#COVID19 Ni sahihi Humphrey Polepole kuonesha Msimamo wake wa kutochanjwa?

Mh Rais kaacha watu wachague. Sioni shida ya wanaounga mkono kuonesha hadharani misimamo yao na hata wale wanaopinga pia. Imekua dhambi kusema sitachanjwa hadharani wakati ni haki na uhuru wa mtu kuchagua atakacho.Imekua haki mtu kunadi ubora na umuhimu wa chanjo lkn kosa kubwa sana mtu kuelezea mattz ya chanjo na habari zote hasi kuhusu chanjo. Kuna tatizo sehemu.
 
Huchanji piga kimya. Kelele za nini!??
Hakuna kupiga kimya, lazima tuwaamshe nyumbu kama wewe mnaopenda kubugia michanjo hovyo hovyo bila kujua imetoka wapi!

Hii inatakiwa iwe kampeni endelevu ili wajinga wote waamke.

Zile enzi za kuwadunga watu masumu huku mnapiga dili za mpunga na mabeberu zimefika mwisho.
 
Ipo shida tena si ndogo, maana wanaotaka chanjo wanaona wanahaki kuongea kuhusu hiari yao ila wasiotayari kuchanjwa wanatizamwa kama ni haramu wao kuongea maamuzi yao mbele ya watu.

Watu wamesahau WASIWASI NI AKILI PIA.

Dunia nzima chanjo bado ni mjadala. Ikiwa bado mjadala unaendelea hata kwa matabibu itakuwaje kwetu sisi??

Nadhani tuchague moja, ikiwa tunataka wasiotaka chanjo wakae kimya basi hata wanaotaka chanjo wanyamaze kimya mambo yaende kimya kimya. Kama tunataka hamasa ya chanjo turuhusu na wengine kuzungumza pia.
 
Hivi kwanini wale wote wanaosema hawachanjwi (atleast for now) wanahusishwa na hiki kinachoitwa hujuma!? Hujuma ipi tena hii? Haya ni madhara ya kufundishwa ukondoo na kufuata kila anachosema mtawala hata kama akili yako inakuambiwa hii sio sawa.

Itafika muda watu watachanjwa tu. Ni kama yellow fever. Unaweza usihitaji kuchanja ila siku unataka kuvuka kupitia pale terminal #3 ndio utaambiwa huwezi kuvuka hapa maana kule uendako huingii bila hiyo chanjo.
 
Hawa madalali wa chanjo hawawezi kuelewa hii. Wanataka wakudunge machanjo bila kuulizwa swali.

Ukihoji wanakwambia nyamaza ati haujui sayansi!

Kwao sayansi ni kudunga watu machanjo bila kuhojiwa swali lolote.

Yaani unadungwa kimya kimya uende ukagande damu huko kwako utajijua mwenyewe ilimradi wao washapewa kibunda cha dola na mabeberu.
 
Nashindwa kuelewa hata mimi.Kundi linaloamini katika chanjo limejipa mamlaka ya kuongea chochote kuhusu chanjo. Hili ni swala la uhai, sasa mtu anaposema nachanjwa maana yake anaona ni muhimu kwa uhai wake.Yule anayesema sichanjwi pia kaona ni muhimu kwa uhai wake.Sasa kwanini iwe vita?
 
Huyu alisema Magu mzima anachapa kazi.
Huyu amesema hachanjwi.
Kuna shida gani
 
Mataga tu..
 
Inasikitisha mnoo.. Upole, uungwana, hekma ya mtu inapo tasfiriwa kama "udhaifu"..pole pole gwajima na washirika wao. Kuna lugha wanaielewa...!! Nadhani wakati umewadia wa kuwaelewesha.. Kwa lugha hiyo..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…