Ni sahihi kumpa kichapo dingi iwapo anampiga mama?

Ni sahihi kumpa kichapo dingi iwapo anampiga mama?

baba yako akikwambia ana mpiga sababu amemnyima utelezi utajibuje,je nawewe nisahihi mtoto wako kukuchapa makofi pale unapogombana na mama yake? mambo mengine nikujipa laana mwenyewe, maana ulichomfanyia baba yako ndivyo utakavyo fanyiwa na kwa uzao wakopia
 
Anatandikwa tu akileta upuuzi wazazi wenye kujitambua hawakwaruzani mbele ya macho ya watoto kama ugomvi ameshindwa kuuacha baada ya kuamuliwa na kujifanya nunda kuendelea kumfanya kibogoyo maza kinacho fuatia ni makonde mpaka akili zimrudi
Vipi km mama yako huyo ndo anamnyuka baba yako, vipi utampiga mama yako. Kichwa kisicho na maarifa ni sawa choo kilichojaa kinyesi. Yataka moyo.
 
Hivi wazazi mnagombana vipi mbele ya watoto, achilia mbali kupigana!!

Aibu kubwa hii...
Mambo haya unaweza dhani ni story ilaa omba yasitokee kwa wazazi wako ni Mtihani mkubwa sanaa.. Kama mzee hajitambui anajenga chuki na mwisho laana kwa watoto lakini Nilichojifunzaa Jitahidi kusuluhisha ugomvi wa baba na mama bila kupendelea na mbebeshe mzee majukumu ya kumantain amani ndani ya familia..
 
Sio sahihi kabisa, tena huyo mtoto hana adabu
Jamaa mmoja mtu mzima na familia yake ana wazazi wake ambao wako above 60. Sasa dingi yake akajitia ukidume kumpiga mama yake mbele ya jamaa. Jamaa akaingilia na kumtwanga baba yake, akimkunja chini. Hili suala ni sahihi? Baba yako akimpiga mama yako mbele yako unaweza ungilia kupigana na dingi?
 
Back
Top Bottom