Ni sahihi kwa Mwanaume aliyeoa kupika?

We unapika kaka? Kama hupiki nini kinakuuma hivyo hadi unaanzisha uzi? We unahisi mambo yote unayofanya yanawafurahisha wanaume wenzio? Mbona hawakusemi na wanakuacha na machaguo yako?

Hujui kuna wanaume wanatafuta hela na wanazo kukuzidi, alafu wanatoa hicho kichapo kwa wake zao kukuliko wewe na hao hao wanasaudia wake zao kupika na wana enjoy life kukuliko?
 
Sio wote wanafanya kazi kwa muhindi kama wewe, kuingia saa 12 kutoka haijulikani.
Kazi ni uhai, ni kipimo cha ukamilifu wa utu, bila kujali anafanya kazi kwa nani
 
Mwanamke anakuwa ana test dawa zake kama zimeanza kufanya kazi kama bado arudi tena kwa babu yaani mwanamke ukimsaidia kazi siku moja tu basi anaona dezo kila siku atakutest ukiingia king tu umeisha.
 
Sio kwamba kisa ni mwanamke bas anajua kupika kila kitu kama kinavyo takiwa.

Sio Siku zote mke atakuwa na afya na nguvu za kuweza kunyanyuka kukupikia

Ni moja ya njia za kudumisha mapenzi yao, kuonesha appreciation juu ya kaz nzuri anayoifanya kwa kumuhudumia mme pamoja na familia bas anaamua kumpa zawadi ya kumpikia chakula kizuri

Kupika ni interest kama kishabikia mpira au movies.
 
Mmh! kazi kweli kweli
 
Safi sana mkuu
 
Kuna huyo mmoja anakuna hadi nazi 😂😂 basi akiweka chumvi anaonja mwenyewe kwa mwiko kama imekolea yani ni huruma
 
Ni msaidizi kwel hujakosea, kwa iyo pika kwanza ukichoka ukusaidie [emoji23][emoji23][emoji23]
Kupika ndo miongoni mwa kazi za mwanamke kumsaidia mumewe wakati mumewe akiwa katika harakati za kutafuta pesa. Kuna msemo wanasema mwanamume hakai jikoni. Na mume akioa wanasema kapata jiko iweje sasa apike yeye na jiko lipo?
 
Una miaka mingapi?
 
Kupika ndo miongoni mwa kazi za mwanamke kumsaidia mumewe wakati mumewe akiwa katika harakati za kutafuta pesa. Kuna msemo wanasema mwanamume hakai jikoni. Na mume akioa wanasema kapata jiko iweje sasa apike yeye na jiko lipo?
Wanaopika acha wapike lakini wasijitetee eti wanawasaidia wake zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…