Ni Rais wa Watanzania wote au ni Rais wa waliompigia kura tu?

Ni Rais wa Watanzania wote au ni Rais wa waliompigia kura tu?

Majuzi hapa Rais Magufuli alinukuliwa akiwaasa watu waukatae ubaguzi.

Lakini kwa baadhi ya kauli zake, watu wanaweza kusema aanze yeye kwanza kuufanyia kazi huo ushauri wake maana mara kadhaa keshawahi kutoa kauli ambazo zilionekana kuwa ni za kibaguzi.

Karibu miaka 3 ilopita, niliwahi kumsema kuhusu hizo kauli zake.


[Kwa wale ambao huwa mnadai sijawahi hata mara moja kumpinga au kumsema Magufuli kwa sababu eti ni Msukuma mwenzangu, take that!].

Kwenye hizi kampeni za mwaka huu, Rais Magufuli katoa baadhi ya kauli ambazo kwa kweli hazikuwa sawa.

Wiki chache zilizopita alisikika akisema kwamba hatopeleka maendeleo kwenye sehemu ambazo watachagua mbunge au wabunge wasio wa chama chake.

Nilijiuliza mengi sana, yakiwemo haya;

Hivi, huyu Rais anatambua kwamba ni Rais wa Tanzania nzima na Watanzania wake, licha ya vyama wavipendavyo au ni Rais wa baadhi tu ya Watanzania na baadhi tu ya sehemu za Tanzania?

Hayo maendeleo anayosema hatoyapeleka huko ambako hawatochagua wabunge wa CCM, hao waishio huko hawalipi kodi?

Hela za kodi, ambazo ndo hutumika kuleta maendeleo, hutoka kwa Watanzania wa kada zote.

Iweje sasa yeye aseme kuwa hatopeleka maendeleo kwenye sehemu zenye wabunge tofauti?

Inastaajabisha sana na inaleta maswali fikirishi.

Huenda huyu Rais wetu hajui kuwa hata huo mshahara wake ni Watanzania wa kada zote ndo walimpao.

Pia, natumai hadhani kuwa hizo hela za kodi zetu ni zake binafsi.

La, huwezi kusema eti utawanyima watu maendeleo wakati hela si zako na ni za kwao.

Yeye ni nani hadi aseme hatopeleka maendeleo sehemu mpaka watu wawachague CCM?

Kauli za kushangaza sana......
Mkuu,pamoja na mambo haya ya kushangaza sana, lakini la kushangaza zaidi, bado wewe huwa unamsapoti huyu kichaa.
 
Only corpses will vote for ccm.
Kamanda wako anatiketi ya kurudi Brussels tarehe 18 December vipi wewe utaenda naye?

October 28th kura zote za ndio ni kwa JPM.

JPM ANATOSHA
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
 
Kamanda wako anatiketi ya kurudi Brussels tarehe 18 December vipi wewe utaenda naye?

October 28th kura zote za ndio ni kwa JPM.

JPM ANATOSHA
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
Wherever but I can't vote for thieves and murderous
 
Wherever but I can't vote for thieves and murderous
Simple advice you can take it or not" IF YOU CAN'T FIGHT THEM,JOIN THEM"

October 28th ni USHINDI WA KISHINDO KWA JPM

JPM ANATOSHA
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
 
Simple advice you can take it or not" IF YOU CAN'T FIGHT THEM,JOIN THEM"

October 28th ni USHINDI WA KISHINDO KWA JPM

JPM ANATOSHA
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
Not only my vote but I will shed my blood 28/10 I will confirme what I write ..
 
We si unamsaporti shetani Sasa kina Cha Lissu kimekuwa kirefu umeanza kugeuka?

Mwaka huu tutaelewana tu hakuna kulemba mpaka kieleweke...

Kura zitalindwa kwa namna yeyote ile mpaka Lissu atangazwe

Yaani Ni hivi tarehe 28 tupo kituoni saa 11 asubuhi bila kuona wakala wa chadema akiingia pale ndani hakuna shughuli ya kura itaendelea pale.

Watu tumehamua kufanya mabadiliko na mabadiliko yana ghalama zake..
UMEHAMUA SIO?
 
Rais muda mwingine hutumia utani na hapo ndipo watanzania tunapotosha maana na kusema kuwa Rais anaubaguzi
Kuna muda inabidi tuchuje katika hali ya ukweli na uhalisia
Tusichukulie utani kuwa subjects ......Wasukuma ni watu wa utani na hilo linajulikana
ni watu gani wanaongea bila kuwa na utani hata kidogo?
Utani wakati yeye mwenyeww ameshawaambia watu wa majimbo fulani kwamba hakupeleka maendeleo kwa sababu hizo na hatapeleka kama hawatachagua atakavyo!! Wewe vipi wewe!!!
 
Kwa hiyo JPM sio rais wa watz wote?

Kusema tu flani ni Raisi wa Watanzania wote inafaa hiyo kauli iendane na Matendo ,mna msifia Rais kuwa ni mkweli akiahidi ana timiza ahadi zake.

Swali ni kwa nini atoe Kauli za kibaguzi dhidi ya Wananchi wake na kinyume kabisa na Katiba!?.Hebu tizama Haki na Wajibu katika Katiba yetu.👇👇



17
(4) Ni marufuku kwa mtu yeyote kubaguliwa na mtu au
mamlaka yoyote inayotekeleza madaraka yake chini ya sheria
yoyote au katika utekelezaji wa kazi au shughuli yoyote ya
Mamlaka ya Nchi.
(5) Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa masharti ya ibara hii
neno "kubagua" maana yake ni kutimiza haja, haki au mahitaji
mengineyo kwa watu mbalimbali kwa kuzingatia utaifa wao,
kabila, pahala walipotokea, maoni yao ya kisiasa, rangi, dini,
jinsia au hali yao ya maisha kwa namna ambayo watu wa aina
fulani wanafanywa au kuhesabiwa kuwa dhaifu au duni na
kuwekewa vikwazo au masharti ya vipingamizi ambapo watu wa
aina nyingine wanatendewa tofauti au wanapewa fursa au faida
iliyoko nje ya masharti au sifa za lazima, isipokuwa kwamba neno
"kubagua" halitafafanuliwa kwa namna ambayo itaizuia Serikali
kuchukua hatua za makusudi zenye lengo la kurekebisha
matatizo katika jamii.
(6) Kwa madhumuni ya kuhakikisha usawa mbele ya sheria,
Mamlaka ya Nchi itaweka taratibu zinazofaa au zinazozingatia
misingi kwamba -
(a) wakati haki na wajibu wa mtu yeyote vinahitaji
kufanyiwa uamuzi wa mahakama au chombo
kinginecho kinachohusika, basi mtu huyo atakuwa na
haki ya kupewa fursa ya kusikilizwa kwa ukamilifu, na
pia haki ya kukata rufaa au kupata nafuu nyingine ya
kisheria kutokana na maamuzi ya mahakama au
chombo hicho kingenecho kinachohusika;
(b) ni marufuku kwa mtu aliyeshtakiwa kwa kosa la jinai
kutendewa kama mtu mwenye kosa hilo mpaka
itakapothibitika kuwa anayo hatia ya kutenda kosa
hilo;
(c) ni marufuku kwa mtu kuadhibiwa kwa sababu ya
kitendo chohote ambacho alipokitenda hakikuwa ni
kosa chini ya sheria, na pia kwamba ni marufuku kwa
adhabu kutolewa ambayo ni kubwa kuliko adhabu
iliyokuwapo wakati kosa linalohusika lilipotendwa;
(d) kwa ajili ya kuhifadhi haki ya usawa wa binadamu,
heshima ya mtu itatunzwa katika shughuli zote
zinazohusu upelelezi na uendeshaji wa mambo ya
jinai na katika shughuli nyinginezo ambazo mtu
anakuwa chini ya ulinzi bila uhuru, au katika
kuhakikisha utekelezaji wa adhabu;
(e) ni marufuku kwa mtu kuteswa, kuadhibiwa kinyama
au kupewa adhabu zinazomtweza au kumdhalilisha."
[/]
 
Sifikirii kama Magufuli anaweza kusema eti sipeleki maendeleo pale kisa sikupigiwa kura!

Hizo ni kampeni tu.
Kwamba anatoa kauli za kibaguzi ili kupata kura ila akiwa Rais hawezi kufanya ubaguzi!!Halafu hapo hapo anasema watanzania tusikubali ubaguzi na tukatae wanaotoa kauli za kibaguzi!
Halafu mbona kule Bunda alisema kwa miaka mitano hakujenga barabara kwasababu walichagua mpinzani na wakirudia hatajenga?

Mnatuchanganya mjue!!!!
 
Back
Top Bottom