Ni pombe gani hutakuja kuisahau maishani mwako?

Ni pombe gani hutakuja kuisahau maishani mwako?

Aise sitamsasahau Smirnoff black ice alichonifanya japo ni tamu kama sprite hadi ilifika kipindi nikiiona mwili unasisimka, japo viroba vya Zed viliwahi nilaza bafuni siku moja kabla ya kuingia pepa ya la saba.
Std 7 ulikua ushaanza kupiga masanga mkuu? Nomaa😀
 
Sitaisahau tyson kiroba kimoja tu ila kilivyonipeleka nilihisi kama nakata moto kitanda kilikuwa kinazunguka balaa.
 
Aise sitamsasahau Smirnoff black ice alichonifanya japo ni tamu kama sprite hadi ilifika kipindi nikiiona mwili unasisimka, japo viroba vya Zed viliwahi nilaza bafuni siku moja kabla ya kuingia pepa ya la saba.
Std 7 ulikua ushaanza kupiga masanga mkuu? Nomaa😀
 
Basi itakua umeanza karibuni kutumia! Wazoefu lazima kuwe na visa vya hapa na Pale[emoji3] mara mtu kalala nje na funguo za mlango kashika mkononi dah[emoji3][emoji3]
...


Uje basi nikufundishe kunywa, na wew ili tupate kisa/visa.
 
Kuna kipindi nilikuwa napenda kunywa amarula occasionally na hasa nikipata ofa[emoji2957]
Nakumbuka best angu alikuwa na birthday hivyo nikajikoki nikanunua ile kubwa. Tumekula vizuri tukaanza kunywa...mara best akaniambia hii kitu haijachangamka tuchanganye na k vant...yeye ni mtu wa pombe tofauti na mimi...bwana bwana si nikakubali nikawa naweka kidogo kidogo.

Chupa ilivyokaribia kuisha nikashangaa ulimi unakuwa mzito mdomoni[emoji2]Story haziendi tena ikabidi tuite tax. Hatukufika mbali kichefuchefu hiki hapa, mikono mizito sikuweza hata kufungua kioo nikatapikia ndani kwenye miguu...yani nililegea hatari. Dereva akamind akataka tumlipe na ya kuosha gari[emoji2]

Kufika home naona nyota tu nikaingia chooni kwa kutambaa....nilifanikiwa kuvua suruali tu[emoji85]
Tangu siku hiyo mapenzi na amarula yakaisha...nimekuja kuionja mwaka jana baada ya kama miaka 4 hivi ila niliinywa kwa tabu sana so nimeachana nayo.
Ulikosea sana kuchanganya kvant na amarula... hizi ni pombe za aina mbili tofauti sana
 
Nilikunywa konyagi kubwa na kadogo nusu alafu dry nilizima aisee,simu nikaacha kwenye taxi niliumwa siku mbili sili sinywi from that day sijawahi na sitawahi kunywa konyagi hata ndugu zake siwataki[emoji1787]
Nguvu ya kumaliza hyo ya kwanza uliitoa wap mpaka ukaongeza?
 
nimewahi ghafilika sana hapo kitambo kwaajili ya pombe zangu

1: Nilialikwa na wanangu flani wapo mbele kitambo kufika nikapokelewa na kinywaji aina flami ya beer inaitwa Redhorse
nikaanza vyombo vipya rasmi bila kujua ni bia moja kali 8 percent alc. vol.
Nilikomaa zikafika 7 nikakata moto na nikalala siku tatu sijiwezi

2:Nimerudi home nakuta kuna kinywaji kipya dogo akaniambia kinaitwa K-Vant basi nikasema tupewe hiyo jichupa le kubwa lile likaisha 3 men
likaletwa lingine hapo nilikula lakini pass ndefu sana nilirudisha chenji nikasema maini itatoka nililala kwa tabu sana lakini niliwahi kuponea kwasababu ya Valeur kitambo kidogo na hii ingenitoa kama siyo hospital

3:Hii nilikuwa na mkuu moja tulikuwa ukweni kwake kabla ya kufika akaona ni vyema turashie kidogo KIBO GOld(maisha ktk mwanga bora)
kufika ukweni akapokelewa kwa shangwe na mama mkwe wake akaleta hizo hizo hizo.
Baadae baba mkwe alirudi kutoka mishe zake akachafua meza nae basi cha aibu nilirudisha chenji ukweni kwa jamaa
mama mkwe akaniambia pole nikaona aibu zaidi kwanzia hapo nikatia adabu na pombe siyo chai wakuu
Namba 1 hii chombo redhorse wananchi wa HongKong au Guangzhou wanajua matatizo yake kama sio mnywaji.Hii kitu weka mbali na watoto
 
Back
Top Bottom