Ni sahihi kumpa kichapo dingi iwapo anampiga mama?

Ni sahihi kumpa kichapo dingi iwapo anampiga mama?

Mambo haya unaweza dhani ni story ilaa omba yasitokee kwa wazazi wako ni Mtihani mkubwa sanaa.. Kama mzee hajitambui anajenga chuki na mwisho laana kwa watoto lakini Nilichojifunzaa Jitahidi kusuluhisha ugomvi wa baba na mama bila kupendelea na mbebeshe mzee majukumu ya kumantain amani ndani ya familia..
Ni kujitahidi kuacha malumbano na ngumi mbele za watoto tu mkuu hakuna namna nyingine.
 
Mzee wangu anapigo kama hizo sema yeye matusi makubwa anamtukana maza ila yeye ni mtu wa pombe chakari,huwaga najibizana naye tu kumtisha na kumpa biti sijawahi kumpiga ila anakera Sana usiombe yakutokee ktka familia Yako.Yani matusi ya nguoni anayotokukana kila mtu anasikia yaacheni, Mambo mengine huwezi pata laana ila usimpige ila mchimbie mikwara tu kama huyu wangu hadi anaogopa anaona nitampiga kumbe simpigi
 
Ila hao watoto kumpiga baba yao badala ya kuamulia ugomvi sio Domestic violence ni international violence si ndio?!
Mjomba kibaka kudhuru au kuua mtu kwa sababu yoyote ile ni kosa, ila hakimu kufunga au kunyonga huyo kibaka siyo kosa, kama haujaelewa soma tena
 
Kuna washikaji wangu walifanya kama unavyo taka kufanya wewe . Walimchezeshea kichapo mshua wao hadi nguo za mshua zikavuka. Hawa jamaa ni mtu na mdogo wote wanaume wana mdogo wao wakike pia huyu wa kike alikua bado mdogo .


Ila hawa jamaa hakuna kitu walifanya kikafanikiwa na hakuna kitu cha thamani walinunua kikadumu zaidi ya mwezi.

Mshua wao alicho kifanya aliamua kuto Fukuza mtu wala yeye kuondoka ila aliamua kujitenga na wao. Alichukua tu geto moja la nje na kuwaachia nyumba kubwa na wao na mama yao.

So mzee anakageto kake la nje hana habari na mtu na kubwa kuliko mzee ana pensheni yaani anaishi vimaisha vyake na tangu siku hiyo hajawahi ongea na hao watoto na huu ni mwaka 15 na zaidi tangu tukio litokee.

Yaani mzee ni kama amewatenga na hataki hata habari zao. Vikao vya kibalozi vya aina yote vilikaliwa kusuruhisha jibu la mzee lilikua hata nyie mnashida na watoto chukueni kama mnawataka na anae taka huyo mke amchukue pia mimi sina matatizo na mtu .na huyu mwanamke alisha lia machozi ya rangi zote alimaliza ila mzee kadinda

Huyu mzee anapendeza kichizi yani yaani full mastory na watu huku nje na ni mcheshi balaa ila ukitaka kumuuzi mgusie Jabari za wanawe.


So bro kuwa makini na hatua unayo taka kupiga
Stori za vijiweni. Pia sijasema mimi ndiyo nataka kuchukua hiyo hatua.
 
Anatandikwa tu akileta upuuzi wazazi wenye kujitambua hawakwaruzani mbele ya macho ya watoto kama ugomvi ameshindwa kuuacha baada ya kuamuliwa na kujifanya nunda kuendelea kumfanya kibogoyo maza kinacho fuatia ni makonde mpaka akili zimrudi
Safi.
 
baba yako akikwambia ana mpiga sababu amemnyima utelezi utajibuje,je nawewe nisahihi mtoto wako kukuchapa makofi pale unapogombana na mama yake? mambo mengine nikujipa laana mwenyewe, maana ulichomfanyia baba yako ndivyo utakavyo fanyiwa na kwa uzao wakopia
Vipi baba yako wa kambo akinyimwa utelezi na mama yako halafu akaanza kumpiga? Au hili ni kwa baba mzazi tu!!?
 
Back
Top Bottom