Underwood
JF-Expert Member
- Dec 25, 2020
- 1,909
- 3,120
Kuna kijiji nilifika kutafuta ndizi biashara miaka hiyo.
Aisee ni mbali katikati ya turiani na korogwe njia ya pori kwa pori.hamna magari ni kwenda kwa baskeli tu alafu unachepuka kwenda mlimani huko nikakuta kakijiji aisee vijumba kichekesho,alafu wana mfalme wao yaani chakula wanakula woote familia zoote pale kwa mfalme.
Kila kaya inaleta ilichopika pale.
Nilikula mboga mboga mpk nilikoma.
Siku nikalogwa nikanunua kuku 2 wameniuzia wao wenyewe kaya 1 niliokuwa nakaa nikawapa wapike nikajua ntakula japo nusu aaah wakapeleka kwa mfalme kule tunakokula nikaambulia kibawa,yaani mkulu ana nyofoa kinyama anampa mtu kushoto au kulia kwake kinatumwa mpk kikufikie kila mtu kakishika
Nilikasirika sana.
Ertugul [emoji23][emoji23][emoji23]