Mkuu Sasa ukipika unaishiwa damu?, Mimi nadhani mwanamme aliyeoa sio tu napaswa kupika, Bali pia anapaswa kufua nguo, kuogesha watoto na kufanya shughuli zote za nyumbani ambazo zinafanywa na mwanamke.
Huu ni ukiritimba uliokithiri kwa baadhi ya wanaume wanaoamini kuwa wako juu kuwaliko wa wanawake, Mimi kwangu nafua nguo, naogesha watoto na kupika na pika Ila sijawahi kuona ikiwa nadharauliwa na mke wangu, zaidi ya yote, naagizwa kununua mboga, chumvi, nyanya na kadhalika .
Upendo wangu kwa mke wangu uko pale pale, yeye pia ananipenda na kuniheshimu.
Don't complicate life kijana!!