Ni nini sababu na suluhisho kwa wachagga kuwa na meno yenye rangi ya manjano/kahawia?

Ni kutokana na floride katika maji, sidhani kama unaweza kureverse hiyo kitu ila kama ni mtoto inabidi usinywe maji ya bomba, usitumie dawa za mswaki zenye flouride ya nyongeza.

Pia kuna filter za maji zinazoweza kuondoa floride kwenye maji.
 
Inaonekana ww ni raia wa Brazil mambo ya kaskazini huyajui yaani hadi Tanga wamejaa waoza meno??? Hapana mkuu waoza meno hata siku moja huwez kuwakuta ukanda wa pwani na ikitokea yupo bas ni vizazi vya moshi /arusha.Nenda tanga afu njoo uandike
Mkuu sio waoza meno ni wenye meno ya rangi. Kuna tofauti kati ya kuoza meno na kupata rangi za manjano.
 
Duu Wachaga tena..watani zangu kazi wanayo...sijawahi kuona inaisha wiki bila kuwa na post at least 3 zinazowahusu nyingi zikiwasema vibaya lakini ukweli mchungu ni kwamba ndio wameikamata nchi kupitia organ zote muhimu
Wanaowasema wachaga hapa n wivu tu unawasumbua.
Ukwel mchungu mtan.
 
Meno yenye rang yamedominate zaid Arusha tena n part ya arusha syo ukanda mzima.
N sehemu kubwa ya wachaga meno hayana rang
 
Tatizo lipo zaidi sehemu ya Arusha kuliko uchagani...na Arusha ni maeneo haswa ya Meru, na sababu ni maji yenye wingi wa Fluoride. Fanya utafiti vizuri ndugu.

Zipo njia za kuondoa hiyo fluoride ila sijui ni kwa kiasi gani wanazingatia.
 
Jamani, acha kuwapaisha hawa watu ivo, hebu mtukumbuke na Sie makabila machanga
 
hili jukwaa bila kutusema wachagga hamuoni raha, acheni kutafuta kiki za kijinga.
 
Usiseme vitu usivyovijua kiongozi. Ukisema kuanzia Tanga hadi Manyara unakuwa muongo, tena muongo mkubwa wewe.
Ni wakazi wa kuzunguka Ml. Kilimanjaro na Ml. Meru ndio wana meno yenye rangi. Siku nyingine jifunze ndio uongee.

Mkoa wa Simiyu ni karibu 80 percent
 
Mimi wachaga nina tatizo nao kwenye mambo ya CHADEMA tu. Hizi issue nyingine za meno,biashara,wizi na mademu wao hazinihusu.
 
Tatizo ni maji sio uchafu. Katika maisha yangu nimeona hili tatizo katika mikoa ya Manyara, singida, Arusha na Kilimanjaro. Ila siku hizi kuna utaalam wa kusafisha yawe meupe. Kuna baadhi ya hospitali za meno wanafanya hii kazi lakini ni gharama kidogo na sio watu wengi wanaweza kulipia huduma hii.
 
Kiukweli mimi nimeishi moshi tangu utotoni mpaka kuwa mkubwa kwa watu walituzunguka walikua na meno meupee na maji ya moshi ni matamu asee asikuambie mtu nimetembea mikoa mingine sijaona maji mazuri kama ya moshi
Huyu mleta mada unashindwa kutofautisha na watu wa arusha ambao maji yao kama magadi hivi
 
Acha uongo...nimeishi Kibosho na Huru watu wana meno ya manjano haswa hata wameru,mbona wamasai wana meno meupe pee?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…