Upembuzi wa kina inabidi ufanyike ili kujua adui wa kweli wa hao watu ulio wataja alikuwa ni nani, maana unaemtaja ukiacha madaraka yake yale mengine alikuwa mwenyekiti wa chama chake.
Mapokeo ya mateso na ukatili yaliranda hadi kuvifikia viambaza vya jumba letu la haki na taratibu za familia yetu, na huko ndiko tulikoshuhudia vituko Lisu akiwa mjumbe wetu katika jumba hilo na ameumia akiwa kazini, mh hadi leo huwa siamini macho na masikio yangu kuhusu alicho kifanya mzee wa baraza,alikataa kulipa matibabu,akamfukuza kazi na kumpa mateso mengi ya kisaikolojia.
Haya akasema adamke akalalamike kunako PILATO wetu kuhusu maamzi ya mzee wa baraza kubagaza haki zake, unayakumbuka majibu ya pilato? Na walinzi wetu nao je, wewe hujasikia kuwa upelelezi umekwama kumsubiri dereva wa mlalamikaji! maajabu,hukusikia wenzetu mabeberu walijitolea wamtafute huyo adui wa Lisu, ulisikia majibu yao? hahahaha kuwa eti wanao ueledi wa kinguli kumaliza tatizo hili, ulisha wahi kusikia wamemjua mhusika?
HAKI,HAKI,HAKI bado ingali tumboni mwa mama yake!
kwa kifupi adui wa LISU hajulikani hadi leo kwa hali hiyo HATARI juu ya maisha yake bado ipo.