Sheillah Sheillah
JF-Expert Member
- Jun 17, 2020
- 653
- 1,698
Habari?
Unamtafuta fundi kisha unampa kazi yako na unampa malipo yake kama mlivyokubaliana.
Akimaliza kufanya kazi yako anaipiga picha na kuianika mitandaoni akijitangaza kwamba ni yeye kaifanya.
Hapa mfano mkubwa ni fundi wa ujenzi, deco, kupaua ,rangi nk. Wanafanya kazi kisha wanapiga nyumba yako picha na kuianika mitandaoni.
Wengine ni fundi nguo. Unatafuta mshono wako wa nguo yako ya siku yako muhimu mfano harusi, kisha unampa kazi. Akimaliza anaivalisha kwenye mdoli anaiweka kama matangazo na kuituma mitandaoni.
Je ni sahihi nikulipe pesa ufanye kazi yangu kisha utumie kujitangaza bila makubaliano na mimi?