Ni sahihi fundi kupiga picha kazi aliyopewa aifanye, na kuitumia kujitangaza bila makubaliano na mwenye kazi?

Ni sahihi fundi kupiga picha kazi aliyopewa aifanye, na kuitumia kujitangaza bila makubaliano na mwenye kazi?

Sasa umenijibu vizuri, samahani kwa lugha kali.

Mimi jana nimeenda kusuka. Amenisuka nimependeza na nimemlipa hela yake. Baadaye napita instagram nakuta kumbe mimi bila kujua amenichukua video amepost. Nikamwambia ashushe post au anirudishie hela yangu ili nijue mimi ni modo wake wa matangazo.

Wiki kadhaa nyuma mpiga picha alikuja nikafanya photo shoot za gender reveal za my unborn baby. Na lengo ni niziweke baada ya kujifungua. na kila picha niliilipia.
Sasa na yeye akazipost kwenye page yake. Bila ruhusa yangu.

Sasa ndio ninawaza ni sahihi au sio sahihi? au ni mimi nina matatizo.

Bila makubaliano sio sahihi.
Ni sahihi kwa kitu ambacho ni mali yako
 
huo ufundi angeufanya sasa kwa hela yake ndio ajitangaze.
Hii Mambo inaboa sana kwa ma MC wa shughuli aiseee

Mtu umeenda zako kwenye harusi
Umepiga zako masanga
Unaruka majoka kama yote

Afu asubuhi unakuta watu wanakutag instagram,
Kumbe mjinga MC kakupost instagram

Na wife home anakuwashia Moto coz ulienda kwenye harusi bila kuaga

Aiseee ma MC
Punguzeni huu ujinga
 
Hii sjui niiweke kundi la wenye chuki,wabinafsi au wivu kwa sababu hakuna shida yoyote kwa yeye kuipost popote pale
 
Una akili? unajua kusoma na kuelewa?
umeona nimeandika sitaki apige picha mali yangu? Mimi nimeuliza ni sahihi au sio sahihi.
Je kama mimi ni fundi cherehani nimepiga picha nguo ya mtu na sasa ananiletea shida ndio maana nataka kujua ni sahihi au sio sahihi?
..hii nchi ina watu wa hovyo mno! na huyo ni mmoja wao hana akili hata 1
 
Hii Mambo inaboa sana kwa ma MC wa shughuli aiseee

Mtu umeenda zako kwenye harusi
Umepiga zako masanga
Unaruka majoka kama yote

Afu asubuhi unakuta watu wanakutag instagram,
Kumbe mjinga MC kakupost instagram

Na wife home anakuwashia Moto coz ulienda kwenye harusi bila kuaga

Aiseee ma MC
Punguzeni huu ujinga
Hawa ndo wajinga kabisa yani wanatumia watu kujiongezea wafuasi...binafsi lazima aifute na fidia atanipa...sababu ata mm ninayo akaunti mtandaoni na sijipost y unipost wewe...??
 
Watanzania wengi hatujatofautiana roho mbaya na wale Polisi walioua huko Mtwara....unakuta yeye anafanya kila kitu kwa kuangalia mtandaoni ila cha kwake hataki watu wengine waangalie roho mbaya tu hiyo...
Ishu siyo kuangalia mtandaoni ila ni je ameongeza nn katika alichokiona ndo maana ya ubunifu...huyo fundi yeye kaongeza nn
 
Mkuu, kwani anapoitangaza anataja na majina ya Mmiliki?

Mfano;
Hii nyumba ni ya Ms Sheillah, ipo mtaa wa Kinondoni B. Paa na urembo wa ndani nimefanya mimi, Fundi Restart. Hebu angalia ilivyopendeza.

Kama hatoi maelezo ya Mmiliki basi sioni shida. Picha hizo ndizo CV yake. Bila shaka hata wewe ulishawishika baada ya kuona kazi zake.

Lakini kama ni kitu ambacho hukitaki, basi mwanzo wa makubaliano yenu mtahadhari kuwa usingependa nyumba yako ipigwe picha.
Siyo kweli hizo ni janja janja zatulikotoka siyo tunakoenda cv ya picha ni huko nyuma lazima ujue hilo...fundi mjenzi lazima uwe umewahi kuona kazi yake au mtu wako wa karibu awe amemuona kinyozi pia na wengine pia...sasa kazi yako kuwepo kwenye picha haitoi uhakika wa ubora na uaminifu wako....ajue jinsi ya kubrand bidhaa yake ili apate imani na heshima toka kwa watu siyo kwa kutumia faragha za watu hivhiv mwisho ulaumu watu wana roho mbaya ni ujinga....
 
Sasa umenijibu vizuri, samahani kwa lugha kali.

Mimi jana nimeenda kusuka. Amenisuka nimependeza na nimemlipa hela yake. Baadaye napita instagram nakuta kumbe mimi bila kujua amenichukua video amepost. Nikamwambia ashushe post au anirudishie hela yangu ili nijue mimi ni modo wake wa matangazo.

Wiki kadhaa nyuma mpiga picha alikuja nikafanya photo shoot za gender reveal za my unborn baby. Na lengo ni niziweke baada ya kujifungua. na kila picha niliilipia.
Sasa na yeye akazipost kwenye page yake. Bila ruhusa yangu.

Sasa ndio ninawaza ni sahihi au sio sahihi? au ni mimi nina matatizo.
Kuchukuliwa video au picha bila ridhaa yako ni kosa kwa sheria ya cyber.
Privacy yako hapo imekuwa violated.
Hata hilo swala la fundi kufanya kazi na kupiga picha lazima aombe idhini kwako mwenye mali.
Ni vile wabongo hatuna tabia za kupeana mkataba hata kwenye kazi za ujenzi kama hizo. Kwenye mkataba unambana fundi kabisa
 
Sahihi kabisa kuna mtu anatetea huu ujinga anasahau ndo maana mitandao inatoa nafasi ya ww kumtag mtu nayeye kutoa ruhusa au kukataa wanakataa hizi kesi za hakimiliki na faragha za watu
 
Habari?

Unamtafuta fundi kisha unampa kazi yako na unampa malipo yake kama mlivyokubaliana.

Akimaliza kufanya kazi yako anaipiga picha na kuianika mitandaoni akijitangaza kwamba ni yeye kaifanya.

Hapa mfano mkubwa ni fundi wa ujenzi, deco, kupaua ,rangi nk. Wanafanya kazi kisha wanapiga nyumba yako picha na kuianika mitandaoni.

Wengine ni fundi nguo. Unatafuta mshono wako wa nguo yako ya siku yako muhimu mfano harusi, kisha unampa kazi. Akimaliza anaivalisha kwenye mdoli anaiweka kama matangazo na kuituma mitandaoni.

Je ni sahihi nikulipe pesa ufanye kazi yangu kisha utumie kujitangaza bila makubaliano na mimi?
Sioni shida,kwani hataji jina lako wala kuwa hapo ni wapi.Anazungumzia kazi yake tu
 
Habari?

Unamtafuta fundi kisha unampa kazi yako na unampa malipo yake kama mlivyokubaliana.

Akimaliza kufanya kazi yako anaipiga picha na kuianika mitandaoni akijitangaza kwamba ni yeye kaifanya.

Hapa mfano mkubwa ni fundi wa ujenzi, deco, kupaua ,rangi nk. Wanafanya kazi kisha wanapiga nyumba yako picha na kuianika mitandaoni.

Wengine ni fundi nguo. Unatafuta mshono wako wa nguo yako ya siku yako muhimu mfano harusi, kisha unampa kazi. Akimaliza anaivalisha kwenye mdoli anaiweka kama matangazo na kuituma mitandaoni.

Je ni sahihi nikulipe pesa ufanye kazi yangu kisha utumie kujitangaza bila makubaliano na mimi?
Hao ndio "Wachora Ramani".
Muda haupiti unaamia kwako, unaibiwa..
 
Back
Top Bottom