu lakini sisi sote si wakamilifu.. Ni vema tuwatie moyo na ikibidi tuwashukuru na kuwapongeza maana wanayopitia pengine ni makubwa kuliko tunavyolaumu
Mungu ibariki JF