Ni nini kifanyike pale tunapoona mtu anatekwa au kuchukuliwa na watu pasipo ridhaa yake ?

Nehemia Kilave

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2022
Posts
1,414
Reaction score
3,118
Habari wana JF ,natumaini mu wazima wa afya .

Miaka ya hivi karibuni kumekuwa na matukio mengi ya watu kuonekana wanachukuliwa kwa nguvu au kutekwa na kupotea kabisa .

Kubwa zaidi katika matukio hayo kunaonekana kikiwa na watu pembeni wakishuhudia matukio hayo huku muhusika akipambana peke yake

Je ni sahihi mtu kuchukuliwa kwa nguvu hata kama itakuwa ni vyombo vya usalama ? Kama sio nini kifanyike kwa wanao shuhudia haya matukio?

Je tuwaombe hawa watu utambulisho kutoka kwa viongozi wa mitaa

Je tutumie umoja na nguvu kuzuia hilo jambo lisitokee

Je tuombee NIDA na vitambulisho vya wanaofanya zoezi hilo la ukamataji ?

Au ni sahihi tuache wahalifu wakamatwe ,tatizo tutajuaje wanaomchukua muhaligu ni wanausalama .​
 
Huo utaratibu wote wanaujua na wasomea. Wanafanya wanachojua kwa malengo mengine
 
Kama unaweza rikodi tupia mitandaoni esp magroup ya whatsapp na FB ya wambea na wenye viherehere, wale waandishi wa kujitolea, utamuokoa.
 
Ukisimamishwa na polisi tii, sheria,hili litasaidia polisi wetu kutotumia nguvu za ziada!
 
Kwanza lazima tujiridhishe kuwa huyo anayekamatwa tuna mfahamu au tuna taarifa nae zozote,isijekuwa tunaingilia kazi ya polisi kukamata mtuhumiwa hatari anayetafutwa muda mrefu sana.

Pili, haina haja ya kugombana na askari ambao wapo kazini ila kuna umuhimu wa kufahamu taarifa za awali ambazo hazitazuia askari kufanya kazi yao, mfano kujua kwann mtuhumiwa anakataa kuwekwa chini ya ulinzi wa askari na je,wamemwambia kuhusu tuhuma zake.

Kwasasa tupo kwenye hali ya sintofahamu kama wanajamii kwasababu kuna matukio ya utekaji wa raia ambayo askari au jeshi la polisi wanahusishwa na wao kutonyoosha maelezo yao juu ya hizo taarifa.

Kama raia tunaowajibu na jukumu la kulindana na kuilinda jamii bila kwikwi yoyote lakini muhimu zaidi ni kuzihoji mamlaka na idara husika juu ya ukimya wao kwenye hizi tafrani zinazotukia na kuharibu utulivu na amani kwenye jamii.
 
Wewe kama muoga muoga,rekodi tu hakikisha sura zao zinaonekana,ili akipotea mazima, ndugu tujue tunawamaliza vipi hao watekaji!! Dawa ya moto Ni moto!
 
Habari wana JF ,natumaini mu wazima wa afya .

Miaka ya hivi karibuni kumekuwa na matukio mengi ya watu kuonekana wanachukuliwa kwa nguvu au kutekwa na kupotea kabisa .

Kubwa zaidi katika matukio hayo kunaonekana kikiwa na watu pembeni wakishuhudia matukio hayo huku muhusika akipambana peke yake

Je ni sahihi mtu kuchukuliwa kwa nguvu hata kama itakuwa ni vyombo vya usalama ? Kama sio nini kifanyike kwa wanao shuhudia haya matukio?

Je tuwaombe hawa watu utambulisho kutoka kwa viongozi wa mitaa

Je tutumie umoja na nguvu kuzuia hilo jambo lisitokee

Je tuombee NIDA na vitambulisho vya wanaofanya zoezi hilo la ukamataji ?

Au ni sahihi tuache wahalifu wakamatwe ,tatizo tutajuaje wanaomchukua muhaligu ni wanausalama .​
Nadhani suluhu ni raia kuruhusiwa kumiliki silaha ikiwezekana ziuzwe kwa bei ya ruzuku. Kwa tulipofikia serikali imeshindwa kutulinda ni bora tujilinde. Unadhani zakaria bila kuwa na bunduki leo angekua hai?
 
Habari wana JF ,natumaini mu wazima wa afya .

Miaka ya hivi karibuni kumekuwa na matukio mengi ya watu kuonekana wanachukuliwa kwa nguvu au kutekwa na kupotea kabisa .

Kubwa zaidi katika matukio hayo kunaonekana kikiwa na watu pembeni wakishuhudia matukio hayo huku muhusika akipambana peke yake

Je ni sahihi mtu kuchukuliwa kwa nguvu hata kama itakuwa ni vyombo vya usalama ? Kama sio nini kifanyike kwa wanao shuhudia haya matukio?

Je tuwaombe hawa watu utambulisho kutoka kwa viongozi wa mitaa

Je tutumie umoja na nguvu kuzuia hilo jambo lisitokee

Je tuombee NIDA na vitambulisho vya wanaofanya zoezi hilo la ukamataji ?

Au ni sahihi tuache wahalifu wakamatwe ,tatizo tutajuaje wanaomchukua muhaligu ni wanausalama .​
Jambo hili ni Suala nyeti Sana lakini nashangaa kuona kwamba watu wanalijadili kwa mizaha.

Sheria za nchi zipo Wazi kabisa kuhusiana na Taratibu za kisheria zinazopaswa kufuatwa katika mchakato mzima wa kuwakamata au kuwatia mbaroni Watuhumiwa mbalimbali. Lakini Sheria hizo hizo hazijaeleza njia zinazopaswa kufuatwa katika Kuwateka watu kwa sababu Kitendo hicho moja kwa moja ni UHALIFU.

Tofautisheni Kati ya Ukamataji Wahalifu na Utekaji Watu (Arrest and Abductions). Kitendo chochote kile Cha kujaribu Kumkamata Mtu yoyote yule au Mtuhumiwa bila ya kufuata Taratibu za Kisheria zilizowekwa inahesabika kuwa ni UTEKAJI na wala siyo UKAMATAJI.

Utekaji daima ni Uhalifu, na daima huwa kunakuwa na Matumizi ya Nguvu, sasa basi, ili Mtu aweze kujihami na Vitendo vya Utekaji ni LAZIMA na yeye Mtekwaji anapaswa Kutumia Nguvu kinzani pia ili kujihami na Uhalifu mbaya kama huo. Tena nguvu kinzani ya ziada inapaswa kutumika na Mtekwaji au Watekwaji ili watu hao waweze kujihami au kujinisuru na vitendo vya Utekaji.

Nini hasa kinapaswa kufanyika ili kupambana na Vitendo hivi vya Utekaji Watu?
Sasa hili darasa pana zaidi na zito, kwa sababu hata Watekaji wenyewe huwa hawajifunzi mbinu za Utekaji Watu katika madarasa ya hadharani. Lakini kwa kuanzia, masuala haya machache tunaweza kuanza nayo:-

1. Education on Public Awareness about Abductions, Abductions Techniques and Counter-Abductions Techniques & strategies.

Kumbuka: Usalama wa Nchi au Usalama wako unaanzia na wewe mwenyewe binafsi.

2. Umilikishaji wa Silaha kwa Watu/Wananchi pamoja na Kuendesha Mafunzo stahili kwa ajili ya Matumizi sahihi kabisa ya hizo silaha zenyewe.

3. Kuweka Sheria Kali za Kuharamisha kabisa Matumizi yoyote yale ya njia za Utekaji Watu kwa Wasimamizi wa Sheria au kwa Vyombo vya Dola kwa kigezo cha eti Kutekeleza shughuli za Usimamizi wa Sheria au kulinda Usalama.

Uzoefu kutoka katika nchi nyingi sana hapa duniani unaonyesha kwamba Vitendo hivi vya Utekaji Watu hasa huwa Vinachochewa na Serikali katika michakato ya kushughulika na Watu fulani fulani katika Jamii, matokeo hasi ya michakato ya aina hiyo huwa inaishia kuibua uhalifu mbaya wa namna hii.
Tuweke Sheria zetu vizuri zaidi: Nobody should be above the law!
 
Ukisimamishwa na polisi tii, sheria,hili litasaidia polisi wetu kutotumia nguvu za ziada!
Ukisimamishwa na polisi tii, sheria,hili litasaidia polisi wetu kutotumia nguvu za ziada!
Mzee Kibao alitii Sheria bila Shuruti, lakini matokeo yake bado aliuawa kinyama Sana.

Worse enough, hata hao Polisi wenyewe nao pia ni miongoni mwa Watuhumiwa Wakuu kabisa ambao daima wamekuwa wakinyoshewa kidope kuhusika na Uhalifu huu mbaya.
 
Kwanza lazima tujiridhishe kuwa huyo anayekamatwa tuna mfahamu au tuna taarifa nae zozote,isijekuwa tunaingilia kazi ya polisi kukamata mtuhumiwa hatari anayetafutwa muda mrefu sana.

Pili, haina haja ya kugombana na askari ambao wapo kazini ila kuna umuhimu wa kufahamu taarifa za awali ambazo hazitazuia askari kufanya kazi yao, mfano kujua kwann mtuhumiwa anakataa kuwekwa chini ya ulinzi wa askari na je,wamemwambia kuhusu tuhuma zake.

Kwasasa tupo kwenye hali ya sintofahamu kama wanajamii kwasababu kuna matukio ya utekaji wa raia ambayo askari au jeshi la polisi wanahusishwa na wao kutonyoosha maelezo yao juu ya hizo taarifa.

Kama raia tunaowajibu na jukumu la kulindana na kuilinda jamii bila kwikwi yoyote lakini muhimu zaidi ni kuzihoji mamlaka na idara husika juu ya ukimya wao kwenye hizi tafrani zinazotukia na kuharibu utulivu na amani kwenye jamii.

Endapo kama Taratibu za ukamataji Watu watuhumiwa zingefuatwa, au endapo kama Wananchi wengi zaidi wangekuwa wanashirikishwa kikamilifu kwenye michakato ya utungaji wa Sheria za nchi, na endapo kama Sheria za Nchi zingemuweka kila Mtu kuwa yupo chini ya Sheria, basi matukio haya ya Utekaji Watu yasingeweza kushamiri Kama tunavyoona hivi Sasa hapa nchini Tanzania.

NB:
Utafiti uliofanyika hapa Tanzania unaonyesha kwamba, Matukio haya ya Utekaji Watu yameshamiri zaidi na kushika kasi kubwa sana mara tu baada ya Serikali kupitisha au Kufanyia Marekebisho ya Sheria ya Usalama wa Taifa Mwaka 2023, Marekebisho ambayo yamewapa Kinga ya kutoshitakiwa Mahakamani kwa Maafisa au Mawakala wa Idara ya Usalama wa Taifa katika Makosa mabaya ya kutenda Jinai, ikiwemo na kuua Watu.
It was a GRAVE MISTAKE!
Haya masuala ya Utekaji Watu ni miongoni mwa matunda mabaya Sana yatokanayo na Marekebisho hayo ya Sheria ya Usalama wa Taifa ya Mwaka 2023.
 
Dawa yao ni kuwazingira tu na kuwashushia kichapo! Au mhusika kujitetea kwa namna yoyote. No way out. Kuruhusu huu ujinga kuendelea kutamalaki, kunawafanya wananchi kuonekana kama kundi la nyumbu katikati ya simba wachache tu.
 
Kwanza lazima tujiridhishe kuwa huyo anayekamatwa tuna mfahamu au tuna taarifa nae zozote,isijekuwa tunaingilia kazi ya polisi kukamata mtuhumiwa hatari anayetafutwa muda mrefu sana.

Pili, haina haja ya kugombana na askari ambao wapo kazini ila kuna umuhimu wa kufahamu taarifa za awali ambazo hazitazuia askari kufanya kazi yao, mfano kujua kwann mtuhumiwa anakataa kuwekwa chini ya ulinzi wa askari na je,wamemwambia kuhusu tuhuma zake.

Kwasasa tupo kwenye hali ya sintofahamu kama wanajamii kwasababu kuna matukio ya utekaji wa raia ambayo askari au jeshi la polisi wanahusishwa na wao kutonyoosha maelezo yao juu ya hizo taarifa.

Kama raia tunaowajibu na jukumu la kulindana na kuilinda jamii bila kwikwi yoyote lakini muhimu zaidi ni kuzihoji mamlaka na idara husika juu ya ukimya wao kwenye hizi tafrani zinazotukia na kuharibu utulivu na amani kwenye jamii.
NAHISI UNA AKILI SANA..UBARIKIWE MURA
 
Unatekwa huku watu wanakurecord 🤣🤣nacheka lakini naogopa
 
Kwanza lazima tujiridhishe kuwa huyo anayekamatwa tuna mfahamu au tuna taarifa nae zozote,isijekuwa tunaingilia kazi ya polisi kukamata mtuhumiwa hatari anayetafutwa muda mrefu sana.

Pili, haina haja ya kugombana na askari ambao wapo kazini ila kuna umuhimu wa kufahamu taarifa za awali ambazo hazitazuia askari kufanya kazi yao, mfano kujua kwann mtuhumiwa anakataa kuwekwa chini ya ulinzi wa askari na je,wamemwambia kuhusu tuhuma zake.

Kwasasa tupo kwenye hali ya sintofahamu kama wanajamii kwasababu kuna matukio ya utekaji wa raia ambayo askari au jeshi la polisi wanahusishwa na wao kutonyoosha maelezo yao juu ya hizo taarifa.

Kama raia tunaowajibu na jukumu la kulindana na kuilinda jamii bila kwikwi yoyote lakini muhimu zaidi ni kuzihoji mamlaka na idara husika juu ya ukimya wao kwenye hizi tafrani zinazotukia na kuharibu utulivu na amani kwenye jamii.
Unajua process za kukamata wahalifu? Tatizo ni kuwa hao wakamataji wanakiunga taratibu. Hizo sheria ziliwekwa kwa sababu maalum i.e kuzuia watu wasio polisi kuteka watu kwa malengo maovu. Kosa ni la polisi kwa kuondoa uaminifu waliotakiwa kuwa nao. Tatizo litaondoka kwa kuwa serikali yenye kujali haki za raia wake.
 
Mimi nafikiri tuandike katiba mpya itakayomwezesha mwananchi kuingilia kati pale wanapoona vyombo vya Dola vikitumia nguvu kubwa dhidi ya raia kwa kigezo cha kuna askari jeshi au usalama wa taifa.
Hawa watu wanaonyesha kulewa madaraka!... Unamnyosheaje mwajiri wako bunduki anapokuja kuhoji juu tukio ambalo hajalielewa?
 
Bahati mbaya tabia hizi zikianza huwa haziondoki, ni mpaka pale wanaozifanya wapatwe na matokea mabaya sana yatakayowalazimisha kuziacha.
 
Ni kutoboa tires za magari ya watekaji Kisha hatua zingine ziendelee.
 
Back
Top Bottom