Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 98,439
- 145,410
Majuzi hapa Rais Magufuli alinukuliwa akiwaasa watu waukatae ubaguzi.
Lakini kwa baadhi ya kauli zake, watu wanaweza kusema aanze yeye kwanza kuufanyia kazi huo ushauri wake maana mara kadhaa keshawahi kutoa kauli ambazo zilionekana kuwa ni za kibaguzi.
Karibu miaka 3 ilopita, niliwahi kumsema kuhusu hizo kauli zake.
www.jamiiforums.com
[Kwa wale ambao huwa mnadai sijawahi hata mara moja kumpinga au kumsema Magufuli kwa sababu eti ni Msukuma mwenzangu, take that!].
Kwenye hizi kampeni za mwaka huu, Rais Magufuli katoa baadhi ya kauli ambazo kwa kweli hazikuwa sawa.
Wiki chache zilizopita alisikika akisema kwamba hatopeleka maendeleo kwenye sehemu ambazo watachagua mbunge au wabunge wasio wa chama chake.
Nilijiuliza mengi sana, yakiwemo haya;
Hivi, huyu Rais anatambua kwamba ni Rais wa Tanzania nzima na Watanzania wake, licha ya vyama wavipendavyo au ni Rais wa baadhi tu ya Watanzania na baadhi tu ya sehemu za Tanzania?
Hayo maendeleo anayosema hatoyapeleka huko ambako hawatochagua wabunge wa CCM, hao waishio huko hawalipi kodi?
Hela za kodi, ambazo ndo hutumika kuleta maendeleo, hutoka kwa Watanzania wa kada zote.
Iweje sasa yeye aseme kuwa hatopeleka maendeleo kwenye sehemu zenye wabunge tofauti?
Inastaajabisha sana na inaleta maswali fikirishi.
Huenda huyu Rais wetu hajui kuwa hata huo mshahara wake ni Watanzania wa kada zote ndo walimpao.
Pia, natumai hadhani kuwa hizo hela za kodi zetu ni zake binafsi.
La, huwezi kusema eti utawanyima watu maendeleo wakati hela si zako na ni za kwao.
Yeye ni nani hadi aseme hatopeleka maendeleo sehemu mpaka watu wawachague CCM?
Kauli za kushangaza sana......

Bomoabomoa Mwanza: Rais Magufuli omba radhi kama....
Kauli uliyoitoa mapema leo huko Mwanza ya kwamba watu wa huko 'wasibomoleshwe' nyumba zao kwa sababu wao ndo walokupa urais si nzuri hata kidogo. Ni kauli ya kibaguzi kabisa na ambayo inapaswa kupingwa na mtu yeyote yule mwenye akili timamu. Wewe unatoa kauli kama hiyo huko Mwanza huku kukiwa...