Uchaguzi 2020 Ni nini kimeitokea CHADEMA? Tumefikaje huku kupost picha za 2015?

Uchaguzi 2020 Ni nini kimeitokea CHADEMA? Tumefikaje huku kupost picha za 2015?

Countrywide

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2015
Posts
20,694
Reaction score
32,527
Habari wana JF, leo nipo kushangaa jambo ambalo sijui imekuwaje linatokea tena kwa viongozi wa chama. CHADEMA imefeli kwenye suala zima la habari kipindi hiki cha kampeni, imefeli sana.

Binafsi sikutegemea kama chama kingeweza kufika huku. Viongozi wetu wanaoongopewa na nani? Ili iweje? Lissu ana wafuasi wengi sana na hata baadhi ya maeneo kwenye kampeni zake watu wamejitokeza wengi, tatizo ni habari kufika kwa wakati kitu kinachopelekea viongozi kutuma habari ambazo sio sahihi kwa Umma.

Viongozi wanatuma picha za mwaka 2015 ili iweje? Mbona za mwaka huu zinaweza kutumika tu vipi zikihaririwa? Chama kifanye tathmini ya yanayoendelea ili kuzidisha imani kwa wafuasi wake.

Kuthibitisha nachosema, link hii hapa kuonyesha hizo picha ni za 2015
LOWASA AVUNJA REKODI SUMBAWANGA MJINI

.
IMG_20200902_165126.jpg
 
Sawa kabisa mkuu lakini na serikali ya wakati huu ya kimabavu inazuia kurushwa matangazo kwa vyama vingine tuondokane na watu hawa October.
Sisi hatuhitaji kuangalia tv, sisi tupo muda wote you tube, jf, twitter na IG
Huko kunatosha
Diamond alisusiwa nyimbo zake kuchezwa kwenye media, lakini akatusua IG, Youtube na mambo yakaenda
 
Back
Top Bottom