Kuna kijiji kipo katikati ya Kidete wilaya ya Kilosa na Mpwapwa magenge 30 kinaitwa Nana, kwa Mara ya kwanza nilikaa hapo wiki moja bila kuoga, dumu la maji ya mtoni ni buku mnatumia kupikia na kunywa, anayewauzia hayo maji akitoka alfajili kufuata maji na punda anarudi SAA 10 jioni.
Nilipoanza kutafiti maisha yao siku moja Mwenyeji akanipeleka kwa mama mmoja ndio ana club ya pombe za kienyeji ila Mimi nilikwenda kununuwa mihogo asubuhi tuchemshe kunywea chai kambini.
Sasa nikashangaa kila mlevi anayekuja pale amebeba kibegi cha sports mgongoni nikamuuliza mbona hii style siielewi? Akaniambia huku watu hawana pesa ukitaka kunywa pombe unakuja na maindi kwenye kibegi yanapimwa mama muuza anakupa pombe yeye anachukuwa mahindi, aisee Yale maisha ni Bonge la adventure kwangu.
Sehemu zenye madini zina asili ya kutokuwa na maji, madini na maji havikai pamoja, serikali iwahurumie watu hawa kuwapelekea maji maana hata ukichimba visima Mirefu huwezi kupata maji sehemu yenye madini.