Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Watu mna unafiki humu hivi mmeshindwa kutaja vijiji vya Singida kweli???
Watu wa singida vijijini ni watu wa ajabu sana. Imagine mtu ana kuku zaidi ya 50 lakini hachinji hata iweje...Ajabu ni kua hua wanauza kuku ili wapate hela ya kununua mlendawa kusagwa. Yaani huo mlenda unakua kama unakula ugali na hina zile za miti.
Mnyaturu akija kwako usimpikie kuku wala nyama pika mabamia wanapenda makamasi kamasi kwente chakula chao😂🏃🏃
 
emu tufafanulie kuhusu majimoto, pako vipi kwenye uwekezaji wa kilimo
Nimefanya kazi kama na kuishi huko. Nakushauri, nenda kapige mishe. Ni eneo zuri sana na watu wanalima sana. Kilimo kikubwa ni Mpunga na wanatoa kwenye bonde la Mwamapuli, Mamba, lake Rukwa na Kasansa. Kuna elimu za umwagiliaji za uhakika na Mpunga wanaolima hawatumii mbolea. Pana mzunguko mkubwa wa Pesa kwani wasukuma na Waha wengi wameinvest huko kwenye Kilimo, Biashara na ufugaji. Pia wanalima ufuta kama zao lingine la kibiashara. Pamechangamka sana na muda wataipata hadhi ya Mamlaka ya Mji mdogo Maji moto. Panapitika mwaka mzima kwa barabara za uhakika, unaweza kwenda Sumbawanga, Mpanda Mjini na Tabora pitia daraja la Kavuu. Nenda mkuu, ukiwa na akili unatoka kimaisha. Kunefunguka sana japo ni nilitoka huko 2014
 
hebu fafanua zaidi kuhusu hiki kijiji mkuu, kuna wakati nilitaka kwenda hapo.
Sasa panaweza kuwa Pazuri kwani ni kijiji na sasa ni kata ya Wawindaji. Nimeishi huko japo zamani. Barabara sasa nasikia ni ya uhakika na mawasiliano sasa nasikia yapo. Ni pazuri kwa kweli kwani jamaa wanalima sana japo zao kubwa ni Tumbaku. Kijiji hiki kuna misitu mingi ya asili ukiwa Majanja unapiga maisha oitia Mininga na Mikora. Pia kuna wanyama wengi ukiwa jangili utapiga pesa. Kijiji hiki kuna kijiji kingine jirani kipo Singida kama sikosei, kuna madini na watu wanapiga sana pesa. Ni pazuri bro, nenda kafanye Maisha japo nakushauri Majimoto is the best.
 
Tabora Kuna sehem Moja Kuna njia panda ya kwenda mpanda na barabara lingine linaingia maporini......Picha linaanza mwenyeji alokuja kutupokea usiku mwenyewe alitupoteza, pili hatukua tukiona nyumba Wala chchte ni Giza tu......Tumesogea mbele tukashuka kweny gari kuangalia tuelekee usawa gani katokea bonge bonge ya joka tukakimbilia kweny gari tukaanza tena kuitafuta njia tukaipata

Tulivofika hapo msibani tukala tukala usiku nmelala nasikia kitu kikubwa kipo mgongoni kwangu kuwasha tochi nakutana na panya analinga a kichwa na Putin. Weeeh nlipiga kelele watu wote wakaamka nduki
Asubui nmeamka wakasema tuende tukapaone sehem alipozikwa ndugu yetu tukafika tukaanza kurudi nyumbani tukakutana tena na joka nlikua natetemeka hadi nikaingia period

Tukarudi nyumbani muda wote natembea sion nyumba za watu nkajiuliza Ina maan huku watu wanatokea wapi kumbe huko ndani ya msitu zaid

Siku tunarudi tukakutana barabarani na fisi mara na mbwa mwitu mara nyoka kakaa katikati ya barabara eeeh nyumba tukaona chache sana zenyewe ziko mbali mbali
Tulivofika center bwana weeeh nilijikuta nipo hospital maan nlikata moto gafla baada ya kusema tumbo linauma

Nilijiuliza watu huko wanaish vp, nyoka kila Kona, fisi mbwa mwitu,wanakunywa maji meupe kama maziwa, hospital ni mbali kias kwamba lazima uombe Pooh
Nadhani una maanisha njia panda ya Ipole, wilaya ya Sikonge, Tabora; ukiacha barabara ya kuelekea Mpanda, unayooka kushoto kwako kuelekea Rungwa. Hapo mlipokutana na bonge la joka hapo panaitwa Kitunda. Usipochukua tahadhari unaweza liwa na simba. Mbele kidogo kuna mji unaitwa Kitunda - watu wanachimba madini pale. Ukitoka Rungwa unaelekea Kambi Katoto (upande wa kusini), Chunya kisha unaelekea Mbeya. Unabidi uwe na roho ngumu kiasi ili uweze kuishi kule. Ukitoka Rungwa kuelekea Kaskazini utaingia Itigi, kisha barabara kuu kuelekea Singida au Manyoni.
 
Chato
Najiuliza sana watu wa chato wanaishije.

Kama siyo uchizi lile wazo la kujenga ule uwanja lilitolewaje na fedha zikatengwa.

Sasa kuna mataahira bungeni wakaja na wazo chto iwe mkoa alafu Muleba iwe sehemu ya huo mkoa...
Yaani sisi wahaya tukawe ndani ya mkoa wa chato?

Hii nchi iliingiliwa kinyume na maambile aise
 
Nadhani una maanisha njia panda ya Ipole, wilaya ya Sikonge, Tabora; ukiacha barabara ya kuelekea Mpanda, unayooka kushoto kwako kuelekea Rungwa. Hapo mlipokutana na bonge la joka hapo panaitwa Kitunda. Usipochukua tahadhari unaweza liwa na simba. Mbele kidogo kuna mji unaitwa Kitunda - watu wanachimba madini pale. Ukitoka Rungwa unaelekea Kambi Katoto (upande wa kusini), Chunya kisha unaelekea Mbeya. Unabidi uwe na roho ngumu kiasi ili uweze kuishi kule. Ukitoka Rungwa kuelekea Kaskazini utaingia Itigi, kisha barabara kuu kuelekea Singida au Manyoni.
Kuna watu mna vipaji vya kushika majina ya vijiji
Sehem ambazo nimefila Nanjilinji kama unakunja lindi ruangwa.na ifinsi
 
Uzi mzuri sana, huko maporini inaonekana ndipo penye hela. I wish watu wa serikalini wangeona huu uzi labda wangeingiwa huruma kutafuta hivi vijiji na kupeleka services especially kuwachimbia visima vizuri vya maji na zahanati
 
Kuna vijiji vipi Bumbuli daah wakuu acheni tu tulienda na gari njian watu wanatushangilia kma ni Raisi anapita tukafika mwisho wa barabara tukaanza kubeba jeneza hadi nyumbani tulichoka zaidi ya masaa6 kule tuwaachie nguruwe pori au wahamishiwe vijiji vya Kilimanjaro kuacha Mwanga.
 
Back
Top Bottom