Ni rahisi sana kupata kiongozi mwenye kichaa kupitia demokrasia, si njia nzuri ya kupata viongozi

Ni rahisi sana kupata kiongozi mwenye kichaa kupitia demokrasia, si njia nzuri ya kupata viongozi

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Kuna matatizo fulani ya akili humfanya mtu atamani kuwa kiongozi au kujiona yeye ndiye anafaa sana kuongoza. Tukianza na watu wenye kichaa (Schizophrenia) yenyewe. Dalili moja inayoweza fanya watu hawa waweze kupenda kuwa viongozi ni 'delusion of grandeur'.

Hii ni ile hali ya mtu kujihisi anauwezo kupita kiasi, au kwamba ni mkuu sana. Ni dalili moja ya watu wenye kichaa. Sasa dalili kama hii inaweza kumfanya mtu huyu awe na muelekeo wa kutaka uongozi. Na nafasi yake(sababu ya kichaa chake) ya kuwa kiongozi ni kubwa kuliko mtu wa kawaida.

Hypomania: Hypomania nayo ni aina ya kichaa. Watu wenye hypomania huwa waongeaji sana, waongeaji kupitiliza. Hili nalo, kwa kupitia demokrasia linaweza mfanya mtu astahili zaidi kuwa kiongozi.

Narcissism: Mtu mwenye 'narcissism' huwa anajiona wa pekee sana. Anaona hakuna kama yeye. Tatizo hili linaweza mfanya mtu atake na awe kiongozi kupitia demokrasia.

Antisocial/sociapathy: Watu wa hivi husemwa kuwa hawajali haki za wengine, huwa walaghai na huwa na kitu wanaita 'superficial charm', yaani anajitia kupendezwa nawe kinafiki tu au ni mtu wa watu kiuongouongo tu. Nafikiri wanasiasa wengi wanaofanikiwa kwenye mfumo wa demokrasia wanaangukia hapa.

Demokrasia na michakato yake ni mfumo wa hovyo sana. Tunatakiwa kupata mfumo mpya. Mfumo ambao kuna nafasi kubwa za kuwa na viongozi vichaa, haufai kabisa.
 
Kweli tupu. Pia kuna chama kwa nafasi yake kinapinga midaharo ambayo inatoa fursa ya sisi raia kuwahoji au kuwapima vichaa wao waliowateua kuwa marais. Kikifika kipindi cha uchaguzi,njia mojawapo kuwagundua vichaa na sarakasi zao ni kupitisha midaharo kama 3 katika sekta 3 tofauti, hapo turuhusu maswali ya chap, yanayoitaji IQ kuyajibu;. Vichaa watajulikana tu
 
Back
Top Bottom