Ni sababu zipi za msingi zilizosababisha Wakuu wa Wilaya wengi kiasi hiki kuhamishwa vituo vyao vya kazi?

Ni sababu zipi za msingi zilizosababisha Wakuu wa Wilaya wengi kiasi hiki kuhamishwa vituo vyao vya kazi?

Mtumish kuhamishw kituo cha kaz ni jambo la kawaid ambalo husaidia ufanis wa kaz kwa mtumishi


Au wew ni yule mwanakondoo wa mchungaji kmaro
Nadhani hili ndio jibu sahihi. Zingine porojo tu
 
Kama hujui skuhizi kunamtindo wa kupiga hela ndefu kupitia hamisha hamisha ya watumishi...
Mkuu wa wilaya umhamishe lazma umpige milioni kadhaa kutegemeana na umbali hapo bado ma-Ded, ma-afsa utumishi nk.
Hii nimoja ya njia tulivu yakupiga mafungu ya serikali!! Kapigie ka-'mwejero' kaulize kamekula ngapi na bosi zake ngapi? ndoutajua hujui...
 
Kwani gharama za uhamisho ni kiasi gani na gharama ya kumuweka Mkuu wa Wilaya mpya na kumuweka pembeni wa zamani ni kiasi gani. Pia kwa waliohamishwa, Je. Uwepo wao mahali pale ulikuwa unafaidisha Wilaya fedha kiasi gani au ulikuwa uitia Wilaya kiasi gani? Tarakimu za hela ya gharama hizi zituongoze kwenye kujadili maamuzi yaliyofanywa na serikali. Nawaza!!
 
Mtumish kuhamishw kituo cha kaz ni jambo la kawaid ambalo husaidia ufanis wa kaz kwa mtumishi


Au wew ni yule mwanakondoo wa mchungaji kmaro
Itakuwa ni kijana wa kinana.
 
Hivi kama mamlaka ya uteuzi limegundua kuwa hao wakuu wa wilaya walifanya "madudu" kwenye vituo vyao vya awali, ni kwanini wasipigwe chini na kuachishwa kazi badala ya kuwahamisha vituo vyao vya kazi, ambapo mzigo wa kuwalipia hiyo inayoitwa "transfer allowance" tunaibeba sisi walipa Kodi wa nchi hii?
Haya maswali ameulizwa mwenye mamlaka ya utezi wa wakuu wa wilaya ila maoni yangu "kuna wakuu wa wilaya wameondolewa na hawa lazima nafasi zao zijazwe. Wakati wa kuzijaza ni ama uteue wapya au uhamishe wengine kujaza nafazi zilizowazi kwa kuhamisha wengine wanaofaa kulingana na maoni ya anayeteua. Mfano ni yule DC wa Arusha aliyefanya vizuri maeneo yote aliyopelekwa na sasa kahamishiwa Tabora akaweke mambo sawa. Haya ni maoni yangu na yale maswala uliyouliza Kwa mamlaka ya uteuzi NATARAJIA mamlaka hiyo ITAKUJA KUYAJIBU."
 
Lkn kuwapiga chini na kuwa na wastaafu wengi kiasi hicho wanaolipwa hela nyingi ingegharimu hela nyingi zaidi
Basi wangeachwa mahali walipo ili kuepuka gharama za kuwahamisha !!
 
Mkuu wa Wilaya ndo jicho la Raisi kwenye Eneo husika. Ukiona sehemu kuna uhalifu na hakuna hatua zinazochukuliwa basi juwa DC huyo satoshi.
Sasa hatua za kuchukuliwa zinaweza kutofautiana kutokana na extent ya udhaifu. Wengine huishia kutenguliwa na wengine kuhamishwa kituo.
Kilichotokea kwa sasa..wengi wameondoka kwa kushindwa kusimamia fedha za miradi ikiwemo ujenzi wa madrasa.
Tutegemee mshtuko mwengine zaidi kwa ma DED sasa. Bi Mkubwa hakopeshi..ukishindwa ku deliver bas kichwa chako ni dalali yake...no kufokafoka lakini vitendo zaidi
Tusubiri tuone no kufoka foka kama italeta matunda mazuri !! Tunasubiri !
 
Kuweka kumbukumbu sawa kwa wanachotupiga mpaka kufikia kiwango alichoweka mkuu hapa, ni hivi, Posho za uhamisho ni posho ya usumbufu (disturbance allowance) na posho ya kujikimu (subsistence allowance) na posho ya safari (on transit) ikiwa safari inachukua zaidi ya masaa 6 njiani.

Posho ya kujikimu analipwa mtumishi anayehama pamoja na mwenza wake kiwango cha per diem ya siku 1 kwa siku 14, na watoto 4 (kama anao) hulipwa nusu ya perdiem kwa siku hizo 14. Kwa wilayani Per Diem ni Tsh. 200,000/= kwa siku 1.

Mfano ikiwa maDC wote ni wenye ndoa(bila watoto), fedha watayolipwa ni kama ifuatayo:

200,000×14×48×2= Tshs. 268,800,000/= (subsistence allowance)

Disturbance allowance - ni mshahara wa mwezi×miezi 12×10%
4,500,000×12×10%×48=Tshs. 259,200,000 Posho ya Usumbufu
Takribani Tshs. 528,000,000/= itakatika hapo,

Ukijumlisha na posho za watoto na safari njiani inafika hiyo Tshs. 720,000,00/=
Balaa zito mzee wa kazi
 
Back
Top Bottom