Ni Rais wa Watanzania wote au ni Rais wa waliompigia kura tu?

Kwa asili Magufuli hana kipaji cha kuhutubia (public speaking)! Ukimsikiliza hawezi kukupa matumaini.

Ila kile anachokikosa katika kujenga hoja za kihotuba anakijalijizia katika utendaji mahiri (getting things done!).

Tupilia mbali mtu mwenye maneno matamu ya kisiasa but he is crap linapokuja suala la utendaji.

Cha ziada zaidi alichonacho Magufuli, kwa mara ya pili tuna Rais mtaifa, mzalendo kweli kweli.

Tupilia mbali wanasiasa ambao hawawezi kuizungumza Tanzania bila kuitaja dunia -- eti Tanzania inaihitaji dunia kuliko dunia inavyoihitaji Tanzania. Holy Crap!
 
Sifikirii kama Magufuli anaweza kusema eti sipeleki maendeleo pale kisa sikupigiwa kura!

Hizo ni kampeni tu.
Endelea kuweka pamba masikioni, jitoe ufahamu halafu ukitulia, jitafakari.

Kauli iliyorudiwa zaidi ya mara 1000 ni hiyo. Mimi nilitegemea kauli bora kabisa yenye hadhi ya cheo na mamlaka yake ingekuwa, " Ndugu zangu, chagueni wabunge na madiwani ambao ni wachapa kazi. Msibague ni wa chama gani, pimeni uwezo wao wa kuwatumikia kwa sababu maendeleo hayana chama! ".

Hii nileteeni fulani, ooh sina connection nao , inashangaza sana kwa sababu hao wote ni watanzania na wapo nchini, wanaongozwa na mamlaka za nchi hii. Mbona kwenye masuala mengine wanashughulikiwa na taasisi husika chini ya mamlaka hiyo hiyo? Hapo connection huwa inatoka wapi!
 
Sifikirii kama Magufuli anaweza kusema eti sipeleki maendeleo pale kisa sikupigiwa kura!

Hizo ni kampeni tu.
Mkuu tusiwe wepesi kisahau, Magufuli huwabaguwa wapinzani wazi wazi hata akiwa kwenye ziara za kiserekali. Wapinzani nao baada ya kubaini hayo wakaanza kumkacha na kutohudhuria ziara zake.
 
Kwa asili Magufuli hana kipaji cha kuhutubia (public speaking)! Ukimsikiliza hawezi kukupa matumaini.

Ila kile anachokikosa katika kujenga hoja za kihotuba anakijalijizia katika utendaji mahiri (getting things done!)...
Angetekeleza anayo yatekeleza bila kututeka, kutupoteza, kututungia sheria kandamizi na nyanyasaji, kura yangu ningempa. Lkn sasa, yaya geete.
 
Afu kunawatu wanamsikiliza aisee mm Sina huo muda kwakweli Bora niangalie Tin white nijua naangalia comedy kuliko kuangalia hutuba za mtu unayehisi anaheshima kumbe utopolo tu.

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Sikutegemea umpe makavu live magufuli hasa kipindi hiki
 
Sikutegemea umpe makavu live magufuli hasa kipindi hiki
Hiyo ni kwa sababu ya prejudice uliyonayo kwangu na kwa wengine.

Laiti ungekuwa hujaathirika na hizo preconceived notions ulizonazo, wala usingesema kuwa ‘hukutegemea’, kwa sababu, nimeshamsema na kumpinga mara nyingi tu humu huyo Rais Magufuli.

Na huo ni UKWELI ambao huwezi kuupinga.

Na wembe ni ule ule. Akikosea nitamsema na akipatia nitampongeza.

Na Wembe wangu huu unakata kotekote, hata kwa Lisu unakata tu.
 
Hiki ni kipindi cha uchaguzi na wewe unajulikana humu. Hii ni wiki ya lala salama na haikutegemewa hadi wewe umchoke huyu mtu na kuandika haya kipindi hichi. Sijakataa kama hujawai mponda na tabia zake za ovyo. Ila kwa kufanya kipindi hiki nimeona kweli magufuli amechokwa
 

Rais wa hovyo
 
Naweza ‘kujulikana’ lakini hakuna anayenijua.

Kwa sababu kama kweli kuna anayenijua, basi hatoshangazwa na nilichokiandika.

Na kwa taarifa yako tu, kwa vile tu nimempinga na hizo kauli zake, hiyo haina maana kuwa nimemchoka.

Nakushauri uache kufikia mahitimisho juu ya mambo ambayo huna uhakika nayo au ambayo huyajui.
 
Unajua impact ya andiko lako hiki kwake hasa kwenye hizi siku za lala salama??? Au ulikuwa high wakati unaandika???

Magufuli Must go!!
 
Unajua impact ya andiko lako hiki kwake hasa kwenye hizi siku za lala salama??? Au ulikuwa high wakati unaandika???

Magufuli Must go!!
I don’t care about impact.

I don’t think I’m that impactful, anyway.

And I’m not a paid surrogate, either.

I just I call things as I see them.
 
Ubaguzi upo umejikita ndani zaidi kwenye DNA ya Magufuli, hata a pretend vipi hawezi kuficha tabia zake za kibaguzi.
 
Sifikirii kama Magufuli anaweza kusema eti sipeleki maendeleo pale kisa sikupigiwa kura!

Hizo ni kampeni tu.
Akili za kamassy ndio hizi eti hufikiri Kama anaweza kusema??? Kwahiyo aliyoyasema lilikuwa doli lake sio yeye?? Utahira utawaisha lini nyie vipozeo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…