Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Dodoma kuna madini gani?
 
Tanganyika ni kijiji ambacho unakwenda ukifika hapo ndo mwisho wa barabara hakuna kuendelea....siku niliyofika kwenye kile kijiji nilijiuliza maswali mengi sana khs wale watu wanavyoishi kule.
 
Bora hata mpanda, kuna mahali panaitwa MAJIMOTO aisee huko nilipoenda nilijiuliza qatu wamefuata nini, na wengi wao ni wasukuma kule...Ajabu ni kwamba they are making money ile hatari. Ni matajiri wa kutupwa kutokana na kilimo ufugaji na madini.
Yes majimoto nishawahi kufika, hilo jina linatokana na Chem Chem ya majimoto iliyopo hapo kijijini
 
Kuna Kijiji kinaitwa mapangali kipo Iringa.

Unashukia ilula alafu unachukua bodaboda na ni mwendo wa saa 1 nauli kwasasa inaweza kuwa 25000 maana mara ya mwisho ilikua 20000 na hakuna gari la abiria kwenda kule .
Uwe na uvumilivu haswa maana utapanda milima mpaka utahisi bodaboda inapinduka.
Nilivofika kule nikajiuliza hivi watu wanaishije huku japo pesa ipo.
 
Niliwahi kufika kule mwaka 2002 mpaka mimea inaungua kutokana na baridi nilifika kandete, kyejo mpaka isange kupitia kiwanda Cha majani ya chai Katumba au Tandale Tukuyu Mjini.
Nimezunguka sana maeneo hayo, na njia yao ile ya mawe mawe ukitoka katumba kuanza kuitafuta mwakaleli, ila baridi ipo ifupa aisee ,hiyo ni ndugu yake na makete, yani mchana wa saa nane watu wanaota moto
 
Wewe kilimanjaro una maanisha Moshi, njoo same na mwanga ndiyo utajua hujui. Watu huku wamekauka unaweza kuwapasua kuni na ukapikia maharage yakaiva haraka kuliko stima
Wilaya ya mwanga iko vizuri Sababu watu wengi wanaishi miliman mfano usangi na ugweno kunafikika kwa lami

wilaya ya same ndo changamoto Kuna vijiji kama chome unajiuliza watu wanaishije kwanza ni mliman sana
 
Umeishawahi kufika mamba kwa nabii eliya? Guantanamo ni mbinguni
Wilaya ya same jiographia yake ni ngumu sio mimba hata chome hapafikiki kirahisi ndomaana wapare wa same hawapendi kwenda kwao sababu hapafikiki ni tofauti na wapare wa same kwao kuna lami yaan kunafikika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…