Ni sahihi kumpa kichapo dingi iwapo anampiga mama?

Ni sahihi kumpa kichapo dingi iwapo anampiga mama?

Kuna washikaji wangu walifanya kama unavyo taka kufanya wewe . Walimchezeshea kichapo mshua wao hadi nguo za mshua zikavuka. Hawa jamaa ni mtu na mdogo wote wanaume wana mdogo wao wakike pia huyu wa kike alikua bado mdogo .


Ila hawa jamaa hakuna kitu walifanya kikafanikiwa na hakuna kitu cha thamani walinunua kikadumu zaidi ya mwezi.

Mshua wao alicho kifanya aliamua kuto Fukuza mtu wala yeye kuondoka ila aliamua kujitenga na wao. Alichukua tu geto moja la nje na kuwaachia nyumba kubwa na wao na mama yao.

So mzee anakageto kake la nje hana habari na mtu na kubwa kuliko mzee ana pensheni yaani anaishi vimaisha vyake na tangu siku hiyo hajawahi ongea na hao watoto na huu ni mwaka 15 na zaidi tangu tukio litokee.

Yaani mzee ni kama amewatenga na hataki hata habari zao. Vikao vya kibalozi vya aina yote vilikaliwa kusuruhisha jibu la mzee lilikua hata nyie mnashida na watoto chukueni kama mnawataka na anae taka huyo mke amchukue pia mimi sina matatizo na mtu .na huyu mwanamke alisha lia machozi ya rangi zote alimaliza ila mzee kadinda

Huyu mzee anapendeza kichizi yani yaani full mastory na watu huku nje na ni mcheshi balaa ila ukitaka kumuuzi mgusie Jabari za wanawe.


So bro kuwa makini na hatua unayo taka kupiga
Funzo kabisa hili.
 
Anatandikwa tu akileta upuuzi wazazi wenye kujitambua hawakwaruzani mbele ya macho ya watoto kama ugomvi ameshindwa kuuacha baada ya kuamuliwa na kujifanya nunda kuendelea kumfanya kibogoyo maza kinacho fuatia ni makonde mpaka akili zimrudi
Huyu unaemwita mama mwenzio anamwita mke au baby wake nawamejuana kitambo kabla hujazaliwa sasa usimpangie mtu maisha nampenz wake kaa pemben au nenda kwamkeo
 
huyo mzee kwanza hana adabu wala busara,....suala la mzee kupigwa alistahili kabisaaaa....
 
Jamaa mmoja mtu mzima na familia yake ana wazazi wake ambao wako above 60. Sasa dingi yake akajitia ukidume kumpiga mama yake mbele ya jamaa. Jamaa akaingilia na kumtwanga baba yake, akimkunja chini. Hili suala ni sahihi? Baba yako akimpiga mama yako mbele yako unaweza ungilia kupigana na dingi?
Sio sahihi kabisa kupiga baba yako,angewaamua tu lakini sio.kumpiga
 
Mzee wangu anapigo kama hizo sema yeye matusi makubwa anamtukana maza ila yeye ni mtu wa pombe chakari,huwaga najibizana naye tu kumtisha na kumpa biti sijawahi kumpiga ila anakera Sana usiombe yakutokee ktka familia Yako.Yani matusi ya nguoni anayotokukana kila mtu anasikia yaacheni, Mambo mengine huwezi pata laana ila usimpige ila mchimbie mikwara tu kama huyu wangu hadi anaogopa anaona nitampiga kumbe simpigi
Hama kwenu haraka hizo laana unazitafuta iweje matusi yakukele wewe namamako hayamkeri mana yangemkera angeshavunja ndoa tangu enz zaujana
 
Huyu unaemwita mama mwenzio anamwita mke au baby wake nawamejuana kitambo kabla hujazaliwa sasa usimpangie mtu maisha nampenz wake kaa pemben au nenda kwamkeo
Vipi baba wa kambo ambaye mama yako naye ni mke na babe wake?
 
Jamaa mmoja mtu mzima na familia yake ana wazazi wake ambao wako above 60. Sasa dingi yake akajitia ukidume kumpiga mama yake mbele ya jamaa. Jamaa akaingilia na kumtwanga baba yake, akimkunja chini. Hili suala ni sahihi? Baba yako akimpiga mama yako mbele yako unaweza ungilia kupigana na dingi?
Oa na wewe acha ujinga
 
Kwenye hili epuka Sana laana ya mshua. Sisi alikua alikua anawapiga kweli.. tulikua tunakaa mbali Sana na huo ugomvi. Sasa siku Moja kaka akijitia kiherere chake kuingilia ugomvi. Mzee akaitisha kikao akasema mke anamnyimba unyumba ndo maana amapiga.

Tangu siku hiyo Kila Mtoto alikaa mbali na huo ugomvi. Ila Leo wanapendana mno na wake zake. Kaka Tena akalianzisha siku nyingine Tena. Mzee hakuongea kitu. Ila had Leo kaka alishaishia kwenye ulevy wa pombe. Laana ya Mzee kaa nayo mbali sana
 
Back
Top Bottom