Habari wana JF, leo nipo kushangaa jambo ambalo sijui imekuwaje linatokea tena kwa viongozi wa chama. CHADEMA imefeli kwenye suala zima la habari kipindi hiki cha kampeni, imefeli sana.
Binafsi sikutegemea kama chama kingeweza kufika huku. Viongozi wetu wanaoongopewa na nani? Ili iweje? Lissu ana wafuasi wengi sana na hata baadhi ya maeneo kwenye kampeni zake watu wamejitokeza wengi, tatizo ni habari kufika kwa wakati kitu kinachopelekea viongozi kutuma habari ambazo sio sahihi kwa Umma.
Viongozi wanatuma picha za mwaka 2015 ili iweje? Mbona za mwaka huu zinaweza kutumika tu vipi zikihaririwa? Chama kifanye tathmini ya yanayoendelea ili kuzidisha imani kwa wafuasi wake.
Kuthibitisha nachosema, link hii hapa kuonyesha hizo picha ni za 2015
LOWASA AVUNJA REKODI SUMBAWANGA MJINI
.
View attachment 1556520