#COVID19 Ni sahihi Humphrey Polepole kuonesha Msimamo wake wa kutochanjwa?

#COVID19 Ni sahihi Humphrey Polepole kuonesha Msimamo wake wa kutochanjwa?

Rais Samia awashughulikie hao kenge haraka ni wahujumu wa wazi kwa jitihada zake,awaweke pembeni kabisa na utawala wake na wala haiwezi kuwa nongwa maana hata Magufuli alifanya hivyo kwa baadhi ya wana CCM wenzake mfano ni Membe.
Yaani hawa Kenge ni wengi saana asiwangalie usoni aisee ,nadhani ameshawaona awashugulike na sisi tupo pamoja nae kwenye hilo kwa asilimia mia moja
 
Yaani hawa Kenge ni wengi saana asiwangalie usoni aisee ,nadhani ameshawaona awashugulike na sisi tupo pamoja nae kwenye hilo kwa asilimia mia moja
Labda alete kutoka Zanzibar,lakini wa huku bara,😂😂😂 wanavaa barakoa mbele yake huku wakilaani utumwa huo.
Hii TZ ya Magufuli mtahangaika na akina Polepole JPM walimuelewa Sana.
Badala ya kujibu hoja mnakimbilia kulaumu wanaotuma akili zao.

Hebu tuambie Sasa wewe ukichomwa hiyo chanjo itafanya kazi kwa muda gani mwilini?

Kwanini mtu lazima ajaze consent form tofauti na chanjo zingine?

Unajua short term na long term side effects za hizo chanjo?

Je hii chanjo inakukinga na maambukizi?
 
Misimamo ni kitu chema sana, kuliko kuwa bendera fata upepo, ni jambo jema kusimamia unapoamini
Kweli kabisa. Kuwa na msimamo ni jambo jema. Mimi ni CCM na Mtumishi wa Serikali lakini SITACHANJA kwani chanjo ni hiari na nimeamua kutochanja. Wanaotaka kuchanja, wakachanje!
 
Wafumbe midomo yao basi... Kwani tumewaomba waongee... Nonsense.

Huchanji piga kimya. Kelele za nini!??
Bora huyo anayeongea kiliko anOfanya maigizo yakuchanjwa nonsense [emoji16][emoji3][emoji23]
 
Hakuna kupiga kimya, lazima tuwaamshe nyumbu kama wewe mnaopenda kubugia michanjo hovyo hovyo bila kujua imetoka wapi!

Hii inatakiwa iwe kampeni endelevu ili wajinga wote waamke.

Zile enzi za kuwadunga watu masumu huku mnapiga dili za mpunga na mabeberu zimefika mwisho.
👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍
 
Wafumbe midomo yao basi... Kwani tumewaomba waongee... Nonsense.

Huchanji piga kimya. Kelele za nini!??
Unachanja piga kimya kwani wasiotaka chanjo wamewaomba muongee?
Acheni watu watoe maoni yao ilimradi hawavunji sheria.
 
Rais anapingwa zaidi ndani ya CCM kuliko hata kwa UPINZANI, na ni muhimu zaidi kujenga imani kwa wananchi kupitia mahitaji yao kuliko kujenga CHUKI kwa watu ambao hawakubaliani na mawazo yako, mwaka 1994 enzi za Rais Mwinyi kulikuwa na G55, naona 2024 kuna G55 inaandaliwa mapemaa na kuna mtu namwona anapasha kuingia CHAMWINO 2025 mapemaaaa kama kunywa uji wa mgonjwa
 
Mkuu sukuma gang woote na mataga woote hawako pamoja na Mama na wanamuonesha dharau waziwazi kabisa...

Lakini subiri...dawa yao ishaiva.

Kipindi cha dictator hakuna Taga lolote lilikuwa na uwezo wa kunyanyua pua yake..hata kwa matukio ya aibu yalokuwa yakifanywa nae..
Subiri.
Hata mama 2020 hakuwahi kuvaa barakoa. Kwa nini
 
Viongozi wetu wasipoangalia ishu ya chanjo italigawa taifa.

Kwani ni taifa moja mpaka sasa? Isitoshe huyo Polepole ana ushawishi gani mpaka aligawe taifa kwa msimamo wake? Alishapoteza ushawishi anataka kupata publicity ya bei chee. Alikuwa na msimamo wakati wa rasimu ya Warioba, alipoingia kwenye mlo akaanza kutetea upande wa mlo na kuacha msimamo. Hicho anachoonyesha kwa sasa sio msimamo, bali anataka arudishwe kwenye mlo mkubwa tena.
 
Back
Top Bottom