Ni route ipi rahisi kutoka Mwanza kwenda Ruvuma?

Panda basi za Mwanza-Iringa(isamilo or whatever) ulale Iringa upunguze safari,then kesho yake unaamka saa 3 asubuhi,saa 4 unapanda super feo and the like of zinazotoka Dodoma kwenda Ruvuma imeisha hiyo..ukilala Dodoma utachoka sana na hautopata muda wa kupumzika vya kutosha..
Route nzur iyo at gharam zip chin MZA-iringa 35k ataingia kule kama sa4 iv night kesh yake mapem tu sa 12 on the way to Songea(20k) anafik sa7 tu
 
Pale noma niliwahi kufika saa 9 usiku nikitokea Dar,,,safari ilikua naenda Songea ilibidi nichukue gesti kwa baridi kali.

Kufika room aisee kila kitu cha baridi hadi kitanda mpaka blangeti la kulalia ,nikavua viatu ili nilale nikashindwa mwishowe nikalala na viatu mpaka asubuhi hii ndo ilikua mara yangu ya kwanza kulala na viatu nikiwa najitambua kwenye kitanda.Asubuhi jua lilitoka saa 5.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] miaka hio nilikua natoka zangu mbinga mchana usiku na lala makambako,kesho yake nasepa moro.
ila hapo makambako kuna baridi sana ila asijari atapata maji ya moto
 
Kwema wakuu,

Nina safari ya kutoka mwanza kwenda Ruvuma, Ombi langu kwenu ni root ipi nikipitia itakuwa rahisi kwangu kufika uko?

Pia ni mabasi yapi mazuri nitumie ili nipunguze gharama, maana vyuma vimekaza.

Shukrani!
Mwanza hadi Moro, unalala kisha kisha asubuhi panda newforce au superfeo ya songea, Kama zipo gari za mwanza iringa, mwanza njombe ni nzuri zaidi, mwanza Mbeya kisha unashuka makambako unalala kisha alfajiri unaanza safari ya songea mapema saa4 uko songea kama unaenda mbinga, nyasa, tunduru, na etc au ukitaka kuenjoy tulia kidogo ule kuku maeneo ya deluxe na mauno ni wewe tu, kila kitu kipo
 
Ukitokea makambako huwezi kufika songea saa 4 hapo atafika saa 7 kwani gari zile kwa kua root ni fupi njiani wala hawana haraka.
Mwanza hadi Moro, unalala kisha kisha asubuhi panda newforce au superfeo ya songea, Kama zipo gari za mwanza iringa, mwanza njombe ni nzuri zaidi, mwanza Mbeya kisha unashuka makambako unalala kisha alfajiri unaanza safari ya songea mapema saa4 uko songea kama unaenda mbinga, nyasa, tunduru, na etc au ukitaka kuenjoy tulia kidogo ule kuku maeneo ya deluxe na mauno ni wewe tu, kila kitu kipo
 
Kwema wakuu,

Nina safari ya kutoka mwanza kwenda Ruvuma, Ombi langu kwenu ni root ipi nikipitia itakuwa rahisi kwangu kufika uko?

Pia ni mabasi yapi mazuri nitumie ili nipunguze gharama, maana vyuma vimekaza.

Shukrani!
Panda basi mwanza to mbeya,kupitia mtera,shuka makambako ambako utapanda mabasi ya kwenda ruvuma
 
Pale noma niliwahi kufika saa 9 usiku nikitokea Dar,,,safari ilikua naenda Songea ilibidi nichukue gesti kwa baridi kali.

Kufika room aisee kila kitu cha baridi hadi kitanda mpaka blangeti la kulalia ,nikavua viatu ili nilale nikashindwa mwishowe nikalala na viatu mpaka asubuhi hii ndo ilikua mara yangu ya kwanza kulala na viatu nikiwa najitambua kwenye kitanda.Asubuhi jua lilitoka saa 5.
😂😂😂😂😂
 
Option ya nne panda bus mpaka dar then chukua meli inaitwa mv mdee unafika siku hiyohiyo na abiria mnakuwa 19 tu.
 
Kwani yale mapangaboi ya Jiwe hakuna route ya Mwanza to Ruvuma?
Route za bombadier ziko tele daily. Unapaa kutoka Mwanza kupitia Dar hadi Songea. Ndani ya masaa 5 utakuwa Songea na gharama yake haizidi laki mbili! Ukijumulisha hiyo gharama ya mabasi ya kuungaunga ukijumulisha na gharama za malazi na chakula njiani pamoja na usumbufu utagundua kuwa usafiri wa pangaboi ni cheaper.
 
Dr
Songea bombardier Imeanza kwenda lini? Nakumbuka walijaribu pale mwanzo halafu wakasitisha huduma nadhan baada ya kuona wanapata hasara , Ruvuma bado haijachangamka . Lakini pia umenishangaza kwenye quotation za nauli, hiyo route Kama kweli imeanza haiwezi kuwa laki mbili , labda kuanzia laki tano huko as hizo ni safari mbili tofauti kabisa , Kama ilivyo mbeya to mwanza kwa sasa
 
Route za bombadier ziko tele daily. Unapaa kutoka Mwanza kupitia Dar hadi Songea. Ndani ya masaa 5 utakuwa Songea na gharama yake haizidi laki mbili! Ukijumulisha hiyo gharama ya mabasi ya kuungaunga ukijumulisha na gharama za malazi na chakula njiani pamoja na usumbufu utagundua kuwa usafiri wa pangaboi ni cheaper.
[emoji848]! Mkuu lini umetumia hiyo njia uliyoielezea?
 
Atachoka sana atafika iringa saa nne au zaidi mpaka apate sehemu ya kulala inaweza kuwa saa sita wakati Dom wana fika saa 12 wanapumzika na kesho 12 wapo songea
Kwa nini asiende mpaka Iringa? Kuna mabasi ya MZA - Iringa siku hizi!
 
Au kavipi aKamate usafiri wa asili vuuuuuu kufumba na kufumbua songi hii hapa[emoji23][emoji23][emoji23]
au mnasemaje?
 
[emoji848]! Mkuu lini umetumia hiyo njia uliyoielezea?
Check na ofisi ya ATCL iliyopo mtaa wa Kenyatta Road hapo Mwanza, watakuelekeza namna utakavyo connect na route yao ya kanda ya kusini mara utakapotua JNIA hapo Dar.
 
Back
Top Bottom