Sababu za mwanzo kabisa za kutoa govi ninazozijua mimi ni sababu za kiimani zaidi, ambapo mtu wa kwanza kabisa kukata govi alikuwa ni mzee Ibrahimu katika kitabu cha Mwanzo 17;10, pale Mungu alipofanya naye agano na kumuahidi kuwa atampatia uzao mwingi, na tena mzee Ibrahimu hapo kabla alikuwa akiitwa Ibraimu na baada tu ya kukatwa govi akabatizwa jina jipya akaitwa Ibrahimu, yeye alikatwa govi yake akiwa na umri wa miaka tisini na tisa (99). Hili ni agizo la Mungu Mwenyewe kwa Ibrahimu na kizazi chake chote na watumwa wake wote. Ila kwa siku za hivi karibuni nimewahi kusoma sehemu fulani ikitoa sababu za kutahiriwa ikiwa ni masuala ya kiafya zaidi. Niishie hapa.